Kwa nini wanawake huwa na tabia ya kukojoa mara nyingi zaidi kuliko wanaume ikiwa vibofu vyao viko sawa kwa ukubwa?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kibofu cha mkojo cha wanaume na wanawake kinaweza kushikilia kwa urahisi kati ya mililita 400 na 600 za mkojo.
Muda wa kusoma: Dakika 4

"Tunasimama tena?" Hili ni lalamiko la kawaida kwa safari za familia, na mara nyingi huelekezwa kwa wanawake.

Kuanzia vichekesho vya televisheni hadi vicheshi vya kusimama, wazo kwamba wanawake wana vibofu vidogo limekuwa mzaha wa kitamaduni. Lakini Je hii ni kweli?

Jibu fupi ni, si kweli. Picha kamili inaonyesha mwingiliano mgumu zaidi—na wa kuvutia zaidi—kati ya anatomia, fiziolojia, na hali ya kijamii. Wanawake wanaweza kuhisi wanahitaji kwenda chooni mara nyingi zaidi, lakini ukubwa halisi wa kibofu chao sio tofauti sana.

Kibofu cha mkojo ni puto yenye misuli iliyoundwa ili kunyumbulika. Vitu viwili muhimu hufanya hatua hivo iwezekane: misuli ya detrusor na epithelium

Detrusor ni safu ya misuli laini inayounda ukuta wa kibofu. Mnumbuliko wake sio wa kawaida - inaruhusu kibofu kunyoosha bila kuchochea mara kwa mara ishara "kamili". Tunapohitaji kukojoa kwa haraka, hujibana kwa nguvu ili kutoa mikojo.

Mshipa wa ndani, kwa jina epithelium, hufanya kazi kama origami ya kibayolojia, kunyoosha na kujikunja ili kukidhi kiasi kinachopanuka, huku ikilinda tishu zilizo chini kutokana na sumu ya mkojo uliohifadhiwa.

Pia unaweza kusoma

Tofauti kati ya wanaume na wanawake

Kimaumbile kibofu cha kiume na cha kike ni sawa zaidi kuliko tofauti zao. Vyote viwili hubeba kati ya mililita 400 na 600 za mkojo. Kinachozunguka kibofu cha mkojo kinaweza kuathiri hisia na uharaka, na hapa ndipo tofauti zinapoanza.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaume huwa na uhuru zaidi

Hata iwapo mimba haipo, mapungufu ya anga yanaweza kusababisha kibofu cha mkojo kuamsha hisia za uharaka mapema.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata kibofu kilichojaa kwa ujazo wa chini, labda kutokana na athari za homoni, kuongezeka kwa hisia, au uhusiano kati ya usaidizi wa sakafu ya pelvic na misuli inayonyoosha kibofu.

Sakafu ya fupanyonga—kundi la misuli inayotegemeza kibofu cha mkojo, uterasi, na matumbo—ni muhimu.

Kwa wanawake, inaweza kudhoofika kwa sababu ya kujifungua, mabadiliko ya homoni, au kupita kwa muda tu, na kuharibu uratibu kati ya kushikilia na kutolewa.

Sehemu kubwa ya udhibiti huo inategemea sphincter ya nje ya urethral, ​​pete ya misuli ambayo hufanyakazi kama mlinzi wa kibofu cha mkojo, kukusaidia kusubiri wakati unaofaa zaidi ili kukojoa.

Ni sehemu tata ya sakafu ya pelvic na, kama misuli yoyote, inaweza kupoteza uwezo wake au kujizoesha tena.

Wakati huo huo, maambukizi ya njia ya mkojo (ya kawaida zaidi kwa wanawake kutokana na urethra fupi) yanaweza kuondoka katika kibofu, na kuongeza mzunguko wa kukojoa hata baada ya maambukizi kupita.

Nenda tu "haidhuru"

Tabia za kwenda msalanai zinaweza kutofautiana kutokana na tamaduni tofauti. Lakini tangu umri mdogo, wasichana wengi mara nyingi hufundishwa "kwenda msalani mara kwa mara ili kuepuka vyoo vya umma. Tabia hizi zinaweza kusababisha kibofu cha mkojo kuwa tupu kabla ya wakati, kupunguza uwezo wake wa kujinyumbua na kunyooka.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika trimester ya mwisho ya ujauzito, shinikizo kwenye kibofu husababisha wanawake kulazimika kwenda chooni mara nyingi zaidi.

Wanaume, kwa upande mwingine, kwa kawaida hupewa uhuru zaidi au kuhimizwa kusubiri. Mtu yeyote ambaye amewahi "kukalia kiti cha choo pia atatambua kuwa kujali kwa usafi huathiri tabia.

Kwa wakati, kibofu cha mkojo hujifunza. Huwezi kubadilisha ukubwa wake, lakini unaweza kufundisha uvumilivu wake.

Mafunzo ya kibofu, mbinu iliyokuzwa na Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza na Jumuiya ya Wapasuaji wa Urolojia ya Uingereza, inahusisha kuongeza hatua kwa hatua muda kati ya safari ya kwenda msalani.

Hii husaidia kurejesha uwezo na kupunguza hisia ya uharaka za kwenda msalani .

Mara nyingi pamoja na mazoezi ya sakafu ya pelvic, ni njia ya ufanisi na isiyo ya haraka ya kurejesha udhibiti, hasa kwa wale wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kibofu au kushindwa kujizuia.

Wanawake wanaweza wasiwe na kibofu kidogo zaidi, lakini wana nafasi ndogo ya kujizuia, kimaumbile. Wakati mwingine mtu anapozungusha macho wakati wa mapumziko ya kwenda msalani, mkumbushe si kuhusu nia dhaifu au kibofu kidogo . Ni juu ya maumbile, tabia, na homoni.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla