Lishe: faida za kiafya zisizotarajiwa za pilipili

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Iwe nyekundu, kijani kibichi, machungwa au manjano, pilipili ni mojawapo ya viungo vinavyotumiwa zaidi duniani.

Isidore Kouwonou

BBC Afrika

Inapatikana jikoni katika maeneo mbali mbali duniani. Iwe nyekundu, kijani kibichi, rangi ya chungwa au manjano, pilipili , ni mojawapo ya viungo vinavyotumiwa zaidi ulimwenguni, ina ladha nzuri, yenye sifa za kiafya zisizotarajiwa na ambazo wataalamu wa lishe wanashauri binadamu yeyote awe nazo.

"Tchssss, tchssss", hakuna mtu anayeweza kukataa kwamba hana tabia ya kufanya ishara hii ya asili kila wakati anapokula chakula chenye ladha tamu , lakini chenye viungo sana, au "viungo vilivyokolea viungo", kama wasemavyo huko, kusini mwa Togo.

Athari ya pilipili katika mchuzi, ambayo tumekuwa tukiifurahia , daima imesababisha walau kila mtu kulalamika, hata kuna wale wanaofikiria kuwa ni muhimu kunywa pombe kiasi ili kukabiliana na chakula " kilichoungwa vizuri.” kwa pilipili.

Katika maeneo mengi ambayo yanapika chakula hiki huko Bè-Kpota, mojawapo ya wilaya maarufu sana za Lomé, mji mkuu wa Togo, kuna kile kinachoitwa Maman Ayimouto (Ayimolou ni chakula cha Togo chenye mchanganyiko wa wali na maharagwe ambacho huliwa na pilipili nyeusi yenye viungo vingi) , BBC Afrika imebaini kwamba chakula hicho huwa hakina ladha, na hata vigumu kukila ikiwa wakati hakina pilipili ndani yake.

Watu wengi wanapenda vyakula vyenye "viungo vingi" ambavyo, zaidi ya hayo, vinapendekezwa na wataalamu wa lishe kwa sababu ya faida zake za lishe zilizomo ndani ya pilipili.

"Mchuzi mzuri wa viungo ndio ninaokunywa ili kuondoa kufungua pua zilizoziba. Pilipili husaidia wakati unapokuwa na mafua kwani hutoa taka iliyohifadhiwa humo,” anadakia Alex Komi, mpishi katika mkahawa mmoja huko Cotonou.

Lakini ni nini cha pekee kuhusu kitoweo hiki, pilipili hoho, ikinachowafanya watu wapendezwe sana nacho?

Pilipili ni nini?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa kweli, pilipili ni jina linalopewa mimea kutoka kwa familia ya Solanaceae ambayo matunda yake hutumiwa kama kitoweo au mboga. Inajulikana kuwa kali. Na kuna zaidi ya aina 200 za pilipili zilizowekwa katika aina 5, kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe, na mtaalamu wa usafi na ubora wa chakula, Dk Mathieu Tobossi, ambaye anabainisha kuwa tofauti zinapatikana katika sura, rangi, nguvu ya viungo na ukubwa wa hii. viungo.

Ikumbukwe kwamba kipengele cha ukali cha pilipili cha pilipili kinahusishwa na kuwepo kwa sehemu inayoitwa capsaicin ambayo inatoa nguvu hii kwa viungo.

Tunapata pilipili ambayo capsaicin iko kwenye kiwango cha sifuri (pilipili kwa mfano), kiwango cha 1 (kaprika), kiwango cha 2 (pilipili kali), kiwango cha 3 (pilipili kali), kiwango cha 4 (pilipili kali), kiwango cha 5 (pilipili kali), kiwango. 6 (pilipili kali/cayenne), kiwango cha 7 (pilipili kali/arbol), kiwango cha 8 (pilipili ya ndege), kiwango cha 9 (pilipili ya tabasco), kiwango cha 10 (pilipili inayolipuka/abanero).

Ni tunda lenye virutubishi vingi na madini mengi na na hivyo kuifanya pilipili kuwa mshirika mkubwa katika lishe ya kupunguza uzito.

Sifa za matibabu na faida

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtaalamu wa lishe hasa anazungumzia pilipili nyekundu (cayenne) ambayo ingekuwa na sifa nyingi zaidi.

Pilipili, hasa cayenne, husaidia kupunguza maumivu na kuboresha utendaji wa wanariadha, kulingana na tafiti fulani. Ni viungo ambavyo husaidia kurekebisha na kudhibiti viwango vya sukari ya damu.

"Vipengele hivi vyote huruhusu pilipili ili kukuza kuchoma mafuta na kupunguza uchovu," anasema Dk Tobossi, akiongeza kuwa pia ni kipengele kinachopigana kwa ufanisi dhidi ya matatizo ya oxidative.

Pilipili ya Chili, kulingana na yeye, huchochea hamu ya kula na inakuza mzunguko wa damu kwa sababu ya uwepo wa capsaicin. Inapendekezwa kwa watu ambao wanakabiliwa na indigestion na uvimbe wa tumbo. Pia ni antibacterial yenye ufanisi ambayo huondoa mvutano wa misuli na maumivu.

Mtaalamu wa lishe hasa anazungumzia pilipili nyekundu (cayenne) ambayo ingekuwa na sifa nyingi zaidi. "Ina nguvu ya kupunguza kwa kiasi kikubwa maumivu kutokana na arthritis, maumivu ya mishipa, maumivu ya shingo, tumbo na maumivu ya mgongo," anaongeza.

"Tafiti zimeonyesha kuwa ulaji wa pilipili wa mara kwa mara unahusishwa na kupunguza hatari ya kifo kutokana na ugonjwa wa moyo na mishipa," anasisitiza.

Kuna chuki fulani kuhusu pilipili pilipili ambayo mtaalamu alitaka kuibua mara moja. Wengi wanaamini kuwa pilipili ndio chanzo cha tatizo la vidonda ambalo watu wengi wanaugua. Pia kuna mazungumzo ya hemorrhoids inayohusishwa na viungo hivi.

Hatahivyo hupuuza madai haya na kusisitiza kwamba pilipili hulinda tumbo dhidi ya vidonda vya tumbo kwa kupunguza asidi ya tumbo.

Mtaalamu wa lishe anasisitiza zaidi kuwa pilipili huimarisha afya ya matumbo kuhusiana na usafirishaji.

Hata hivyo, anashauri wale ambao tayari wana vidonda waepuke kula pilipili kali kwa sababu “inaweza kuongeza maumivu” kwenye tumbo.

Wataalamu wa chakula wanasema kuwa hakuna hatari katika kula pilipili , isipokuwa kwamba haipaswi kutumiwa vibaya kwa kiasi kikubwa, kwa sababu inaweza kuathiri ute wa utumbo.

Hii ndiyo sababu unapaswa kuepuka matumizi ya ziada ya pilipili

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wataalamu wa lishe wanashauri wale ambao tayari wana vidonda waepuke kula pilipili, haswa kali, kwa sababu "inaweza kuongeza maumivu" tumboni

Wataalamu wa lishe wanashauri wale ambao tayari wana vidonda waepuke kula pilipili, kwa sababu "inaweza kuongeza maumivu" tumboni.

“Kiungo chochote cha viungo huwa na mwelekeo wa kuchochea vidonda,” anaonya Dakt. Mathieu Tobossi, anayewashauri wenye vidonda kuwa waangalifu wanapokula pilipili.

Hii hasa inahusu pilipili kali yenye muwasho ambayo inapaswa kuepukwa. Ushauri huu unahusu watu wanaougua magonjwa fulani mahususi ikiwa ni pamoja na:

  • Tezi dume
  • Mipasuko ya njia ya haja kubwa
  • Tatizo la asidi tumboni (Reflux ya gastroesophageal)
  • Maambukizi ya njia ya mkojo
  • Ugonjwa wa utumbo
  • Mzio kwa pilipili
  • Vidonda vya tumbo

Thamani ya lishe

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sahani ya wali uliokaangwa kwa vungo

Hapa, mtaalamu wa lishe anasisitiza pilipili aina ya , cayenne (pilipili nyekundu) inayotumiwa sana duniani kote. Ni pilipili ambayo inaweza kufikia urefu wa 3 hadi 4cm .

Muundo wa lishe wa pilipili ya cayenne una 66% ya wanga, 20% ya lipid (aina ya mafuta yanayofanya kazi mbali mbali mwilini) na 14% ya protini.

Inatoa juu sana wa nishati mwilini ikiwa na ,kalori 321,anasema.

Lipids zake huyeyuka kwa urahisi na kwa hiyo haziwezi kusababisha cholesterol katika mishipa ya damu au moyo.

Mboga hii, anaonyesha, ina kalori chache, sukari kidogo na ina maji na nyuzi nyuzi zinazosaidia katika usagaji wa chakula. Aidha anasema ina madini kama vile chuma, shaba, manganese, fosforasi na magnesiamu. "Tunapokula kiasi pilipili nyekundu kila siku tunapata lishe ya yenye vitamini A, C na B, ambao hupatikana ," anaarifu Dk. Mathieu Tobossi.

Kwa hiyo inashauriwa kuwa na maono mazuri na rangi ya kuangaza. Vitamini C ambayo husafisha mwili (antioxidant) husaidiamMifumo ya kinga na neva hufaidika na vitamini B6 iliyomo kwenye pilipili hiyo.

Pia kuna uwepo katika kiungo hiki cha vitamini K ambayo ina inasaidia katika uimarishaji wa mifupa. Pia kuna potasiamu ambayo husaidia kurekebisha shinikizo la damu na zinki ambayo huchangia uponyaji wa jeraha.

Kuna viungo vya Flavonoids na carotenoids kwenye pilipili hoho ambavyo ."Zinasaidia kupunguza madhara ya sumu za kikaboni kama vile na mkazo wa oksidi ambao hutuzeesha haraka," anaongeza mtaalamu wa lishe na mtaalamu wa usafi na ubora wa chakula.

Kwa thamani hizi za lishe , tunaweza tu kufurahia kula pilipili kama kiburudisho na pia kwa ajili ya thamani yake kwa mwili. Lakini kuwa mwangalifu, lazima uitumie kwa wastani kila wakati.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi