Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 09.08.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joao felix
Muda wa kusoma: Dakika 3

Meneja wa Aston Villa Unai Emery anataka kumsajili mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 24, ambaye ana nia ya kuondoka Atletico Madrid. (BirminghamLive),

Liverpool wanaendelea kumtaka mshambuliaji wa England na Newcastle Anthony Gordon. Mpango wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 uliporomoka mwezi Juni na huenda bei ya Gordon ikapanda. (Liverpool Echo)

Real Madrid na Paris St-Germain wanamtazama mlinzi wa Chelsea Josh Acheampong, 18, kama chaguo linalowezekana la beki wa kulia. Mwingereza huyo ni mhitimu wa akademi ya Chelsea. (Independent)

Beki wa West Ham Kurt Zouma anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Shabab Al Ahli baada ya kuafikia makubaliano na Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 29. (Sky Sports)

pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Kurt Zouma

Maelezo ya picha, Kurt Zouma

Leicester wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Argentina na Brighton mwenye umri wa miaka 19 Facundo Buonanotte kwa mkopo. (Mail)

Real Sociedad wanajaribu kumshawishi mchezaji anayelengwa na Liverpool Martin Zubimendi kukataa kuhamia Anfield. Kiungo huyo wa kati wa Uhispania ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 51. (Times – Subscription Required)

Liverpool wamekataa ofa nyingi kwa mlinzi wa Uholanzi Sepp van den Berg, 22. Hoffenheim, Stuttgart, Wolfsburg, Mainz, Borussia Monchengladbach na Bayer Leverkusen zote zinavutiwa. (Sky Germany)

Brentford wamekubali mkataba wa mkopo, na kipengele cha kununua ambacho kinaweza kuwa cha lazima na cha thamani ya karibu £10m, ili kumsaini kiungo wa kati wa Uswidi Jens Cajuste, 24, kutoka Napoli. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Conor Ghallagher

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Valencia Miguel Angel Corona anasema Atletico Madrid ilijaribu kufuta uhamisho wake wa kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Conor Gallagher mwenye umri wa miaka 24 ili kutanguliza mpango wa kiungo wa kati wa klabu yake ya Uhispania Javi Guerra, 21. (Athletic – Subscription Required)

Birmingham City wamekubali mkataba na Rennes kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Wales Jordan James, 20. (Independent)

Marseille wana nia ya kumnunua mshambuliaji wa England na Arsenal Eddie Nketiah, 25. (Sky Sports)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nketia

Bournemouth wako kwenye mazungumzo ya hali ya juu na Barcelona ili kumsajili beki wa Mexico Julian Auraujo, 22, kwa mkataba wa euro 10m (£8.56m). (Fabrizio Romano)

Beki Mfaransa Billy Koumetio, 21, yuko mbioni kuhama kutoka Liverpool hadi Dundee. (Athletic – Subscription Required).

Fulham wameongeza hamu ya kumnunua beki wa Aston Villa, Diego Carlos. Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa na Villa iko tayari kwa ofa. (Telegraph – Subscription Required)

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla