'Kusitishwa' kwa misaada ya kijeshi ya Marekani kuna maana gani kwa Ukraine?

u

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Uamuzi wa Rais Donald Trump wa kusitisha misaada yote ya Marekani kwa Ukraine ni pigo kubwa - sio kwa Kyiv pekee bali pia washirika wa Ulaya ambao wamekuwa wakishawishi utawala wa Marekani kuendelea kuwaunga mkono.

Hii si mara ya kwanza kwa Marekani kukataa kutoa msaada wa kijeshi. Wanachama wa Republican katika Bunge la Congress walizuia kiasi kikubwa zaidi cha msaada wa kijeshi wa Rais wa wakati huo Joe Biden kwa Ukraine katika msimu wa jkiangazi wa mwak 2023.

Lakini Ukraine ilifanikiwa kupata kwa shida hifadhi iliyopo ya risasi kwa usaidizi wa Ulaya.

Congress hatimaye iliidhinisha msaada wa £60bn katika mwaka 2024. Ilikuwa ni wakati muafaka - Ukraine ilikuwa ikijitahidi kuepusha mashambulizi mapya ya Urusi mjini Kharkiv. Kuwasili kwa silaha za Marekani zilizochelewa kulisaidia kubadili hali hiyo.

Sawa na mwaka wa 2024, inaweza kuchukua miezi kadhaa kabla ya athari za kukatwa kwa misaada ya Marekani kuonekana - angalau katika suala la risasi na vifaa.

Mataifa ya Ulaya yameongeza polepole uzalishaji wao wa makombora ya mizinga. Kwa ujumla Ulaya sasa inaitoa Ukraine asilimia 60 ya misaada yake - zaidi ya Marekani.

Hata hivyo, msaada wa kijeshi wa Marekani bado ni muhimu kwa Ukraine. Afisa mmoja wa Magharibi hivi majuzi aliielezea kama "krimu " katika suala la silaha.

Uwezo wa Ukraine wa kulinda watu na miji yake umeegemea pakubwa mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga ya Marekani - kama vile betri za Patriot na NASAMS - zilizotengenezwa kwa pamoja kwa ushirikiano na Norway.

Marekani imeipa Ukraine uwezo wa kufanya mashambulizi ya masafa marefu - kwa makombora ya HIMARS na ATACM.

Marekani imepunguza matumizi yake ndani ya Urusi, lakini bado yamekuwa muhimu kufikia malengo ya thamani ya juu ndani ya maeneo yanayokaliwa.

Sio ubora tu, bali pia wingi. Kama jeshi lenye nguvu zaidi duniani, limeweza kutuma mamia ya Humvees za ziada na magari ya kivita - nambari ambazo majeshi madogo ya Ulaya hayangeweza kufikia.

Kutokuwepo kwa baadhi ya usaidizi huu kunaweza kuchukua muda kufikia hadi maeneo ya mstari wa mbele. Lakini kunaweza kuwa na athari ya papo hapo inayotia wasiwasi zaidi, si haba katika suala la ugavi wa kijasusi.

Hakuna taifa linaloweza kufanana na Marekani katika masuala ya uchunguzi wa anga za juu, kukusanya taarifa za kijasusi na mawasiliano. Na hautolewi tu na jeshi la Marekani , lakini pia kampuni za kibiashara

d

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanajeshi wa Ukraine akitayarisha mtandao wa satelaiti kutoka kampuni ya Elon Musk ya Starlink
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Chukua kwa mfano mtandao wa mawasiliano wa satelaiti wa Elon Musk wa Starlink. Kila mstari wa mbele nilioutembelea una sahani ya Starlink.

Zinatumika kutoa habari za hivi punde kwenye uwanja wa vita. Zimekuwa muhimu kuratibu mashambulizi ya silaha na ndege zisizo na rubani.

Katika siku za nyuma, Pentagon imekiri kwamba imekuwa ikifadhili njia hii ya mawasiliano. Ikizingatiwa kuwa Elon Musk ni mtu muhimu katika utawala wa Marekani, inaonekana kuna uwezekano mkubwa kwamba sasa atakuwa tayari kutekeleza mswada huo. Yeye pia ni mkosoaji mkali wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Je, Marekani itazuia nchi za Ulaya kutuma vifaa vyao vilivyotengenezwa na Marekani kwa Ukraine? Wakati Ulaya ilipotaka kutoa ndege za F-16 zilizotengenezwa na Marekani kwa Ukraine, ilibidi kwanza kupokea kibali cha Washington.

Na kisha vipi kuhusu matengenezo ya vifaa vinavyotolewa na Marekani? Marekani pia imekuwa ikitoa mafunzo kwa vikosi vya Ukraine na kisha kuvisaidia kutunza vifaa vinavyotolewa na Marekani.

Biden aliondoa vikwazo kwa wakandarasi wa Marekani wanaofanya kazi nchini Ukraine kuelekea mwisho wa muhula wake. Jeti za F-16 hasa zinahitaji wahandisi na vipuri ili kuendelea kufanya kazi.

Uamuzi wa Trump wa kusitisha msaada unaweza, kwa wengi nchini Ukraine na kwingineko, ukaonekana kuwa wa kuudhi. Lakini pia kuna lengo la kisiasa la kuwalazimisha wakae kwenye meza ya mazungumzo mapema.

Matumaini kati ya washirika wa Ulaya ni kwamba itakuwa ni usitishaji wa muda mfupi tu. Bila msaada wa Marekani, Ukraine italemewa na mapambano makali zaidi.

Imehaririwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi