Kifo cha Malkia Elizabeth: Waafrika watoa wito wa kuombwa radhi

Chanzo cha picha, CHRIS PARKINSON/BBC
Katika kituo cha redio ya jamii katikati mwa kitongoji cha Hillbrow Johannesburg, MJ Mojalefa anaandaa kipindi cha redio ambacho kinarusu wasikilizaji kushiriki kwa kupiga simu studio baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II.
DJ mwenye umri wa miaka 22 anataka hadhira yake kubwa ya vijana kushiriki mawazo yao juu ya urithi wa himaya ya Uingereza, ambayo hapo awali ilijumuisha Afrika Kusini.
"Tulitawaliwa na Waingereza na [Malkia] hakuwahi kubadilisha asili ya uhusiano huo," mpiga simu mmoja anamwambia, katikati ya sauti ya chini ya muziki wa Amapiano.
"Watu wameendelea mbele, na yaliyopita ni yamepita," mwingine anasema.
Kuhusu MJ Mojafela, anataka msamaha kutoka kwa Mfalme mpya Charles III: "Watu wengi wanasema Malkia hakuomba radhi na ndivyo walivyotaka kutoka kwake."
Afrika Kusini ilikuwa jamhuri mwaka 1961. Kufikia wakati huo ubaguzi wa rangi uliofanyika ulikuwa sheria kwa miaka 13, tisa kati hiyo, Malkia Elizabeth II alikuwa kama Malkia kartika kiti cha ufalme.
Kwa vijana wengi wa Afrika Kusini historia hiyo imewaacha wakihangaika namna ya kupatanisha maisha machungu ya zamani na ya sasa.
Hayo ni maoni yaliyosikika tena wakati akizungumza na wasanii Mzoxolo "X" Mayongo na Adilson De Oliveira. Kazi yao inalenga katika kuondoa ukoloni.
"Tunapoangalia historia ya Afrika Kusini, hatuangalii tu kwa kutengwa," anasema De Oliveira. "Jambo moja linaongoza lingine."
Akiongea na bibi yake kuhusu uzoefu wa kuishi chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi kulileta msisitizo mkubwa kwa Mayongo. "Huwezi kuondoa makovu. Na unaponyaje majeraha hayo?" anauliza.

Chanzo cha picha, CHRIS PARKINSON/BBC
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lakini wote wawili wanasema kwamba wakati huu unatoa fursa kwa Mfalme Charles III kujenga uhusiano mpya na bara.
"Sisi hatuna huzuni" anasema De Oliveira. "Tunafikiri kwamba uhusiano wa baadaye ambao ufalme unaweza kuwa nao na Afrika unaweza kuwa kwa kuwajibika na kuja mezani kufanya mazungumzo haya na nchi za Afrika."
Walipoulizwa itakuwaje, wote wawili wanasema wanataka mazungumzo kuhusu fidia, kurejeshwa kwa vitu vya kale na kurudishwa kwa rasilimali za madini, kwa mfano almasi kubwa zaidi kuwahi kupatikana Star of Africa ambayo sasa ni sehemu ya taji lenye vito vya madini (Crown Jewels) yla Familia ya Kifalme ya Uingereza.
Wito huo wa kurejeshwa kutoka kwa utawala wa kifalme wa Uingereza kwasababu ya ukoloni unasisitizwa zaidi kaskazini mwa Nairobi.
Kenya ilipitia kipindi chake cha mpito wake wiki iliyopita wakati William Ruto alipoapishwa kama rais wa tano wa nchi hiyo tangu uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1963.
Ni wazi kuwa licha ya kuzingatia kuhusu mkuu wao wa serikali anayeingia madarakani, kifo cha Malkia bado kilikuwa habari ya ukurasa wa mbele nchini Kenya.
Pia imesababisha mjadala mpya kuhusu uhusiano wa nchi hiyo na mtawala wake wa zamani wa kikoloni.
"Inasikitisha kwamba tumepoteza binadamu," Nelson Njau mwenye umri wa miaka 30 anasema nje ya Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi chenye viti 60,000 ambapo Rais Ruto aliapishwa.
"Lakini walichofanya kwa utamaduni wa Kiafrika, kwa mataifa ya Kiafrika, kwa utajiri wetu, kwa shirika letu la jamii - kwa kweli wanahitaji kujitokeza na kutuomba msamaha."

Chanzo cha picha, JOE BARRETT/BBC
Pembeni yake, Sammy Musyoka mwenye umri wa miaka 29 anatikisa kichwa kukubali: "Bado tunahisi kuwa tunachukuliwa kama watu tuwasio sawa."
Hisia hiyo inatokana na kiwewe cha historia. Miezi michache tu baada ya Malkia Elizabeth II kukalia kiti cha Ufalme, uasi wa Mau Mau wa Kenya dhidi ya utawala wa Uingereza ulikandamizwa kikatili, huku Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya ikisema watu 90,000 waliuawa, kuteswa au kulemazwa.
Mnamo 2013, serikali ya Uingereza ilikubali kuwalipa Wakenya wazee 5,000 $22.6m (£19.9m) kama fidia kwa unyanyasaji walioupata wakati wa utawala wake wa kikoloni.
Wakenya wengi wazee, tofauti na wenzao wadogo katika umati wa kuapishwa kwa Rais Ruto, wanafikiria ni furaha kwa mamlaka yao ya zamani ya ukoloni.
Caroline Murigo, ambaye anasema ana zaidi ya miaka 50, anatuambia habari za kifo cha Malkia zilikuwa za kusikitisha.
"Ni mtu ambaye nimemfahamu maisha yangu yote. Ilikuwa ya kusikitisha lakini ilikuwa wakati wake. Tunamtakia kila la heri Mfalme mpya, Mfalme Charles."
Huku Mary Muthoni mwenye umri wa miaka 46 akidhani kuwa utawala wa kifalme bado una umuhimu kwa Wakenya leo. "Watatusaidia kuboresha uchumi wetu, na kuboresha miundombinu yetu katika nchi yetu."
Ujumbe rasmi wa rambirambi kutoka kwa viongozi na maafisa katika bara hilo karibu kwa kauli moja zimesifu utawala wa Malkia, rekodi ya uwajibikaji na ushirikiano wa muda mrefu na bara hilo.
Nchini Uganda, ambako alifanya ziara yake ya mwisho barani Afrika kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola mwaka 2007, bunge lilifanya kikao maalum kumuenzi.
Urithi mmoja wa utawala wa kikoloni wa Uingereza ni kwamba Nigeria ni makao ya mojawapo ya jumuiya kubwa zaidi za Kianglikana duniani. Kanisa la Nigeria lilifanya Ibada ya Kumkumbuka Malkia Elizabeth huko Abuja, ambapo mkuu wake, Mchungaji Ali Buba Lamido, alisema kuwa kama mkuu wa Kanisa la Uingereza, Malkia pia alikuwa muhimu kwa Waanglikana wa Nigeria.

Mwandishi wa BBC ambaye alihudhuria sherehe hiyo alisema hali ilikuwa mbaya lakini wengi hawakutaka kutoa rambirambi zao labda tafakari ya mjadala mkali juu ya urithi wa Ufalme wa Uingereza barani Afrika.
Huku Nairobi katika makazi yasiyo rasmi ya Mathare, Douglas Mwangi mwenye umri wa miaka 32 anafikiri Malkia anafaa kusherehekewa kwa kazi yake na Jumuiya ya Madola, ambayo aliongoza kwa miaka 70. Ni shirika huru la nchi 56, nyingi zikiwa makoloni ya zamani ya Uingereza.
Mnamo 2018, alitembelea Jumba la Buckingham kupokea Tuzo ya Viongozi Vijana wa Malkia (Queen's Young Leaders Award) kutoka katika kiti cha Ufalme. Alipata mafunzo na ufadhili kutoka katika mfuko wa Malkia wa Jumuiya ya Madola ambao ulisaidia shirika lake kusaidia vijana wenye ujuzi wa IT. Anasema mfuko huo umesaidia zaidi ya watu 14,000 huko Mathare tangu 2014.
"Hiyo [tuzo] ilitupa uaminifu. Tunajifunza mbinu bora za kile kinachotokea katika Jumuiya ya Madola na kuona jinsi tunavyoweza kuboresha mtindo wetu. Marehemu Majesty the Queen alikua Malkia akiwa na umri mdogo sana na aliamini katika uongozi wa vijana. watu."
Lakini si wote wanaona vivyo hivyo. Nikiwa nje ya uwanja wa kitaifa wa Kenya, Bw Njau, mfanyabiashara, anasema haoni jinsi Jumuiya ya Madola inavyomsaidia:
"Nimejaribu kutafiti jinsi tunavyonufaika Wakenya kwa kuwa katika Jumuiya ya Madola na inaonekana kama inawanufaisha viongozi wachache tu, watu wachache."
Mjadala uliofuatia kifo cha Malkia katika bara hilo ni ishara tosha kwamba kuna majeraha na majeraha mengi ambayo hayajapona tangu enzi za ukoloni na wengi wanahisi sasa ni wakati wa Uingereza na Mfalme wake mpya kufanya mazungumzo ya uaminifu na Waafrika kuhusu jinsi ya kuponya hali hii ya maumivu ya zamani.















