Je, supu ya kuku inaweza kutuliza mafua?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuanzia juisi ya machungwa hadi vimumunye vya zinki, supu ya kuku hadi tembe za kitunguu saumu, kuna dawa nyingi za kujitibu ukiwa nyumbani. Lakini kuna ushahidi kuwa dawa hizo zinakabiliana na mafua kikamilifu?
Kupatwa na mafua ni kawaida ,ikiwa ni takriban virusi 200 vinavyosababisha hali hii.
Ingawa kuna tiba za nyumbani zilizopo, ufanisi wake hutegemea sana kupiga jeki kingamaradhi.
Kingamaradhi hupigana na virusi kwa kutumia kinga mbili kuu: mfumo wa kinga wa asili na mfumo wa kinga wa mabadiliko, ambao hujenga seli za kumbukumbu kwa ajili ya kukabiliana na virusi baadaye.
Tofauti na tetekuwanga, virusi vya mafua hubadilika, hivyo unaweza kuipata mara nyingi.
Inaaminika kuwa mtindo wa maisha na wa chakula huathiri mfumo wa kingamaradhi.
Lakini ni zipi tiba za nyumbani unazoweza zikumbatia ili kukabiliana na mafua?
Je, virutubisho kama vile kitunguu saumu vinaweza kupigana na virusi?
Lakini kingamaradhi hupungua hasa kwa watu walio na afya nzuri wakati viwango vya virutubisho au vitamini vikipungua kuzidisha kutumia vitamini ambazo zinaaminika kupiga jeki homa hakutasaidia chochote, anasema Charles Bangham, mkuu wa divisheni ya magonjwa yakuambukizana katika chuo kikuu cha Imperial mjini Uingereza.
"Lishe bora ni muhimu, na virutubisho vinaweza kusaidia tu kama kuna upungufu wa vitamini au madini fulani, kama vile zinki au vitamini C.
Ingawa hakuna ushahidi madhubuti kwamba tiba kama supu ya kuku inasaidia, tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa multivitamini zinaweza kupunguza dalili za mafua.
Utafiti mdogo pia uligundua kwamba virutubisho vya vitunguu vinaweza kusaidia kupunguza makali ya mafua.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je vitamini C husaidia kutibu mafua?
Virutubisho vingine vingi watu hutumia wanapohisi dalili za mafua ni Vitamini C.
Utafiti wa 2023 uligundua kuwa virutubisho vya vitamini C vinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa ukali wa dalili za mafua kama homa ya pua, kikohozi, na maumivu ya koo kwa karibu asilimia 15%.
Utafiti mwingine pia ulisema virutubisho hivi vinaweza kusaidia zaidi na dalili kali za baridi.
Hata hivyo, juisi ya machungwa inaweza kuwa na manufaa kidogo: hakuna ushahidi thabiti kwamba juisi ya machungwa inazuia mafua, inapunguza dalili au inapunguza muda wa kuugua mafua.
Hii ni kwa sababu haijazidi viwango vya vitamini C vinavyohitajika kama virutubisho vya kila siku.
Chupa ndogo ya juisi ya machungwa ina karibu 72mg ya vitamini C, ambayo ni zaidi ya kiwango cha chini kinachoshauriwa cha 40mg, lakini bado kidogo kuliko virutubisho vingi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, madini ya zinki inasaidia kutibu mafua?
Zinki pia ni tiba inayotumika kupunguza makali ya mafua.
Utafiti mmoja ulionyesha kuwa vidonge vya zinki (zilizo na 80-92mg) hupunguza muda wa dalili za mafua kama homa ya pua kwa takriban theluthi moja, huku ikipunguza kikohozi na kupiga chafya kwa asilimia 22%.
Utafiti ulionyesha kuwa matumizi ya vidonge vya zinki gramu 80 kwa siku, ikiwa vinatumiwa ndani ya saa 24 tangu dalili za kwanza, vinaweza kusaidia kutibu mafua.
Hata hivyo, tafiti nyingine zimeonyesha kuwa kipimo na muda wa matibabu ni muhimu.
Utafiti wa 2020 ulionyesha kuwa vidonge vya zinki nusu gramu 72 vilivyotumika kwa siku tano hazikuathiri kasi ya uponaji wa mafua.
Wale waliotumia dawa za kutuliza mafua katika siku mbili baada ya majaribio.
Watafiti wanasema kwamba matokeo haya hayathibitishi ukosefu wa ufanisi, na utafiti zaidi unahitajika kubaini kama kipimo kikubwa au muda mrefu wa matibabu kunaathari.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mara nyingi, wanasayansi wanasema vitamini na madini ni bora zaidi vikiambatana na vyakula tunavyokula ikilinganishwa na kula virutubisho - lakini ni bora zaidi ukila vitamini C kama virutubisho ili kuongeza viwango vyake haraka mwilini.
Kwa madini ya zinki ni tofauti.
Ili madini ya zinki yakusaidie kupambana na mafua, pendelea kutumia vimumunye vya zinki na sio vidonge vya zinki ama ule vyakula vilivyo na madini ya zinki, anasema Hemila.
"Vimumunye vya Zinki huyeyushwa polepole katika eneo la koo na athari ya zinki ni ya ndani," anasema. "Hatujui utaratibu wa biokemikali wa athari hii ni nini.
Lakini tafiti za kupata vimumunye vya zinki kuwa bora zilitumia vipande vikubwa vya vimumunye ambazo zimeyeyuka kwa hadi dakika 30 mdomoni."
Athari ya dawa za kipozauongo kwa mafua
Bado, tatizo moja ni kwamba watafiti hawakuwa na mwelekeo wa kuangalia kama watu walikuwa na upungufu wa kitu kama vitamini C au zinki kabla ya kuanza kanuni za mlo.
Kwa hiyo, faida yoyote ya kupambana na mafua inaweza kuwa wagonjwa wengine walikuwa wakirekebisha upungufu wa madini, badala ya virutubisho kuongeza kinga mwilini kwa watu wenye afya.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tatizo lingine ni nguvu ya dawa za kutuliza maumivu.
Ingawa tafiti nyingi, kama ile ya virutubisho vya vitunguu, hutumia kundi la dawa ya kupozauongo ili kupima athari, kuna baadhi ya vitu, kama supu ya kuku au juisi ya machungwa, ambavyo tunaamini vinatufaa licha ya kukosa ushahidi wa kisayansi.
Dawa ya kipozauongo imeonekana kusaidia kupunguza dalili nyingi, kama maumivu na ugonjwa wa tumbo, ingawa sababu hazieleweki vizuri. Kwa hiyo, athari ya dawa za kupozauongo zinaweza kusaidia kutuliza mafua.
Utafiti mmoja uligundua kuwa watu waliyoamini katika manufaa ya mmea wa echinacea walipona haraka zaidi kuliko wale waliyoamini kuwa haifai.
Hata hivyo, tafiti nyingine hazikuonyesha mabadiliko yoyote kwa wale waliotumia mmea wa echinacea bila kujua.
Hali hii pia inaathiriwa na imani za watu; kwa mfano, imani kwamba maziwa husababisha utezi wa pua iligundulika kwa wale waliyoamini hivyo.
Athari ya dawa ya kipozauongo inaweza kuimarishwa na uhusiano wa kuaminiana kati ya mgonjwa na mtaalamu wa afya, au hata kwa imani za familia na marafiki.
Wataalamu wanasema kuwa dawa ya kipozauongo inaweza pia kusaidia, hata wakati mtu anajua kuwa hana chochote ni dawa ya kipozauongo, ikiwa imetumika kwa uaminifu.
Kwa watu wengi wenye mifumo ya kinga ya afya, tunaweza kutegemea nguvu ya kipozauongo kupambana na virusi vya majira ya baridi, ingawa virutubisho vya zinki au vitunguu vinaweza kusaidia pia.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid












