Kula ngozi ya nyama ya kuku kuna madhara gani?

Kuku

Kuku ni miongoni mwa nyama ambayo hupendwa sana duniani.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linakadiria kuwa mwaka 2021 tani milioni 133 za nyama ya kuku ililiwa duniani.

Ulaji wa nyama kuku ni maarufu kwa sababu ni wa bei nafuu, ina mafuta kidogo, na inakabiliwa na vikwazo vichache vya kitamaduni au kidini.

Aidha, ni nyama yenye protini nyingi na chanzo muhimu cha vitamini na madini. Na pia ina viwango muhimu vya mafuta yenye faida, ambayo yanaweza kusaidia afya ya moyo na mishipa.

Lakini, chakula hiki maarufu sana pia kinaonekana kuzungukwa na mashaka na idhana tofauti.

Kwa mfano, ngozi ya kuku inajulikana kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta. Kwa hivyo, ni vizuri kula kuku na ngozi au tunapaswa kuiondoa kabla ya kuanda kitoweu murua?

"Ngozi ya kuku ina asilimia 32 ya mafuta yaani, kwa kila gramu 100 za ngozi tunayokula, gramu 32 ni mafuta," María Dolores Fernández Pazos, mtaalamu wa lishe katika Kituo cha Taarifa za Lishe ya Nyama, aliambia BBC Mundo.

Kati ya mafuta haya yaliyomo kwenye ngozi ya kuku, anaelezea mtaamu, theluthi mbili ni mafuta yasiyo na madhara, kile kinachoitwa "mafuta mazuri", ambayo husaidia kuboresha viwango vya damu.

Na theluthi moja ya mafuta ndio ambayo huchangia kuongeza viwango vya mafuta "mbaya" katika mwili wa binadamu.

Mwnamke anakula kuku

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hiki ni kiwango sawa cha mafuta kinachopatikana kwenye nyama ya kuku. Kwa hiyo, anasema mtaalam, "ikiwa tunakula kuku na ngozi, tutaongeza ulaji kiwango cha kalori mwilini kwa takriban 50% ".

Kwa hivyo, kwa mfano, ikiwa tutakula kipande sita vya nyamaya kuku isio na ngozi, tutakuwa tunatumia kalori 284 (kulingana na data ya lishe ya Idara ya Kilimo ya Marekani), huku 80% ya kalori ikitoka kwa protini na 20% kutoka kwa mafuta.

Lakini nambari hizo huongezeka sana ikiwa tunajumuisha ngozi: sehemu ya kifua cha kuku itakuwa na kalori 386, na 50% kutoka kwa protini na 50% ya mafuta.

Kwa hivyo, mtaalamu wa lishe Dolores Fernández anapendekeza, kuondoa (ngozi) kabla ya kula, ili kutoongeza kalori au mafuta zaidi kwenye sahani."

"Kwa watu ambao hawana historia ya ugonjwa, na uzito wa kutosha kwa urefu wao, muundo wa mwili, tunaweza kupendekeza kuacha ngozi ya kuku wakati wa kupikia na kuiondoa kabla ya kula, kwa kuwa uwepo wa ngozi wakati wa kupikia utasaidia nyama kukauka kidogo na kuwa na ladha tamu zaidi," anasema mtaalam.

Kuku choma

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, ni sawa kugandisha tena nyama ya kuku aliyoyushwa?

"Hapana. Haipendekezwi kugandisha tena nyama ya kuku ambayo imeyeyushwa," anasema mtaalamu wa lishe wa CINCAP.

"Lengo la kugandisha chakula ni kuzuia ukuaji wa vijidudu kwenye chakula. Kwa hivyo kwa kuyeyusha chakula, vijidudu hivyo vinaweza kuanza kukua tena."

Na huu ni ushauri ambao unatumika kwa nyama zote ambazo zimeyeyushwa.

Njia pekee ambayo ni salama kugandisha tena nyama iliyoyeyushwa barafu ni baada ya kupikwa.

"Kwa kutumia njia hii, tutaondoa uwepo wa vijidud na tunaweza kugandisha tena nyama," anasema Dolores Fernández.

Nyaka ya kuku

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni ipi njia bora ya kuyeyusha kuku?

Njia bora ya kuyeyusha kuku, wataalam wanasema, iko kwenye jokofu.

"Kupunguza baridi hadi joto la kawaida kunaweza kuongeza ukuaji wa vijidudu ambavyo tulitaja hapo awali na kuharibu bidhaa."

Kwa kuwa kuyeyuka kwenye okofu kutakuwa polepole, inaweza kuchukua kama masaa 24 kwa kuku mzima. Lazima tupange mapema wakati mzuri wa kutoa nyama ya kuku kutoka kwenye jokofu.

Wataalamu wanasisitiza kwamba nyama ya kuku haipaswi kamwe kuyeyushwa kwenye joto la kawaida au katika maji ya moto.

Jinsi ya kuepuka sumu na nyama ya kuku?

Kuku, kama tunavyoona, ni moja ya chakula bora zaidi, maarufu na kinachotumiwa sana duniani, lakini pia mara nyingi ni chanzo kikuu cha sumu ya chakula.

Nyama mbichi ina bakteria aina ya Campylobacter na pia, mara kwa mara huwa na Salmonella na Clostridium perfringens.

Ndio maana ukila kuku ambaye hajaiva vizuri au ukichafua vyakula au vinywaji vingine na kuku mbichi au juisi zake unaweza kupata sumu kwenye chakula.

Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vinakadiria kwamba kila mwaka nchini Marekani karibu watu milioni moja huugua kutokana na kula nya ya kuku iliyo na vijidudu hatari.

Hivi ni vidokezo vya msingi kutoka kwa mtaalamu katika Kituo cha Taarifa za Lishe ya Nyama ya Kuku:

  • Nawa mikono yako kabla ya kuandaa aina zote za chakula na mara kadhaa wakati wa maandalizi yake, hasa ikiwa vyakula vibichi na vilivyopikwa vinaandaliwa kwa wakati mmoja.
  • Unapoandaa kuku na vyakula vingine vibichi, tumia vifaa na vyombo tofauti, na epusha kugusana kwa vyakula vilivyopikwa vile vilivyo tayari kuliwa.
  • HATUpaswi kamwe kuosha nyama ya kuku, kwani hii inaweza kusababisha, pamoja na chembe za maji zinazomwagika, kuchafua mahali pa kazi.
  • Pika nyama ya kuku vizuri: Hakikisha nyama imeiva vizuri upande wa ndani au karibu na mifupa na viungo.
  • Ikiwa una mabaki ya kuku kutoka kwenye mlo mmoja na unataka kula wakati ujao, pasha moto upya.