Kwanini wimbo wa "All i want for Christmas is You" bado unatawala msimu wa Krismasi wa kizazi cha sasa

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Jeffrey Ingold
- Nafasi, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 7
Wimbo wa All I want for Christmas is You" ya mwimbaji Mariah Carey ulitoka mwaka wa 1994 na kufanya mafanikio makubwa, lakini baada ya miaka 30, imekuwa wimbo unaotawala msimu wa likizo. Nini siri ya mafanikio yake?
Kama tunavyojua kuna mambo matatu ambayo ni hakika maishani: kodi, kifo, na kwamba kila mwezi Disemba, All I Want for Christmas Is You itakuwa sehemu ya orodha ya nyimbo za Krismasi.
Ima uko kwenye maduka, karamu za ofisini, au unacheza orodha ya nyimbo za likizo, unajua msimu wa sherehe umeanza unapoisikia.
Wimbo huu, uliotolewa miaka 30 iliyopita, umejiunga na viwango vya Krismasi vya jadi kama Blue Christmas na Rockin’ Around the Christmas Tree, na umeendelea kuwa maarufu kila mwaka.
Ingawa ulianza kwa mafanikio kiduchu, wimbo huu sasa umeongoza katika chati zaidi ya nchi 25, ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, na kutangazwa rasmi kuwa wimbo bora zaidi wa Krismasi na Billboard mwaka 2023.
Mafanikio yake ya kudumu na umaarufu mkubwa sasa yanajenga swali: Nini kilichofanya wimbo huu kuwa jazanda ya Krismasi kama Santa Claus mwenyewe?
Hakika ni wimbo wa kufurahisha,"asema Dkt.Brittany L. Proctor,profesa wa masomo ya uanahabari na utamaduni katika The New School,New york.
"Ukitathmini nyimbo zilizo na maudhui ya krismasi hazifurahishi sana,"Kwa Dkt Proctor ,All i want for Christmas is You ,ilichukua hadhi ya krismasi na kuigeuza kuwa maudhui makuu"kwa kuleta pamoja vipengele vya injili,R & B,na pop" kwa njia ya kufurahisha ambayo inahusiana na mbwembwe za krismasi ",kama vile mwandishi wa nyimbo Kate Solomon aiambia idhaa ya BBC,ni wimbo bora wa pop ambao hutokea tu kuwa wa Krismasi."
Jinsi inavyoipatia mahadhi ya krismasi kikamilifu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Sio rahisi kutunga nyimbo za kizazi kipya za Krismasi.
Wasanii kama vile Taylor Swift, Justin Bieber na The Killers (kutaja wachache) wamejaribu, lakini nyimbo zao zote za asili zimeshindwa kutawala miaka kadhaa baadaye.
Kulingana na Nate Sloan, mwanamuziki na mwandalizi mwenza wa podikasti ya Switched On Pop,kinachofanya kutunga nyimbo ya sherehe ya krismasi kuwa ngumu inalazimu wasanii wa pop kuvumbua na kuunda mahadhi mapya".
Sloan anaonyesha kwamba hata wakati wasanii wa kisasa kama vile Dua Lipa au Bruno Mars wanaporejelea sauti za zamani kama disco au jack swing mpya katika muziki wao, "lazima isikike mpya na mpya ... lakini mwezi Disemba inapoanza kuna msukumo huu kinyume kabisa kutoka kwa mashabiki, ambapo hupendelea tungo za miaka ya 1940 na 1950 na Bing Crosby na Brenda Lee."
Nyimbo za kisasa za msimu wa krismasi huwa hazidumu kwani wasanii wengi hujaribu kuweka mahadhi ya jadi na kuchanganya na ya sasa .
Kama ilivyo kwa wimbo wa krismasi wa Santa Tell Me iliyoimbwa na muimbaji Ariana Grande.
Hata hivyo, All I Want for Christmas Is You ya Mariah Carey ina mafanikio makubwa katika kutekeleza hili kwa ustadi, ikicheza kwa ufanisi kati ya enzi za muziki na aina mbalimbali.
Carey alisema lengo lake lilikuwa kuunda wimbo usio na wakati, na kwa hiyo, haujisikii kama wa miaka ya 1990. Hii ndiyo sababu alifuatilia sauti ya “Wall of Sound” ya Phil Spector, akitumia mbinu alizozitumia na Ronnie Spector kutoka Ronettes katika toleo lao la Sleigh Ride.
Kama anavyosema mkosoaji wa tamaduni za nyimbo za pop, Aisha Harris, wimbo huo “huhisi kuwa ni wa kisasa na uliozoeleka,” kutokana na “ala, kengele zinazolia, na maelewano ambayo ni heshima kwa Krismasi ya Darlene Love (Baby Please Come Home)”.
Wimbo huo ulipokuwa ukitoka kwa mara ya kwanza, ulionekana kama wa zamani, na kutokana na kuchezwa kwake mara moja kwa mwaka, kila wakati unasikika kuwa kibao kipya.
Aidha,kibao cha All I want for Christmas is You ni matumizi yake ya kwaya ,ambayo unahisi ni wa enzi nyingine yamuziki.
Kama anavyoeleza Nato Sloan,'Nyimbo nyingi za pop za kisasa, kama Wimbo wa A Bar na Shaboozey, ni nyimbo zenye noti za msingi nne," anasema Sloan. "Lakini nyimbo za likizo kama Wimbo wa Krismasi (Chestnuts Roasting on an Open Fire ) zina kordi hizi mseto ambazo zinabadilika kila mara.
" Anakadiria wimbo wa All I Want for Christmas is You ina kordi 13, na hivyo kukufanya uhisi kuwa "unapitia mazingira tofauti ".

Chanzo cha picha, Alamy
Zaidi ya ubora wa kibao chenyewe,kuna vigezo vingine muhimu ambavyo vimesaidia All I Want for Christmas Is You kuwa wimbo wa sikukuu wa aina yake.
Kwanza kabisa, ni msanii mwenyewe, Mariah Carey. Akiwa na ufahamu mkubwa wa chapa yake, Carey ni mtaalamu wa kujua kile kinachofanya kazi kwake. “Anapenda Krismasi, na hutokea kwamba kitu anachopenda pia kinamletea mapato na rasilimali,” anasema Aisha Harris.
Katika kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake ya 2020, Carey alielezea jinsi familia yake ilivyoharibu likizo, na alijiahidi kwamba atakapokua, atafanya Krismasi kuwa “kamili kila mwaka”.
Alijaribu pia kuweka chapa ya biashara ya “Malkia wa Krismasi” mnamo 2022, ingawa ombi lake lilikataliwa.
Ukuzaji wa wimbo wa Krismasi
Ukuaji wa wimbo huu ulipata msukumo mkubwa ulipoonyeshwa katika filamu maarufu ya Love Actually ya 2003, ambapo wimbo huo ulifanywa maarufu zaidi alipohusishwa na tukio la kipekee iliyoimbwa na mwigizaji Olivia Olson.
Filamu hiyo ilitolewa wakati Carey alikuwa akipitia kipindi kigumu katika kazi yake, baada ya kushindwa kwa filamu yake ya Glitter na kufanyiwa utani kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari.
Nusra apoteze umaarufu wake wa kimataifa, lakini umaarufu wa Love Actually ulileta ufanisi mpya kwa wimbo huo, na kumfanya kuwa kiungo katika msimu wa Krismasi.
Kama anavyosema Dkt. Proctor, “Uhusiano huu wa kimaelewano kati ya mapenzi ya watu kwa filamu na upendo wa wimbo ulisaidia wimbo kuenea zaidi na kufikia familia nyingi .”
Tangu wakati huo, Mariah Carey ameendelea kutafuta njia bunifu za kuweka All I Want for Christmas Is You katika mioyo na akili za mashabiki.
Mnamo 2010, alitoa albamu ya pili ya Krismasi, ikiwa ni pamoja na toleo la “Sikukuu ya Ziada” la wimbo huo.
Aidha, kumekuwepo na matoleo mengine maarufu, kama “SuperFestive!” aliloshirikiana nalo na Justin Bieber (2011), uchezaji maarufu wa wimbo na The Roots kwenye Jimmy Fallon (2012), na duet with Michael Bublé (2013).
Mnamo 2019, Carey alianzisha utamaduni wa kila mwaka wa kutuma video kwenye mitandao ya kijamii, akitangaza “Ni wakati” wa kuanza msimu wa Krismasi mwezi Novemba tarehe mosi, jambo ambalo limekuwa sehemu ya sherehe ya Krismasi kwa mashabiki duniani kote.

Chanzo cha picha, APple TV+
Harris ameongezea sifa wimbo huu wa All I Want for Christmas is You' namna muimbaji Carey anaendelea kuubadilisha kulingana na mashabiki wanavyopenda na namna ya kuiwasilisha mitandaoni.
"Biashara nyingi na maeneo ya umma yanatumia majukwaa kama Spotify na Apple kucheza nyimbo," anasema, na wakati wa msimu wa likizo "wanacheza nyimbo zilezile mara kwa mara".
Sababu isiyoeleweka ya athari yake ya kudumu
Kuna kipengele kingine muhimu, ambacho mara nyingi hupuuzwa, cha mtindo huu wa sherehe ambacho husaidia kuelezea kinachovutia jamii: Utangulizi.
Kuingia kwa sekunde 50, sauti ya polepole na ya kupendeza ya Carey haifanyi tu hali ya wasiwasi, lakini, kama Sloan anapendekeza, ni kama "hisia kama vile kwamba unaingia kwenye nafasi mpya".
Wakati kengele za sleji inayokokotwa na farasi na ngoma zinapopigwa mwishoni mwa utangulizi kwa "mdundo wa tatu", inasikika "kama farasi anayekimbia mbio au kuendesha gari la kuogelea... ni tangazo kwamba hatutaingia tu katika ulimwengu wa wimbo huu, lakini ulimwengu huu wa msimu ambao ni wa kipekee na ulichokisiliza awali".
Kasi ya mawimbi ya sauti,ya utangulizi wa kibao cha All I Want for Christmas is You, hukupa fikra na hisia kuwa msimu wa Krismasi umeanza rasmi.
Zaidi ya yote, All I Want for Christmas Is You inagusa mioyo ya watu kwa sababu ni wimbo unaosherehekea matumaini na ndoto, hasa katika kipindi cha Krismasi.
Mistari yake, ambapo Carey anasema kwamba hataki chochote isipokuwa mtu mmoja tu, yanazungumza kuhusu tamaa ya kweli na furaha ya Krismasi.
Kama anavyosema Kate Solomon, “Krismasi ni wakati wa matumaini, na wimbo huu una ujumbe kama huo ni furaha, ni kimapenzi, na inahusiana na kila mtu ambaye amewahi kuwa na shauku ya upendo.” Wimbo unajenga anga ya matumaini, na kwa muda wa sherehe, huleta uwezekano wa kupata kila kitu unachotaka.
Mnamo 2019, Carey alifikia kilele cha mafanikio yake ya Krismasi alipochukua nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard Hot 100 nchini Marekani.
Hata hivyo, wimbo huu alikuwa tayari umejikita katika mioyo ya mashabiki wake kabla ya hapo.
Ingawa Carey alijaribu kutambulisha jina lake kama “Malkia wa Krismasi,” umaarufu usio na kipimo wa All I Want for Christmas Is You unahakikisha kuwa utadumu kama taji la Krismasi kwa muda mrefu, huku wimbo huo ukitawala kila msimu wa likizo.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid












