Mfahamu Anas Al-Sharif - Mwandishi maarufu wa Aljazeera aliyeuawa kwa makusudi na Israel

Chanzo cha picha, Social Media
Akaunti iliyothibitishwa ya mwandishi wa Al Jazeera Anas Al-Sharif ilichapisha wosia ulionasibishwa kwake kwenye jukwaa la X usiku wa manane siku ya Jumatatu, ambapo alisema, "Huu ni wosia na ujumbe wangu wa mwisho. Ukipokea maneno haya, jua kwamba Israel imefaulu kuniua na kunyamazisha sauti yangu."
Katika wasia huo ulionasibishwa kwake, tarehe 6 Aprili 2025, Al-Sharif anasema: "Nilipitia maumivu hayo katika maelezo yake yote, na nilionja maumivu na hasara hiyo mara kwa mara, na pamoja na hayo, sikusita kamwe kueleza ukweli ulivyo, bila ya uwongo au upotoshaji.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images
Dakika chache kabla ya kifo chake, Al-Sharif alichapisha makala yake ya mwisho kuhusu vita vya Gaza, ambapo alisema, "Ulipuaji wa bomu haukomi. Kwa saa mbili, uvamizi wa Israel dhidi ya mji wa Gaza umekuwa ukiongezeka.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Mkurugenzi wa hospitali ya Al-Shifa katika mji wa Gaza alitangaza vifo vya Wapalestina watano katika shambulio la Israel dhidi ya hema lililokuwa na wanahabari karibu na lango la hospitali hiyo.
Waliojeruhiwa ni pamoja na waandishi wa Al Jazeera Anas al-Sharif na Mohammed Qreiqeh, pamoja na wapiga picha wa Al Jazeera Ibrahim Daher na Moamen Aliwa, na dereva wa wafanyakazi Mohammed Noufal.
Mwanahabari Mohammed Sobh pia alijeruhiwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina WAFA.
Kufuatia shambulio hilo kwenye hema la waandishi wa habari, jeshi la Israel lilikiri kumlenga Sharif katika taarifa yake, likisema lilimlenga "kiongozi wa Hamas Anas Sharif, ambaye alikuwa akijifanya mwandishi wa habari wa Al Jazeera."
Jeshi lilimshutumu kwa kuongoza "seli ya Hamas na kuratibu mashambulizi ya roketi dhidi ya raia wa Israel na vikosi vya kijeshi.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lilieleza kuwa operesheni hiyo ilifanywa kwa kutumia risasi za uhakika, sambamba na hatua alizozitaja kuwa zinalenga kupunguza madhara kwa raia, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa anga na ukusanyaji wa taarifa za ziada za kijasusi.
Kwa upande wake, Mtandao wa Vyombo vya Habari wa Al Jazeera umelaani "mauaji ya kukusudia ya wanahabari wetu Anas Al-Sharif na Mohammed Qraiqeh, na wapiga picha Ibrahim Zaher na Mohammed Noufal," kulingana na taarifa iliyotolewa mapema Jumatatu.
Taarifa hiyo ilisema: "Kuuawa kwa waandishi wetu na vikosi vya Israel vinavyokalia kwa mabavu ni shambulizi jipya, la wazi na la makusudi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari... Amri ya kumuua Anas al-Sharif, mmoja wa waandishi wa habari shupavu wa Gaza, na wenzake ni jaribio la kukata tamaa la kunyamazisha sauti kwa kutarajia kukaliwa kwa Gaza.
Kwa upande wake, Hamas ilimuomboleza Al-Sharif, mwandishi wa habari, na kueleza kuwa ni "uhalifu wa kikatili unaovuka mipaka yote ya ufashisti na uhalifu."
Imeongeza kuwa "kuendelea kulengwa kwa waandishi wa habari katika Ukanda wa Gaza ni ujumbe wa ugaidi wa uhalifu kwa ulimwengu mzima na kiashiria cha kuporomoka kabisa kwa maadili na sheria za kimataifa, huku kukiwa na ukimya wa kimataifa ambao umehimiza uvamizi huo kuendelea kuua waandishi wa habari bila kuwazuia au kuwajibika.

Chanzo cha picha, social media
Shutuma za awali za Israel
Msemaji wa jeshi la Israel Avichay Adraee hapo awali aliripoti kwamba mwandishi wa Al Jazeera Anas al-Sharif alikuwa na "mahusiano na Hamas na alishughulikia silaha."
Mnamo Agosti 2024, Adraee alimshutumu Al-Sharif kwa kuficha "shughuli za Hamas na Islamic Jihad" katika shule iliyolipuliwa, akisema katika chapisho kwenye jukwaa la X: "Unaficha uhalifu wa Hamas na Jihad ya Kiislamu kwa kujificha ndani ya shule. Nina hakika kwamba unajua majina ya idadi kubwa ya magaidi wa Hamas kati ya wale waliouawa."
Mnamo Julai 2025, Adraee alisema kwamba Al-Sharif alikuwa "mmoja wa waandishi sita wa Al Jazeera wanaohusishwa na Hamas au Islamic Jihad," madai ambayo Al Jazeera iliyakanusha vikali.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
"Uchochezi"
Wakati huo, Al-Sharif alielezea shutuma za Israel za "ugaidi" dhidi yake kuwa "za uchochezi" na "jaribio la kuninyamazisha, katika juhudi za kusitisha matangazo yangu kwenye Al Jazeera na mitandao ya kijamii."
Aliandika wakati huo, "Ujumbe wangu uko wazi: Sitanyamaza. Sitaacha. Sauti yangu itabaki kuwa shahidi kwa kila uhalifu, hadi vita hivi vikome haraka iwezekanavyo."
Mwishoni mwa Julai 2025, Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari, shirika la kimataifa lisilo la kiserikali, lenye makao yake makuu mjini New York City, lilitoa taarifa ikielezea wasiwasi wake kuhusu kile ilichoeleza kuwa "vitisho vya moja kwa moja na uchochezi wa umma" dhidi ya Anas al-Sharif, kufuatia kusambazwa kwa video na taarifa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii "yakimtaja kwa jina na kuhoji kazi yake ya uandishi wa habari.
Katika taarifa yake, kamati hiyo imezitaka mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama wake na usalama wa wanahabari wote wanaofanya kazi Gaza, ikisisitiza kuwa kuwalenga au kuwachochea waandishi wa habari ni ukiukaji wa sheria za kimataifa zinazolinda kazi ya uandishi wa habari wakati wa migogoro.
Taarifa ya Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari iliendana na msimamo sawa na huo wa Al Jazeera, ambao ulitoa taarifa mnamo Julai 25, 2025, wakidai kwamba unyanyasaji wa mwandishi wake huko Gaza, Anas al-Sharif, ulikuwa sehemu ya "kampeni ya uchochezi" inayolenga waandishi wake wa habari, na ikaona kuwa ni jaribio la kunyamazisha habari zinazoendelea kutoka ndani ya Gaza.
Anas Al Sharif ni nani?
Anas Al-Sharif alizaliwa mwaka wa 1996 katika kambi ya Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, na amekuwa mmoja wa waandishi wa habari mashuhuri wa Al Jazeera tangu kuzuka kwa vita mnamo Oktoba 2023.
Al-Sharif alionekana mara kwa mara katika matangazo ya moja kwa moja kutoka maeneo ya karibu na sehemu za milipuko au njia za mawasiliano, akisambaza picha za moja kwa moja kutoka maeneo hayo.
Mnamo Desemba 2023, alipoteza baba yake, Jamal Al-Sharif (akiwa umri wa miaka 65), katika shambulio la bomu ambalo lililenga nyumba ya familia, baada ya hapo aliendelea na kazi yake ya uandishi wa habari.
Al-Sharif aliripoti kuhusu wenzake, akiwemo Ismail al-Ghoul na Rami al-Rifi, ambao waliuawa katika shambulio la anga kwenye kambi ya wakimbizi ya Shati mnamo 2024.
Al-Sharif ameoa na ana mtoto wa kiume na wa kike. Januari iliyopita, mkewe alichapisha picha yake akiwa na watoto wake wawili kwenye akaunti yake ya Instagram iliyothibitishwa.

Chanzo cha picha, Reuters
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












