Ni nini kitatokea endapo watoto wataachwa wakilia?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mafunzo ya kulala ni mkakati wowote unaotumiwa na wazazi kuwahimiza watoto wao kulala usiku - inaweza kuwa rahisi utaratibu maaalum wa usiku ukifuatwa kama vile kujua jinsi ya kugundua dalili za uchovu wa mtoto mchanga.
Mbinu hii ya kumfunza mtoto mchanga kulala bila mzazi kuwa karibu inajumuisha: wakati wa kuamka usiku au mzazi kujidhibiti ni wakati gani anafaa kumchukua mtoto akianza kulia.
Hii inamaanisha mzazi hata akiwa karibu anatakiwa kujizuia kumbeba mtoto na kumbembeleza.
Inaweza kuhusisha vipindi vya muda vilivyowekwa ambapo mtoto huachwa peke yake.
Pia inaweza kumaanisha kumuacha mtoto na kufunga mlango. Mbinu hizi zote mbili mara nyingi humaanisha kuruhusu mtoto kulia - hadi anyamaze mwenyewe na kulia".
Katika nchi nyingi , wazo la "kuwafunza" watoto wachanga kulala wenyewe bila kusaidiwa sio jambo la kawaida.
Katika baadhi ya nchi kinamama wanashtuka sana wanaposikia kwamba nchini Marekani, watoto wachanga walilazwa katika chumba tofauti.
Lakini katika maeneo ya Amerika ya Kaskazini, Australia na sehemu za Ulaya, baadhi ya familia zinaapa kutafuta mbinu ambazo zinaweza kuwasaidia watoto wao wachanga kulala wenyewe bila kubembelezwa.
Wazazi wako tayari kuwapa mafunzo ya kulala watoto wao wachanga hasa kilio cha usiku kinapoanza kuathiri ustawi wa familia nzima.
Kuna baadhi ya wazazi wanachukulia "mafunzo ya kulala" kama ufunguo wa kupumzika vizuri usiku huku wengine wakihofia huenda yakawa na athari kwa watoto.
Lakini je wataalamu wanasema nini kuhusu hatari na faida zake?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbinu ya mtoto "kuachwa kulia" ilianzaje?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
BBC imebaini kuwa kabla ya karne ya 19, wazazi walio na watoto wachanga hawakujali sana usinizi wa watoto wao wachanga.
Hili limebadilika kwasababu mapinduzi ya kiviwanda yalikuja na siku ndefu za kufanya kazi na kama uhuru ulivyosisitizwa katika enzi ya Victoria, hata watoto walijumuishwa.
Mwaka 1892, mtaalamu wa masuala ya watoto "baba wa watoto", Emmett Holt, alisema mtoto mchanga kuachwa kulia kuna manufaa kwake: "kwa mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, kilio hupanua mapafu", aliandika katika kitabu chake cha The Care and Feeding of Children kinachoangazia masuala ya ulezi.
''Mtoto anastahili 'kuachwa kulia' hadi anyamaze mwenyewe. Hii inatakiwa iwe kwa angalau saa moja, na ikizidi sana iwe kwa kati ya saa mbili hadi tatu.
Hata hivyo kufikia miaka ya 1980, ndipo ''mpango'' wa watoto kuachwa kulia ulianzishwa rasmi.
Mwaka 1985, Richard Ferber alitetea kile alichokiita "kilio kinachodhibitiwa" au "njia ya kumuacha na kutoweka", kuruhusu mtoto alie kwa muda mrefu zaidi. (Baadaye alisema alikuwa ameeleweka vibaya na kusisitiza kwamba hakupendekeza njia hii kwa kila mtoto ambaye halala vizuri.)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo 1987, Marc Weissbluth alishauri kumweka tu mtoto mchanga kwenye kitanda chake cha kulala na kufunga mlango - unaoitwa "kutoweka''.
Baadhi ya watafiti ambao walipendekeza njia hizi za kulala kwa watoto wachanga walisema kufanya hivyo kabla hawajafikisha miezi sita- ni makosa.
Pia wanasema hawapendekezi mafunzo ya usingizi kwa watoto ambao wameathiriwa kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na watoto ambao wamepata kiwewe.












