Wachezaji sita waliotawala mashindano ya Kombe la dunia.

g

Argentina inakabiliana na Ufaransa katika fainali ya Kombe la Dunia Jumapili, huku Lionel Messi na Kylian Mbappe wakionekana kuwa ndio wachezaji wanaoongoza katika timu za mataifa yao katika kipindi chote mwezi mmoja uliopita wa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Je shindano hilo litakumbukwa kama 'Kombe la Dunia la Messi', huku Muargentina huyo akiinua hatimaye akiinua kombe , au Mbappe ambaye ameongoza mafanikio ya ushindi wa Ufaransa baada ya miaka minne nchini Urusi?

BBC Michezo inawaangazia wachezaji sita wengine waliokuwa muhimu katika kuleta mafanikio yan chi zao katika miaka iliyopita:

1: Pele, Brazil – 1958

G

Pele alikuwa na umri wa miaka 17 wakati Brazil ilipokwenda kwenye shindano la Kombe la Dunia la mwaka 1958 nchini Sweden, ikitaka kushinda shindano hilo kwa mara ya kwanza. Katika mechi mbili za ufunguzi mshambuliaji huyo ambaye alikuwa mshambuliaji wakati huo alifanikiwa kufunga magoli 2-0 dhidi ya Muungano wa Usovieti na akashinda bao la ushindi 1-0 dhidi ya Wales katika robo fainali.

Kuanzia wakati ule Pele hakurudi nyuma. Alifunga magoli matatu katika nusu fainali wakati timu yake ilipoilaza Brazil 5-2 na mabao mawili zaidi katika mechi ya fainali iliyomalizika kwa ushindi wa 5-2 dhidi ya Sweden – likiwemo goli alilofunga baada ya ‘kumvisha kanzu’ mlinzi kwa goti na kicha kuuweka mpira wavuni.

Huo ulikuwa ni mwanzo wa mataji matatu ya Kombe la Dunia kwa Pele, ingawa alicheza mechi mbili tu za ufunguzi katika mwaka 1962, kabal aya kupata jeraha lililomuondoa katika shindano.

Katika mwaka 1970 hata hivyo alikuwa katika ubora wake zaidi, ambapo alifunga mara nne – ikiwa ni pamoja na goli la kwanza la Brazil katika ushindi wa mabao 4 -1 dhidi ya Itali katika mechi ya fainali.

 2: Mario Kempes, Argentina - 1978

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kombe la dunia 2014: Argentina iliivunja mioyo ya Waholanzi mwaka 1978

Argentina imeshinda kombe la Dunia mara mbili, na katika nyakati zote , mchezaji amekuwa na nafasi kubwa katika ushindi. Katika mwaka 1978, katika ardhi ya nyumbani, alikuwa ni Mario Kempes.

Mshambuliaji huyu wa Valencia alikwenda katika shindano hilo akiwa ndiye mchezaji aliyefunga magoli zaidi katikaLa Liga katika misimu miwili ya mafanikio na alikuwa ndiye mchezaji pekee wa kikosi cha ambaye hakuwa anacheza soka ndani y anchi hiyo.

Kempes alishindwa kufunga bao katika awamu ya kwanza ya kundi, lakini katika awamu ya pili aling’ara kwa magoli yote ushindi wa 2- 0 dhidi yya Poland, na la kwanza , la pili na la tatu katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Peru.

Ushindi huo uliipelea Argentina katika fainali na Kempes alitingsha wavu mara mbili zaidi, katika ushindi wa timu yake wa 3-1 dhidi ya Uholanzi katika Buenos Aires. Hakuisaidia nchi yake tu kupata mafanikio, bali pia alikuwa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika shindano na mchezaji bora.

3: Paolo Rossi, Italia – 1982

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Alipokwenda katika Kombe la Dunia la 1982 la Uhispania, mshambuliaji wa Italia Paolo Rossi ndio alikuwa tu amerejea kimchezo baada ya kuwekewa marufuku ya miaka miwili kutokana na mchango wake katika Sakata ya mechi ya kupangwa katika Serie A, na meneja wa taifa hilo Enzo Bearzot alikosolewa na vyombo vya habari kwa kumchangua kushiriki Kombe la Dunia.

Lakini baada ya kuanza kwa mchezo duni, mshambuliaji huyo alifunga mabao matatu katika mechi na Brazil na hivyo kuiwezesha nchi yake kushinda na kufikia robo fainali. Baada yah apo aliipatia mabao yote mawili ya ushindi wa 2-0 kwenye nusu fainali , ulioiondoa Poland kwenye shindano, na kufunga bao la kwanza katika mechi ya ushindi wa Italia wa 3 -0 dhidi ya Ujerumani Magharibi .

Magoli sita ya Rossi yalimuwezesha kupata taji la Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot) akiwa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika shindano na taji la Mpira wa Dhahabu (Golden Ball ) kwa kuwa mchezaji bora wa shindano.

4: Diego Maradona, Argentina - 1986

G

Nahodha Diego Maradona aliongoza kwa mfano katika mwaka 1986 alipoisaidia Argentina kushinda Kombe la pili la Dunia katika shindano lililopigwa nchini Mexico. Goli la kwanza alilifunga dhidi ya Italia katika droo ya 1-1 ambayo iliisaidia Argentina kuwa mshindi katika kundi lake.

Katika robo fainali, alifunga mara mbili na hivyo kufanikiwa kuiengua England kwa 2-1. Goli la kwanza lilikuwa maarufu kwa jina 'Hand of God' - wakati Maradona alipoupiga mpira ulioompita Peter Shilton – lakini la pili linafahamika kama moja ya mashambulio bora zaidi ya Kombe la Dunia kuwahi kushudiwa , kwani alichukua mpira , kabla ya kuuvusha juu ya kichwa cha mlizi wa England na kumpiga Shilton.

Baada ya hapo alifunga magoli mawili bora katika nusu fainali ambapo timu yake ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Ubelgiji, hala pia alikuwa kiungo muhimu katika mechi ya fainali walipoichapa Ujerumani Magharibi 3-2.

Akiwa na magoli matano na kusaidia ushindi wa magoli mengine matano,Maradona alikaribia kuwa mshindi wa taji la Golden Ball kwa kuwa mchezaji bora wa shindano

5: Zinedine Zidane, Ufaransa – 1998

Kiungo wa kati mahiri Zinedine Zidane alikuwa ni mchezaji aliyeonyesha ubora zaidi katika Kombe la Dunia la Ufaransa la 1998 kwa timu ya Ufaransa , ambalo Ufaransa ililipokea.

Alikuwa na mwanzo mzuri kwa kusaidia nchi yake kufunga bao la kwanza la shindano, lililofungwa na Christophe Dugarry katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Afrika Kusini.

Zidane wakati ule alikuwa kiungo muhimu wakati walipoishinda Saudi Arabia , lakini baadaye wakawaondoa kwa ushindi wa 4-0 na kukosa katika mechi ya kundi la tatu ya Ufaransa dhidi ya Denmark, pamoja na ushindi wa 1-0 wa kipindi cha ziada dhidi ya Paraguay katika timu 16 za mwisho.

Lakini alirejea kwa mbwembwe, ambapo alifunga bao la mchwaju wa penati lililowaondoa Italia katika robo fainali na kisha akasaidia timu yake kufunga 2-1 katika nusu fainali dhidi ya Croatia.

Katika fainali, Zidane alifunga mabao mawili kwa kichwa katika ushindi wa Ufaransa wa 3-0 dhidi ya Brazil, na mchezo wake uliipatia nafasi ya juu timu yake katika shindano. Miaka miwili baadaye, alitajwa kama mchezaji bora wa Ulaya 2000, ambapo Ufaransa pia ilishinda taji la Euro.

g

Chanzo cha picha, AFP

Kiungo wa kati mahiri Zinedine Zidane alikuwa ni mchezaji aliyeonyesha ubora zaidi katika Kombe la Dunia la Ufaransa la 1998 kwa timu ya Ufaransa , ambalo Ufaransa ililipokea.

Alikuwa na mwanzo mzuri kwa kusaidia nchi yake kufunga bao la kwanza la shindano, lililofungwa na Christophe Dugarry katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Afrika Kusini.

Zidane wakati ule alikuwa kiungo muhimu wakati walipoishinda Saudi Arabia , lakini baadaye wakawaondoa kwa ushindi wa 4-0 na kukosa katika mechi ya kundi la tatu ya Ufaransa dhidi ya Denmark, pamoja na ushindi wa 1-0 wa kipindi cha ziada dhidi ya Paraguay katika timu 16 za mwisho.

Lakini alirejea kwa mbwembwe, ambapo alifunga bao la mchwaju wa penati lililowaondoa Italia katika robo fainali na kisha akasaidia timu yake kufunga 2-1 katika nusu fainali dhidi ya Croatia.

Katika fainali, Zidane alifunga mabao mawili kwa kichwa katika ushindi wa Ufaransa wa 3-0 dhidi ya Brazil, na mchezo wake uliipatia nafasi ya juu timu yake katika shindano. Miaka miwili baadaye, alitajwa kama mchezaji bora wa Ulaya 2000, ambapo Ufaransa pia ilishinda taji la Euro.

6: Ronaldo, Brazil – 2002

Fainali ile ya 1998 ilitarajiwa kuwa kipindi bora zaidi kwa mshambuliaji wa Ronaldo. Hatahivyo alipata mshituko wa ubongo kabla ya mechi na hakutajwa miongoni mwa wachezaji – lakini aliingia , uwanjani , na hakuleta athari yoyote katika mchezo ambao walishindwa na Ufaransa 3-0.

Jeraha baya alilolipata mwaka 1999 lilitishia kukatiza ndoto ya kazi yake ya soka, lakini kilichofuatia kilikuwa ni mojawapo ya hadithi za wachezaji bora zaidi waliotoweka na kurejea tena uwanjani.

Katika shindano la mwaka 2002 la Korea Kusini na Japan, Ronaldo aling’ara baada ya kuaacha nyuma masaibu ya miaka minne ya kiafya , akifunga mabao manane katika mechi saba.

Alipata magoli manne katika mechi za tatu za kundi - moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Uturuki, Lingine katika ushindi wa 4-0 dhidi ya uchina na magoli mengine mawili katika ushindi wa chee wa 5-2 dhidi ya Costa Rica. Halafu likaja goli moja katika ushindi wa 2-0 katika timu 16 dhidi ya Ubelgiji, goli pekee katika ushindi wa nusu fainali wa 1-0 dhidi ya uturuki na magoli yote mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ujerumani katika fainali.

Ronaldo alikuwa mchezaji aliyeshinda magoli mengi zaidi na hakuna mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi yake katika Kombe la Dunia hadi sasa , ingawa Messi na Mbappe wanaweza kufanya hilo katika mwaka huu.