Je, kampuni za teknolojia zinapaswa kusoma ujumbe wa watumiaji?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mmiliki wa kampuni ya Meta Mark Zuckerberg anaelekea kuzozana na serikali ya Uingereza kufuatia hatua mpango wake wa kuimarisha ulinzi wa ujumbe wa watumiaji wa programu tumishi zake zote licha ya kuwepo kwa sheria muhimu ambayo inaweza kuharamisha teknolojia hiyo.
"Usimbaji fiche wa ujumbe kati ya watu wawili", "backdoors" na "uchanganuzi wa upande wa mteja" - safu kubwa zaidi katika teknolojia inaonekana ngumu sana.
Lakini swali ni Je, makampuni ya teknolojia yanapaswa kusoma ujumbe wa watu?
Hicho ndicho kiini cha mzozo ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi kati ya Silicon Valley na serikali za karibu nchi 12 duniani.
WhatsApp, iMessage, Android Messages na Signal zote hutumia mfumo salama kabisa unaoitwa usimbaji wa mwisho hadi mwisho.
Mfumo wa teknolojia hii unamaanisha mtumaji na mpokeaji ujumbe upande wa pili tu, anaweza kusoma ujumbe, kuona picha au video na hata kusikia simu. Hata waunda programu hawawezi kufikia yaliyomo.
Mabadiliko makubwa
Katika miaka 10 iliyopita, programu zilizosimbwa kwa njia fiche kutoka mwanzo hadi mwisho zimezidi kuwa maarufu, huku mabilioni ya watu wakizitumia kila siku.
Serikali nyingi na mashirika ya usalama yalikubali kuimarika kwa teknolojia hiyo - hadi miaka minne iliyopita, wakati Bw Zuckerberg alipotangaza jukwaani programu ya Messenger na kisha Instagram ikahamia kwenye usimbaji fiche wa mwanzo hadi mwisho kama kawaida.
"Tutawawezesha zaidi ya watu bilioni mbili duniani kote kufanya mazungumzo yao ya kibinafsi kwa faragha," alisema.
Tangu wakati huo, Bw Zuckerberg na jeshi lake la wahandisi wamekuwa wakikabiliana na mradi huo polepole na kimya kimya. Kampuni hiyo inakataa kuzungumza na waandishi wa habari wazi wazi kuhusu jinsi kazi hiyo kubwa inavyoendelea au wakati mabadiliko makubwa yatakuwa. "Mwisho wa 2023," ndipo yote yatawekwa hadharani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Huku hayo yakijiri, miito ya kusitisha ubadilishaji au kuimarisha ulinzi na faragha ya watumiaji wa app za mawasiliano imekuwa ikiongezeka.
Mamlaka nchini Uingereza, Australia, Canada, New Zealand, Marekani, India, Uturuki, Japan na Brazili - pamoja na mashirika ya kutekeleza sheria kama vile Interpol - yamekosoa teknolojia hiyo.
Lakini hakuna serikali katika ulimwengu wa kidemokrasia ambayo imetishia kupitisha sheria ambayo itaingilia programu hizi maarufu - hadi sasa.
Kuunda kampuni za teknolojia katika aina fulani ya mlango wa nyuma wa kiufundi ili kuruhusu ujumbe kuchanganuliwa kwa nyenzo zisizo halali ni mojawapo ya kanuni kuu za Mswada wa Usalama Mtandaoni wa Uingereza unaoenea kote, ambao huenda ukapitishwa kuwa sheria katika siku za usoni.
Maafisa wa polisi, ikiwa hawawezi tena kuuliza Meta kuhusu yaliyomo kwenye uumbe wa watu, watakosa chanzo kikuu cha ushahidi wanaotumia mara kwa mara kuwatia hatiani wahalifu au magaidi, serikali inasema.
Na kuna wasiwasi wanyanyasaji wanaweza kutumia programu kama hizo kuwadhulumu watoto kisiri.
Usimbaji fiche wa mwanzo hadi mwisho "utakuwa msaada mkubwa kwa yeyote anayetaka kumuumiza mtoto", Waziri wa Mambo ya Ndani Suella Braverman alimwambia Bw Zuckerberg Jumatatu katika ujumbe.

Chanzo cha picha, PA Media
Na siku ya Jumatano, Chama cha Kitaifa cha Kuzuia Ukatili dhidi ya Watoto (NSPCC) kimetoa ripoti ya uchunguzi wa YouGov ulioagiza, na kupendekeza umma wa Uingereza unataka maafisa wa polisi waweze kupata ujumbe wa watu, kulinda watoto.
Kati ya watu wazima 1,723 waliohojiwa kote Uingereza, asilimia 73 walisema makampuni ya teknolojia yanapaswa, kwa mujibu wa sheria, kuchunguza ujumbe wa kibinafsi wa unyanyasaji wa kijinsia wa watoto na kuuvuruga katika mazingira yaliyosimbwa kutoka mwisho hadi mwisho.
Wengi tayari wamepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto kwenye huduma zao, na kuchangia kufanikiwa kwa hatua zilizochukuliwa, NSPCC ilisema.
"Sasa ni wazi kwamba makampuni ambayo yanataka kupinga haki ya kimsingi ya usalama wa watoto dhidi ya haki za faragha za watu wazima yanaenda kinyume na matakwa ya umma, hatimaye, msingi wa watumiaji," Richard Collard, wa shirika la kutoa misaada, alisema.
Kujibu uchunguzi huo, msemaji wa Meta alisema kampuni hiyo "imetebuni hatua za usalama ambazo zinazuia, kugundua na kuturuhusu kuchukua hatua dhidi ya unyanyasaji huu mbaya" - vikwazo vya umri kwa kuwasiliana na wageni, kwa mfano.
'kudhoofisha faragha'
Siku ya Jumatano, katika hatua inayoonekana kana kwamba ni kuangazia hisia za pande zote mbili za mjadala, watafiti 68 mashuhuri wa usalama na faragha wamechapisha barua inayosema Mswada wa Usalama Mtandaoni utaathiri njia fiche usimbaji ujumbe kati ya watumiaji wa programu husika.
Mswada huo unaweka jukumu kwa makampuni ya teknolojia kutafuta njia ya kutekeleza hatua za usalama wa watoto bila kuingilia faragha ya watumiaji lakini wataalamu wanasema hili haliwezekani.
"Wasiwasi wetu ni kwamba teknolojia za uchunguzi zimewekwa kwa nia ya kutoa usalama mtandaoni," barua hiyo inasema.
"Kitendo hiki kinadhoofisha hakikisho la faragha na, hakika, usalama mtandaoni."
Pia inaweka kielelezo kwa tawala kandamizi duniani kote kufuatilia na kudhibiti kile ambacho watu wanashiriki mtandaoni, wanasema wataalam.
Kujenga upya uaminifu
Mitandao ya WhatsApp na Signal, zimetishia kusitisha huduma zao nchini Uingereza kuliko kuvuruga mfumo wa kudhibiti mawasiliano ya watumiaji wao.
Na kufanya mambo kuwa mabaya zaidi kwa wakosoaji wa teknolojia hiyo, Elon Musk alitangaza, mnamo Mei, yeye pia alikuwa akikamilisha usimbaji fiche, kwenye jumbe za Twitter.
Kubadilisha teknolojia ni ngumu na ni ghali, kama inavyothibitishwa na Meta, lakini wakubwa wa teknolojia wanafikiria.
Baada ya miaka mingi ya kashfa za data, kampuni hiyo kubwa ya teknolojia inaiona hatua hiyo kama ufunguo wa kujenga upya uaminifu katika huduma zake.
Na kwa bahati mbaya, usimbaji wa mawasiliano hurahisisha kazi ngumu ya ukadiriaji ya kampuni hizi zilizotatanishwa - ikiwa hawawezi kuona kile ambacho watumiaji wanashiriki, basi hawawezi kuidhibiti.












