Mbinu tano za kuzuia mshituko wa moyo

Madaktari wanaamini kwamba msongo wa mawazo unaweza kuathiri moyo, jambo linaloweza kusababisha matatizo mabaya zaidi ya kiafya, kama vile kiharusi na mshituko wa moyo.

 Tafiti zilizochapishwa katika miaka ya hivi karibuni zinaonyesha jinsi msongo wa mawazo unavyoathiri moja kwa moja moyo.

Habari njema ni kwamba sababu nyingi zinazoweza kusababisha matukio haya zinaweza kuzuiwa.

Daktari wa moyo aliyezungumza na BBC anasema kuwa udhibiti wa msongo wa mawazo, kulala usingizi wa kutosha, mazoezi na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa moyo vi hatua ambazo zinaweza kuzia mshituko wa moyo.

 Dkt Roberta Saretta,mkuu wa Kituo cha Moyo katika hospitali ya Sírio-Libanês katika mji mkuu wa Brazil São Paulo, Brazil, anaelezea kwamba matatizo makubwa hutokana na watu kushindwa kudhibiti msongo wa mawazo jambo ambalo huathiri pakubwa moyo.

 Wataalamu wa afya ya moyo waliiambia BBC kuwa kuna mambo Matano ambayo yanaweza kumsaidia mtu kuboresha afya yake ya moyo.

1 - Kudhibiti wasi wasi

Kwanza kabisa, ni lazima tutofautishe mambo tunayoweza kuyafanya na yale ambayo hatuwezi kuyafanya, matatizo tunayoweza kuyatatua na mambo tusiyoweza kuyatatua ", halafu tuelekeze mawazo yetu kwa yale tunayoweza kuyatatua au kuyabadilisha ," anasema Agnaldo Piscopo, daktari wa moyo.

Kulingana na daktari Piscopo, kuanza na uzoefu wa kuwa na utulivu na kutuliza mawazo yetu, ni jambo muhimu.

 Lengo la kuwa watulivu litatusaidia kuangazia hali tuliyonayo sasa na kuweza kufikiria kuhusu hali zilizopitaau hali zijazo.

 "Tuna ushahidi kuwa watu wanaokuwa na muda wa kufikiria mambo kwa utulivu (meditate) kuhusu katika hatua ya kushusha shinikizo la damu na viwango vya mapigo ya moyo, huweza kukabiliana vyema na msongo wa mawazo wa kila siku," alisema Poscop.

Daktari pia alisema kwamba ni muhimu kupunguza matumizi ya mitandao ya kijami na habari.

Piscopo alionya dhidi ya kuweka fikra zaidi katika mambo magumu, ambayo hayana suluhu.

2- Kupata usingizi wa kutosha

Kituo cha kudhibiti na kuzia magonjwa cha Marekani (CDC) kinasema kuwa na usingizi usiotosha nyakati za usiku kuna uhusiano na shinikizo la damu, kisukari aina ya 2 na unene wa mwili wa kupindukia – jambo ambalo huathiri moyo moja kwa moja.

Kwa ufupi, ukosefu wa usingizi wa kutosha huongeza mchoko wa mwili na husababisha mtu kukasirika kwa haraka. "Unaweza kuona kuwa iwapo hautapata usingizi wa kutosha, utahisi kuchoka zaidi na kukosa subra mara kwa mara’’, alisema Saretta.

 Kwa ujumla, watu wazima wanahitaji kulala usingizi wala kwa saa 7 za siku. Hii ni muhimu kwa ajili ya kuwa na kumbukumbu bora, kutulia, na kuwezesha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula wa mwili kufanya kazi ipasavyo na kusafisha kemikali za mwili.

3 - Kufanya mazoezi ya mwili

Sawa na kulala, mazoezi ya mwili yana faida nyingi katika maisha ya binadamu

 Kufanya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara ni mojawapo ya tabia muhimu unazofaa ili kudhibiti hatari ambazo zinaweza kuhatarisha afya ya moyo.

Shirika la afya duniani(WHO) linashauri kwamba watu wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 64 "wafanye mazoezi ya sakila kuanzia 150 hadi 300 ya wastani au dakika 75 hadi 150 ya nguvu zaidi" kwa wiki.

Ni muhimu kukumbuka kwamba mazoezi ya mwili, kama vile kukimbia na kuendesha baiskeli, ndio yanayoimarisha misuli na kuongeza pumzi na viwango vya mapigo ya moyo.

Shirika hilo linasema kuwani muhimu kwa mtu hufanya mazoezi ya kuimarisha misuli, kama vile mazoezi ya kutumia vifaa.

4 - Kuwa mwangalifu kuzidisha hali mbaya

Saretta alisema kuwa wakati wa hali ya wasi wsi mkubwa, ni kawaida kwa watu kuvuka mpaka na kufanya makosa mengi.

 Hii ni pamoja na kukosa usingizi, jambo ambalo anasema hutia moyo shinikizojambo ambalo linaweza kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi.

"Katika hali kama hii, ni muhimu kutathmnini hali na kuepuka kujiingiza katika malumbano yasiyo muhimu , kwani kuna hatari ya kurushiana matusi au kupigana ,"anasema Saretta.

5 - Zingatia dalili zamshituko wa moyo

Hatimaye, ni muhimu kwa kila mmtoja kutambua dalili za mshituko wa moyo au kiharusi na kufahamu la kufanya iwapo wanahisi au mtu mwingine anahisi yuko katika hali hii.

 Hatua hizi za huduma ya kwanza zinamaanisha tofauti kati ya maisha na kifo.

"kwa bahati mbaya, 50% ya watu wenye mshituko wa moyo huwa hawana dalili," Piscopo alisema.

 "Iwapo una mshituko wa moyo, ni kawaida kuhisi maumivu kwenye upande wa kushoto wa kifua, ambayo huwa makali zaidi wakati yanapoambatana na kutokwa jasho, kichefuchefu, kizunguzungu na maumivu zaidi", alisema Socesp, daktari wa magonjwa ya moyo.

 Iwapo mtu amewahi kuwa na mshituko wa moyo au ana mshituko wa moyo, au kiharusi, huwa na dalili kama maumivu makali ya kichwa, kupooza kwa uso au sehemu ya mwili, na kutembea kwa shida.

 "Kwahiyo, iwapo utahisi kwamba kuna mabadiliko ya kiafya, kama vile kushindwa kufanya shughuli ambazo huwa unazifanya kwa kawaida, kuwa na mchoko usio wa kawaida au maumivu ya kifua, unashauriwa kuwasiliana na daktari," anasema Saretta.