Martin Fayulu, Mwanasiasa wa upinzani wa DRC asiyetetereka
Na Ousmane Badiane
Mwandishi wa BBC Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images
Mgombea ambaye hakuwa na bahati ya ushindi katika uchaguzi wa rais wa Desemba 2018, Martin Fayulu hakukubali kushindwa kwake na bado anaamini kuwa ndiye mwenye fursa ya kuiongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
"Uwezekano wangu ni mkubwa," alisema wakati wa uchaguzi wa rais uliopita miaka mitano iliyopita. Imani yake ilitokana na ukweli kwamba ndiye aliyekuchaguliwa na muungano wa upinzani DRC kuusimamia katika kinyang’anyiro cha kumrithi Bw Joseph Kabila.
Wapinzani walikusanya kwa pamoja raslimali zao za kifedha, mitandao yao ya ushawishi na umaarufu wao kuwahamasisha watu kumuunga mkono mgombea Fayulu.
Lakini siku ambayo matokeo yalitangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ni Félix Tshisekedi aliyetangazwa kuwa mshindi.
Félix Tshisekedi alikuwa miongoni mwa viongozi wa upinzani walioahidi kumuunga mkono Fayulu kabla ya kuondoa saini yake muda mfupi baadaye.
Kanisa Katoliki na washirika fulani wa DRC wanashikilia kuwa matokeo yaliyochapishwa na CENI hayaonyeshi ukweli wa masanduku ya kura. Wanashuku rais anayeondoka, Joseph Kabila, na mrithi wake walisaini makubaliano ya kisiasa-"mpango wa mtindo wa wanasiasa wa Kiafrika’’. Lakini kambi ya Tshisekedi imekuwa ikikanusha madai hayo.
Kwa upande wake, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) "ilibuni matokeo" ili kupanga kile anachokielezea kama "njama za ghasia zinazolenga mapinduzi ya serikali." »
CENI imekuwa ikikanusha kuwa ilibuni matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2018.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mbali na malalamiko ya mashirika ambayo yalihoji ukweli wa matokeo yaliyotangazwa na CENI , haiba na ushawishi wa Félix Tshisekedi ulianza kubadilisha mazungumzo yao.
Mmoja baada ya mwingine, walianza jinsi makabidhiano ya madaraka yalivyokuwa ya amani bila umwagaji damu, na kuomba nchi ipewe nafasi ya kuandika ukurasa huu mpya katika historia yake.
Martin Fayulu alijikuta peke yake katika mapambano yake kuhusu "ukweli wa matokeo halisi ya kura’’
Majaribio ya upatanishi kuleta maridhiano na kambi ya Félix Tshisekedi yaligonga mwamba kwasababu "rais aliyechaguliwa" aliweka masharti: kwamba rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anatambua kuwa ameiba madaraka kutoka kwake na kuyarudisha kwake. Bila ya kutekelezwa kwa matakwa hay abasi hakuna uhusiano unaowezekana.
Wakati huo huo, mwanasiasa huyu kutoka Faden House aliendelea kuongeza shinikizo zake kupitia vyombo vya habari zinazolenga mamlaka ya Tshisekedi.
Hata alifanikiwa kuandaa maandamano machache yaliyowaleta pamoja maelfu ya wafuasi wake kumtaka Felix Tshisekedi ajiuzulu.
Kwa baadhi ya watu katika mji mkuu Kinshasa, jina Fayulu lilijulikana kama jina la mtu asiyetetereka, mtu ambaye kamwe hakati tamaa.
Sasa muda umewadia tena, kupitia muungano na gavana wa zamani wa Katanga, Moïse Katumbi, na waziri mkuu wa zamani Adolphe Muzito.
Mazungumzo yanaendelea kutafuta mgombea wa upinzani. Wakati huo huo, Martin Fayulu alianza kampeni zake za uchaguzi kwa kuonyesha msimamo wake wa kumkosoa mara kwa mara wa utawala wa nchi wa rais anayeondoka.
Kazi ya muda mrefu katika sekta binafsi

Martin Fayulu alikamilisha ambaye alizaliwa mjini Kinshasa mnamo Novemba 21, 1956, alikamilisha sehemu ya masomo yake ya usimamizi (manejimenti) nchini Ufaransa na Marekani.
Akiwa na shahada mbili za uzamili, ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Paris na ya pili ikiwa ni ya usimamizi wa biashara ambayo aliipata kutoka Chuo Kikuu cha San Francisco, Marekani, Martin Fayulu amejitengenezea fursa katika biashara duniani.
Mkurugenzi huyu wa zamani wa Exxon Mobil, alihudumu miongo miwili katika kampuni ya mafuta ya Marekani. Alipanda katika scheo, akipata vyeo vya kimkakati katika utawala wa ngazi ya juu wa kampuni hiyo nchini Marekani, Ufaransa, Nigeria na Mali.
Cheo chake cha mwisho ilikuwa ni meneja mkuu wa kampuni hiyo nchini Ethiopia.

Ahadi ya kisiasa
Aliingia katika siasa mwaka 1991 baada ya kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Taifa uliowakutanisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali, vyama vya siasa, asasi za kiraia na hata viongozi wa kimila kudai demokrasia ya vyama vingi.
Wakati huo, nchi hiyo ilikuwa ikiongozwa na Marshal Mobutu Sese Seko chini ya utawala wa chama kimoja.
Mwaka 2009, Martin Fayulu aliunda chama cha ECIDE (Commitment to Citizenship and Development) ambacho alikiongoza.
Sauti kali ya hotuba yake ya kisiasa ilimuwezesha kuwavuta kwa idadi kubwa ya vijana wanaotafuta njia mbadala za kijamii na kisiasa.
Alichaguliwa kuwa naibu mkuu wa mkoa kuanzia mwaka 2006 hadi 2011 kisha naibu wa kitaifa kuanzia 2011 hadi 2018.
Wakati wa maandamano ya kuunga mkono demokrasia ya 2016 na 2017, Martin Fayulu alikuwepo sana chini. Wafuasi wake wanampa jina la utani "askari wa watu" na kumuelezea kama kiongozi aliyejaa imani, mwenye nia ya wazi na aliye karibu na wapiga kura mashinani.
Ikiwa wale walio karibu naye wanamsifu mtu mkali na mwenye kanuni, wachambuzi wa siasa za Congo wanamkosoa Martin Fayulu kwa ukosefu wa sera za kisiasa.
Mada za kampeni yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Martin Fayulu alisisitiza nia yake ya mabadiliko na uboreshaji wa nchi.
Rais huyo wa chama cha ECIDE (Commitment to Citizenship and Development) hivi karibuni alielezea nia yake ya kuanzisha jeshi la watu 500,000, waliofunzwa vizuri na wenye vifaa vizuri. Pendekezo hili linalenga kuimarisha usalama nchini na kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa uhuru, wa haki na wa uwazi.
Mwaka 2018, Fayulu alisema anataka kurejesha usalama katika nchi hiyo iliyoathiriwa na mgogoro na anapanga kuhamisha kituo kikuu cha jeshi kutoka Kinshasa hadi mashariki, eneo ambalo ni kitovu cha ghasia.
Wakati wa mkutano wa hivi karibuni na wakazi wa mji wa Bagata, katika jimbo la Kwilu, Martin Fayulu pia alisisitizia umuhimu wa kuwa makini na ufuatiliaji siku ya kupiga kura, ili kuzuia jaribio lolote la udanganyifu wa uchaguzi.
Zaidi ya ahadi zake za usalama na uwazi wa uchaguzi, Martin Fayulu pia alielekeza kampeni yake juu ya mada kama vile uchumi, elimu na upatikanaji wa huduma za afya. Amejitolea kupambana na rushwa na kukuza uwekezaji katika sekta muhimu ili kuongeza ustawi nchi na kutoa ajira nchini DRC.
Pia analenga kubadilisha mikataba ya madini na mafuta ili kuinufaisha nchi na kusisitiza kuwa kazi yake katika Exxon Mobil ilimtayarisha kwa nafasi hii.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












