Mambo 3 yanayoweza kukuepusha mabishano yanayoweza kugeuka kuwa ugomvi

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Kutokubaliana ni sehemu isiyoweza kuepukika ya kuwa mwanadamu, kwani binadamu sote hatuko sawa.

Lakini kuna wakati kutokubaliana kidogo kunaweza kunakotokea katika mazungumzo ya kawaida au kupitia ujumbe wa simu au katika maandishi ya kawaida, au majadiliano ya ana kwa ana juu ya mada nyeti kunaweza kugeuka kuwa uhasama mkubwa au ugomvi.

Huenda umepitia hili wakati wa likizo, wakati wengi wetu tulitumia muda mwingi kuliko kawaida kuwasiliana kwa karibu na familia zetu. Hii wakati mwingine inaweza kuleta mvutano wa siri .

Mabishano au malumbano yanaweza kuanza kwasababu nyingi, kuanzia siasa hadi tabia ya nyingine, kitu ambacho mtu yeyote anayetumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii atafahamu.

Lakini kadiri maoni yanavyokuwa na makali ndivyo majadiliano yanaweza kuwa makali na magumu zaidi.

Kwahivyo unaweza kufanya nini ili kuzuia mabishano madogo kugeuka kuwa malumbano na hata kugeuka kuwa uhasma mkubwa, iwe mtandaoni au ana kwa ana?.

Kama mtaalam wa mahusiano ya kijamii, ninaamini kuzingatia kile mtu mwingine anachosema - na jinsi anavyokisema - ni muhimu, pamoja na kujifunza jinsi ya kuepuka kujibu kwa njia ambazo zinaweza kkuathiri mtu mwingine.

Kumbuka kwamba kutokubaliana ni sehemu ya kawaida ya maisha na mahusiano. Lakini hapa kuna mambo matatu muhimu yanayoweza kukusaidia kuepuka malumbano yanayoweza kugeuka kuwa uhasama mkubwa:

1. Dhibiti mabishano

Ikiwa hukubaliani na mtu, fanya mazungumzo yawe na tija kwa kuepuka matusi ya moja kwa moja. Pia, jaribu kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kumuweka mtu mwingine katika hali ya makabiliano zaidi, kama vile mashtaka, malalamiko, au kejeli.

Sisi huwa tunaweka mkazo mkubwa juu ya yaliyomo kwenye hoja, na pia juu ya mawazo yetu juu ya kile mtu mwingine "anafikiria kweli."

Hoja inahusu nini? Ni kutokuelewana tu, au ni suala la utu, na mtu mmoja ana upendeleo au kuwa na nia mbaya?

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuongezeka kwa mitandao ya kijamii kumebuni majadiliano yasiyo na mwisho.

Tunajali sana ikiwa mtu anaamini kweli kile anachosema. Uchunguzi unaonyesha kwamba mara nyingi tunachukia watu "wasiokuwa na upande " katika mazungumzo fulani.

Lakini haiwezekani kujua nia ya mtu mwingine, kwa hivyo ni bora kuepuka kudhani mbaya zaidi juu ya mtu unayegombana naye.

Vinginevyo, unaweza kuzungumza nao isivyo haki kana kwamba ni wadanganyifu, wasio wa haki, wenye madhara, au wasiojali.

Uwe tayari kusikiliza maoni ya wengine

Wakati mwingine, kile mtu anachosema kinaweza kinaweza kusikika vibaya sana sana. Wakati hii inatokea, kumbuka mambo mawili.

Kwanza kabisa, hakuna kitu tunachosema kina maana moja. Mara nyingi kuna tafsiri nyingi, na huwezi kutegemea ya kwanza inayokuja akilini wakati wa mabishano.

Wakati wa mabishano, inafaa kutulia na kuzingatia tafsiri zote zinazowezekana. Fikiria kuchukua muda kufikiria au kunywa kikombe cha chai ili kujiepusha kwanza na mvutano unaoendelea.

Pili, iwapo mtu anachosema bado kinasikika kuwa hasi upande wako, haijalishi unajaribu kuelewa kiasi gani, waombe waeleze zaidi. Huenda isiwe rahisi, lakini mara nyingi watu wataelewa walichomaanisha ikiwa watalazimika kufafanua.

Kuwasaidia kuhisi wanasikilizwa kunaweza kutuliza uhasama.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtu yeyote anaweza kujihusisha na mabishano

Zingatia muktadha wa mazungumzo

Kuna upande mwingine wa mazungumzo chagua unachosema kwa uangalifu na uzingatie kinachukuliwa vipi na unaozungumza nao. Mtu yeyote anaweza kujipata katika mabishano kwa kusema kitu ambacho atakijutia, ukiwemo wewe.

Jambo moja la kusawazisha kwa uangalifu ni kuwa na kipimo cha majadiliano unayokuwa nayo na jinsi unavyokuwa nayo.

Hii inaweza kuwa na tija ikiwa, kwa mfano, kuomba mazungumzo yazingatie kitu maalum. Hata hivyo, inaweza kufasiriwa kwa urahisi kama ukosoaji kamili wa mtu mwingine.

Ukiamua kushughulikia hoja uliyonayo, huenda ukahitaji kujumuisha kuomba msamaha au kuzungumza kwa sauti ya chini ili kuepuka mtu mwingine kufikiria kuwa utamshutumu kwa namna fulani ya mabishano "vibaya."

Ni changamoto, kwa hivyo usijisikie vibaya ikiwa hutaeleweka sawa mara ya kwanza unapojaribu mbinu hii.

Je, tuna maadili sawa?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Watu hawabishani kwa ajili ya kubishana. Moja ya sababu kuu zinazotufanya tubishane ni kujilinganisha na wengine. Je, tuko sawa na tunamaadili sawa?

Hoja pia zinahusishwa na utambulisho. Majadiliano yenye utata zaidi hutoa hisia kali. Tunafahamu kwamba tunaweza kulaumiwa kwa maoni yetu, na wengine watadhani kwamba tunaweza kuwalaumu.

Lawama za pande zote huweza kuongezeka na kuwa malumbano kwa urahisi, sio tu wakati wa mabishano, lakini katika uhusiano kwa ujumla, na kusababisha kuvunjika kwa muda kwa uhusiano au hata kupoteza urafiki. Watu ambao wanataka kuepuka hili mara nyingi hufikiri suluhisho ni kuweka hisia kando na "kuzingatia ukweli."

Lakini kukataa mwitikio wa kihisia kunaweza kuwa kama kukataa kujitolea kwako mwenyewe kwasababu inayofaa. Kutambua kwamba mtu anahisi hivi ni hatua muhimu katika kujua ni nini unachoweza kufanya kubadilisha mawazo yake kuhusu hisia hizo na ni hoja gani ya kuachana nayo, angalau kwa sasa.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi