Nyimbo ya wake wa wanajeshi yapendwa
Nyimbo ya kikundi cha kwaya cha wake wa wanajeshi wa Uingereza walioko Afghanistan imekuwa ya kwanza katika orodha ya nyimbo za Krismasi zilizopendwa.

Chanzo cha picha, Reuters
Nyimbo hiyo, 'Wherever You Are', ilitungwa kutoakana na maneno yaliyoandikwa kwenye barua baina ya wanajeshi na wake zao.
Ilifika kuwa ya kwanza kati ya nyimbo zinazonunuliwa na watu zaidi ya nusu-milioni ilipotoka tu, juma la mwanzo la Disemba.
Hiyo ni idadi kubwa kushinda jumla ya rikodi zote zilizouzwa juma hilo.
Fedha zitazopatikana katika mauzo zitatolewa kama msaada kwa Royal British Legion, shirika linalowasaidia wanajeshi.








