Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Faida za kiafya za pombe ya mnazi
Pombe ya mnazi , inayojulikana kwa majina kadhaa ya kienyeji, ni kinywaji chenye kileo kilichoundwa kutokana na utomvu wa aina mbalimbali za mitende na minazi.
Inajulikana kwa majina mbalimbali katika maeneo tofauti na ni ya hutumika sana katika sehemu mbalimbali za Afrika, maneo ya carebean, Amerika ya Kusini, Asia ya Kusini, Asia ya Kusini-Mashariki na Mikronesia.
Uzalishaji wa pombe hiyo unaofanywa na wakulima wadogo na wakulima binafsi unaweza kukuza uhifadhi kwani mnazi unakuwa chanzo cha mapato ya kawaida ya nyumbani ambayo yanaweza kuwa na thamani ya kiuchumi zaidi ya thamani ya mbao zinazouzwa.
Inaitwa nekta ya miungu. Kinywaji bora, na hupewa sifa kulingana na aina ya sherehe. Nyimbo zimeimbwa kuihusu na zote ni za furaha.
Kutoka kutangaza kuzaliwa kwa mtoto mpya hadi kilio cha maombolezo, kinywaji hicho kimesifika katika sherehe tofauti na kwamba hutumika wakati wote.
Pombe hiyo ni maarufu katika mataifa mengi ya Afrika mashariki ikiwemo Tanzania na Kenya na magharibi mwa Afrika ikiwemo Nigeria, Ghana na cameroon. Pombe hii asilia pia imezungukwa na simulizi chungu nzima pamoja na hadithi na imani nyingi.
Sukari yake husababisha uchachushaji wa haraka ambao huongeza kiwango cha pombe baada ya saa 2 tu.
Faida za kiafya za pombe ya mnazi mara nyingi hupatikana kaytika simuzlii za kale: Hivyobasi tunaenda kutenganisha ukweli na uwongo.
Pombe ya mnazi ina protini, wanga, amino asidi, vitamini kama vile B3 na C, na madini kama vile zinki na magnesiamu.
Harrison Omonhinmin, mtaalamu wa lishe aliyeidhinishwa, anaeleza kuwa kufuatia utafiti uliofanyika mwaka 2014 wa kutathmini maudhui ya antioxidant ya pombe hiyo ikilinganishwa na vinywaji vingine, Pombe hiyo iliorodheshwa ya mwisho kwa kuwa na upungufu wa vitamini C na antioxidants nyingine.
Lakini usiache glasi hiyo ya mnazi kwa sasa, wacha tuzungumze juu ya faida zake za kiafya.
Ni nzuri kwa sukari yako ya damu!
Kulingana na Omonhinmin, Pombe ya mnazi ina kiwango cha chini cha glycemic, ikimaanisha haipandishi kwa kasi viwango vya sukari ya damu.
Glycemic ni neno linalotumiwa kufafanua muda unaochukuwa kwa viwango vya sukari ya damu kupanda.Ikilinganishwa na vinywaji vingine vya sukari, Pombe ya mnazi ni bora kwa wagonjwa wa kisukari.
Huu sio ulafi, lakini Omonhinmin anapendekeza glasi moja kwa siku kwa wanawake na mbili kwa siku kwa wanaume.
Husaidia macho
Collins Akanno, mtaalamu wa lishe ya jamii, anafichua kwamba Pombe ya mnazi ni chanzo kizuri cha vitamini A, B1, B2 na C. Anaeleza kuwa vitamini hizi husaidia kuzuia kuzorota kwa misuli.
Anaongeza kuwa kinywaji kina madini ya potasiamu ambayo husaidia kuweka macho unyevu na kupunguza mkazo wa macho."
Kupambana na saratani
Bw. Akanno anasema kwamba maudhui ya antioxidant katika Pombe ya mnazi husaidia mwili kuzuia viini kutoka kwenye kuharibu seli mwilini na kusaidia kupambana na saratani.
Anaeleza kuwa "kwa mfano, vitamini B2 (Riboflauini) husafisha glutathione ambayo ni antioxidant muhimu zaidi ambayo hulinda dhidi kuharibu seli mwilini."
Kuimarisha afya ya moyo
"Ikiwa unatafuta chanzo kizuri cha kinywaji ili kusaidia kupambana na ugonjwa wowote wa moyo na mishipa, basi unaweza kuhitaji kunywa Pombe ya mnazi ," Collins Akanno.
Akanno anaamini kwamba lengo la madini ya potasiamu katika Pombe hiyo husaidia neva na misuli kufanya kazi vizuri na kwamba mishipa hii yenye joto na misuli huhakikisha mapigo mazuri ya moyo, ambayo hupunguza shinikizo la damu.
Kinywaji cha kuongeza nguvu mwilini
Kulingana na Omonhinmin, uwepo wa wanga katika pombe ya mnazi husaidia kuweka nguvu katika mwili wa binadamu.
Unatafuta ngozi nyororo na safi?
Unachohitaji kufanya ngozi laini, na nywele zenye afya hupatikana kwenye Pombe ya mnazi.
Akanno anasema kuwepo kwa vitamini, zinki na magnesiamu katika Pombe hiyo kunaifanya kuwa chakula ambacho wataalam wa ngozi na nywele wanapaswa kuzingatia.
Imani kuhusu Pombe ya mnazi
Je Pombe ya mnazi ni nzuri kwa mama anayenyonyesha?
Si kawaida kusikia mapendekezo ya Pombe ya mnazi iliopozwa kuwasaidia akina mama wanaonyonyesha.
Hata hivyo, Omonhinmin anasema hakuna msingi wa kisayansi wa madai haya na kufafanua kuwa kinywaji hicho kina pombe na akina mama wanaonyonyesha wanashauriwa kutokunywa pombe.
Je, Pombe ya mnazi husababisha vidonda tumboni?
Licha ya ukweli kwamba kinywaji hicho kina karibu 5% ya pombe, Collins Akanno anasema hakisababishi vidonda.