'Ukimwi ulichukua uwezo wa kuona wa jicho langu la kulia na kunizuia kutembea'

Chanzo cha picha, PERSONAL ARCHIVE
Mwaka 2015, Vitor Ramos, wakati huo akiwa mwanafunzi wa masomo ya utawala, alianza kupata dalili sawa na za homa ya mafua. "Alikuwa tu anahisi kuwa na muwasho kooni na kuhisi maumivu kiasi. Lakini nani angehusisha hali hii na maambukizi ya HIV ?", anauliza, Victor ambaye alipatikana na virusi hivyo miaka mitatu tu iliyopita.
Vitor anasema ilimchukua muda mrefu kuweza kukubali akilini mwake kwamba alipatikana HIV. "Nilidhani sikuwahi kufanya tendo la ngono na mtu ambaye alikuwa na virusi vya ukimwi, kwasabu katika fikra zangu nilidhani mtu yule angekuwa anaumwa mahututi kitandani na mdhaifu sana ," anasema.
Miaka mitatu baadaye dalili za kawaida za virusi vya HIV zilijitokeza, katika mwaka 2017, Victor alikuwa ameanza kuhara mara kwa mara jambo lililomfanya apoteze uzito wa mwili wa kila zipatazo 20 na kutembelea hospitali nane katika mji wa Araçariguama ambako aliishi, katika mji wa São Paulo, na katika wilaya za karibu na mji huo akitaka kujua ni ugonjwa gani unaomsumbua ,
"Daktari alifanya vipimo vya tumbo na kubaini kuwa nilikuwa maradhi ya Crohn maradhi yanayosababisha majera kwenye mfumo watumbo la chakula (gastrointestinal tract], ndio maradhi aliyoyashuku daktar. Hatahivyo, aliamua kunitibu kama mtu ambaye ana maradhi hayo ", anakumbuka.
Maambukizi ya virusi, yanaweza kumpata yeyote, bila kujali mtu anashiriki ngono ya aina gani. HIV hupatikana katika majimaji, kama vile damu, maji maji ya uke na maziwa ya mama.
Hii ndio maana inashauriwa kutumia mipira ya kondomu wakati wa kufanya ngono, na kwamba akina mama wenye HIV wanapaswa kuwalisha watoto wao maziwa maalumu ya kopo.
Zaidi ya kutobaini maradhi, daktari aliyemhudumia Victor alimpatia dawa ya kuzuia utendaji wa kinga mwilini, tiba inayofaa kwa maradhi ya Crohn, lakini ambayo ni ina madhara makubwa kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV.
"Dawa za kuzuia tendaji wa kinga (Immunosuppressive drugs) zinaweza kudhoofisha sehemu tofauti za mfumo wa kinga inategemea na dawa iliyotolewa.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ukitegemea mgonjwa ambaye alikuwa na seli chache za kinga, iwapo alitumia dawa ambayo iliufanya mfumo kuwa dhaifu sana, kuna hatari ya kumuacha na magobjwa nyemelezi, ambayo wakati mwingine HIV pekee haiwezi kutosha kusababisha", anasema mtaalamu wa magonjwa ya maambukizi kutoka Acre Dyemison Pinheiro, ambaye hakufuatilii kisa cha Vitor.
"Kuanzia siku ambayo nilianza matibabu, hali yangu ilikuwa mbaya kwa haraka zaidi. Ninasema kwamba nilishuka kiafya mithili ya mtu anayeanguka kutoka juu ya kilima na kuporomoka chini bondeni . Nilianza kutembea pole pole, kuendesha hakukusimama, niliketi nyumbani tuu kwasababu nilikuw anahitaji kwenda msalama wakati wowote. Nililazimika kuondoka chuoni", anakumbuka Vitor.
Kutokana na hali yake kuendelea kuwa mbaya, familia yake ilisisitiza kuwa atafute chumba cha dharura. "Nilijaribu kupinga hilo kwa kusema kuwa nilikuwa salama. Lakini siku moja, dada yangu aliwasili akiwa amepania kunichukua.
Nilitembea kuelekea kwenye gari, na wakati tulipofika hospitali, sikuweza kuhisi miguu yangu tena. Ilibidi nitolewe ndani ya gari na mlinzi wa uslama na nikaketi pale kwenye kiti cha magurudumu. Nilihisi kuwa kitu fulani hakikuwa sahihi kabisa mwilini mwangu."
Ilikuwa ni tarehe 8 Aprili, 2018, ambapo Vitor alipatikana na HIV.

Chanzo cha picha, PERSONAL ARCHIVE
Kiwango cha seli za kinga ya mwili (CD4) katika mwili wake kilikuwa cha chini sana. Kwa kulinganisha, kiwango cha kawaida cha mtu mwenye afya kinapaswa kuwa juu ya 500. Kinaposhuka na kuwa 350, huonyesha kuwa mtu huyo ana UKIMWI. Kiwango cha Victor cha CD4 wakati ule kilikuwa ni 2.
"Kwa matibabu, inawezekana kuboresha numba, lakini kiwango hakizingatii kurejea kwa mfumo wa kinga ya mwali . Baadhi ya watu huw ana seli za kinga ya mwili ambazo ni bora zaidi, na kwahiyo, kuna watafiti ambao husema kuwa, wakati idadi inapokuwa chini 350, bila shaka mtu huwa na ana UKIMWI ", anafafanua Pinheiro.
Zaidi ya virusi vya UKIMWI, Victor alibainika kuwa maambukizi ya mfumo wa kati wa neva (neurotoxoplasmosis) Kaposi's sarcoma (au saratani ambayo huathiri sehemu ya ndani zaidi ya mishipa ya damu na maradhi ya zinaa ya Kaswende na HPV.

Chanzo cha picha, PERSONAL ARCHIVE
"Ingawa HIV ni hatari, inaweza kuwa sio hali iayosababisha kifo. Kutokana na dawa za ziada, kutokana na kisa cha maambukizi nyemelezi, inashauriwa kuangazia zaidi kile ambacho ni hatari zaidi ", anasema Pinheiro.
Kwa ujumla, Victor alikaa miezi minne hospitalini, vikiwemo vpindi viwili katiika kitengo cha dharura (ICU).
"Nilipoteza uwezo wa kutembea wa miguu yangu na mikono haikuweza kusonga na ilibidi niwategemee watu wengine. Mwili wangu ulikuwa unaniuma sana, na sehemu moja ya paja langu nilianza kuona kila kitu ni chekundu. Hapo ndipo nilipopelekwa katika chumba cha matibabu ya dharura ICU kwa mara ya pili.

Chanzo cha picha, Personal Archive
"Katika miezi nilitumia pesa nyingi hospitalii, nIlipoteza mwili, uhusu na usiri. Baba yangu aliniuliza: 'Ni kitu gani cha kwanza ambacho ungependa kufanya ukitoka hapa? Kusafiri, kwenda kwenye duka kubwa la jumla...' Na nilijibu ninataka kuoga. Kusimama peke yangu. Alishangaa."
Victor anasema familia yake nzima ilimuonyesha upendo sana katika kipindi cha matibabu. "Iwapo leo nitazungumza wazi kuhusu kuishi na virusi vya HIV kwenye mitandao ya kijamii na kuwatia moyo watu wengine kupimwa, ni kwasababu nilikuwa na uunganji mkono mkubwa wa familia yangu."
Mazoezi ya kimwili ya kuniwezesha kutembea tena yalikuwa ya maumivu. "Wakati wauguzi walipoingia. Nilikuwa ninajifanya nimesinzia, sikutaka kufanyishwa mazoezi , ambayo nisikudhani kwamba yalinisaidia kabisa. Ilikuwa mpaka pale nilipoona ghafla kidole change kinaweza kujigeuza chenyewe ndipo nilipopata motisha."
Kutoka kwenye kiti kile cha magurudumu, Victor alianza kutembea kwa magongo, hatimaye, alianza kutembea kwa mkongojo – mageuzi ambayo yalimchukua mwaka mmoja.

Chanzo cha picha, Personal Archive
Wakati aliporusiwa kuondoka hospitalini, kiwango cha CD4 cha Victor kilikuwa ni 40, idadi ambayo bado inachukuliwa kuwa ni ya chini. Kwahivyo, sharti la kurejea nyumbani lilikuwa ni kwamba arejee hospitalini kila siku kuchomwa dawa kwenye mishipa.
"Walisema nisingeweza kupita kiwango cha kinga 200, kwamba hali yangu ilikuwa mbaya sana. Hizo zilikuwa ni siku ngumu sana. Dawa zilinifanya niwe dhaifu ." Katika vipimo vya mwisho viwili, CD4 yake ilikuwa zaidi ya 470.
Ingawa kiwango hakimaanishi kuwa alipona, kinaonyesha ishara nzuri ya kwamba matibabu yalifanikiwa, jambo ambalo Victor anasema lilliwezekana kwasababu alitekeleza na kufuata matibabu kama alivyoambia kila siku hadi leo, kama alivyoelekezwa hospitalini.
Zaidi ya hayo, musa mfupi baada ya matibabu, Victor aliweza kufikia kiwango cha kutobainika kwa virusi vya HIV, hiyo ikimaanisha kuwa hawezi kusambaza virusi kwa njia ya ngono hata bila kutumia mpira wa kinga.
Kulingana na mtaalamu wa magonjwa ya maambukizi Dyemison Pinheiro, hilo linawezekana kabisa, hata kwa hali mbaya sawa a aliyokuwa nayo Victor, ambapo watu waliopoteza kabisa kinga ya mwili na kuirudishiwa, kiwango cha kutobainika kwa HIV kinaweza kufikiwa kadri tiba inavyoendelea.
Hufanya mazoezi ya mara kwa mara, katika chumba cha mazoezi (gym) au kucheza mpira wa mikono na familia yake, alimaliza shule na hivi karibuni alipata kazi.
"Kwasababu ya ugonjwa niliopatikana nao hivi karibuni, ambao ulinichukua takriban miaka mitatu, UKIMWI ulinifanya nipoteze uwezo wangu wa kuona wa jicho moja, shemu ya usikivu wangu na kufanya mguu wangu wa kushoto uchelewe kupiga hatua kiasi. Lakini ninahisi vyema, ninanaweza kusema nimepona vizuri sana, na leo ninaishi vyema."
Katika mitandao ya kijamii, Victor huwatia moyo wanaume wengine na wanawake kupimwa mapema kabla virusi havijasambaa mwilini kote. Ningewaambia pia watafute wenyewe kuelewa taarifa kuhusu virusi badala ya kushawishiwa na anachosema mtu mwingine. Kuna maisha baada ya kupatikana na ugonwa", anasema.

Chanzo cha picha, PERSONAL ARCHIVE
















