Kwanini mwandishi huyu wa michezo wa Rwanda aliamua kutoroka nyumbani?

Chanzo cha picha, P NSENGUMUKIZA
Kuangazia michezo nchini Rwanda,ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola wiki hii, kwa kawaida ni inachukuliwa kuwa moja ya maeneo salama zaidi kwa waandishi wa Habari, lakini kwa Prudence Nsengumukiza hofu ya mara kwa mara ya kumkwaza mtu aliye madarakani imekuwa juu sana.
Baada ya kukamilisha ukaaji wa uandishi wa Habari wa mwezi mmoja katika Jumba la Makumbusho la Kifalme la Afrika ya Kati nchini Ubelgiji mwaka jana, kijana huyo mwenye umri wa maiaka 33 aliamua kutafuta hifadhi katika mamlaka ya zamani ya kikoloni.
Haukua uamuzi aliouchukua kwa uwepesi- kwani sasa anahofia kuwindwa na mawakala wa serikali ya Rais Paul Kagame, ambao wanafahamika kwa kuwalenga wakosoaji waliopo nje ya nchi.
Tunapozungumza, hataki kutoa maelezo zaidi kuhusu mahali mahali alipo
"Unajua jinsi huduma za usalama za Kigali zinavyofanya kazi. Wana watu kila mahali. Naweza kukuelezea mahali nilipo hivi sasa na siku hiyo hiyo wanaweza kunipata," anacheka kwa kwa hofu.
Sasa anaendesha tuvuti ya kigeni inayokospa serika, moja ya makumi ya tuvuti zilizofungiwa nchini Rwanda.
Tovuti ya nyumbani inayohusishwa na serikali imemtuhumu kwa "uoga" na "kujitafutia riziki kwa kuchafua nchi iliyokupa maziwa", ikionya "pia ni usaliti na hakuna anayesaliti Rwanda na kupata bahati".
Mtangazaji huyo wa michezo alikuwa amefanya kazi katika kampuni ya vyombo vya habari inayounga mkono serikali, ambayo mmoja wa wanahisa wake, wafanyakazi wanaamini, ni jeshi.

Chanzo cha picha, AFP
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Alitoa mfano jinsi hata taarifa ya soka inavyoweza kukuingizamashakani.
Mnamo mwaka wa 2019 APR FC inayomilikiwa na jeshi, iliyoshikilia rekodi ya ubingwa katika ligi kuu ya nchi hiyo, ilitimua wachezaji 16 kutokana na uchezaji mbaya - jambo ambalo Nsengumukiza alitaka kuchunguza kwa kutumia historia yake ya kisheria kama mhitimu wa sheria.
"Nilikuwa na nia ya kumhoji mwanasheria na kuchunguza vifungu vya sheria [kwa wachezaji]... Lakini wazo hilo lilitupiliwa mbali katika mkutano wa asubuhi wa wahariri, baadhi yao wakibishana kuwa wazo hilo halingepokelewa vyema."
Shirika la kutetea haki Human Rights Watch limeandika jinsi uhuru mdogo wa kujieleza unavyovumiliwa nchini Rwanda, likinukuu katika ripoti ya hivi majuzi kwamba karibu wanaYouTube wanane wanaochukuliwa kuwa wakosoaji wa serikali wamefunguliwa mashtaka mwaka uliopita.
Hii ni pamoja na kifungo cha miaka saba jela kwa Dieudonné Niyonsenga, maarufu kama "Cyuma Hassan", ambaye aliwarekodi wakazi kama wanajeshi wakiwafukuza kwa nguvu wakati wa kibali cha makazi duni.
Moja ya mashtaka aliyokabiliwa nayo ni "kudhalilisha mamlaka ya kitaifa na watu wanaosimamia utumishi wa umma".
Chaneli yake Ishema TV, ambayo haipatikani tena kwenye YouTube, ilipata umaarufu wakati alipoangazia mazishi ya 2020 ya mwimbaji wa nyimbo za injili Kizito Mihigo na kubaini majeraha usoni kwenye maiti.
Hii ilionekana kupinga msimamo rasmi kuhusu kifo cha mwanaharakati huyo wa amani na maridhiano - kwamba alijitoa uhai akiwa katika seli ya polisi siku chache baada ya kukamatwa akijaribu kukimbia nchi.

Chanzo cha picha, KIZITO MIHIGO PEACE FOUNDATION
Kitabu cha Bad News cha Anjan Sundaram kinaonyesha ukandamizaji huo, kikiorodhesha waandishi wa habari 60 ambao walipigwa, kukamatwa, kuuawa au kulazimishwa kukimbia baada ya kuikosoa serikali ya Rwanda kati ya 1995 na 2014.
Mmoja wa wanahabari hao ni Eleneus Akanga mwenye umri wa miaka 39, ambaye aliwahi kufanya kazi katika gazeti linalounga mkono serikali la New Times na pia aliwahi kuwa mwasilishaji taarifa kwa mashirika ya habari ya Associated Press na Reuters.
Safari yake ya kuwa mkimbizi nchini Uingereza ilianza mwaka wa 2007 baada ya baadhi ya waandishi wa ndani kukasirishwa.
"Niliketi na mhariri wangu na nikasema: 'Tunahitaji kujua ni nani anayewapiga watu hawa kwa sababu wanahabari hawa walikuwa wakidai kuwa ni maajenti wa serikali wanaowapiga," aliambia BBC.
Iliamuliwa kwamba haingewezekana kuripoti hili - lakini baadaye, ofisi ya rais ilidai kufutwa kwake "kwa jinsi inavyoonekana kuandika hadithi ambayo ilitaka kuiweka Rwanda katika dharau na washirika wake wa maendeleo".
Baada ya kufutwa, Akanga alijaribu kuanzisha gazeti la kikanda, la Weekly Post, lakini baada ya toleo lake la kwanza alizuiliwa na kufutiwa leseni.
Rafiki yake alidokeza kwamba kukamatwa kwake kulikuwa karibu - kwa tuhuma za kuwa jasusi - na alifanikiwa kukimbia.
Miaka 15 baadaye, sasa ni wakili na raia wa Uingereza.

Chanzo cha picha, PA Media
"Kusema ukweli sijapata vitisho vyovyote maalum nchini Uingereza. Lakini bado nachukua tahadhari kama itabidi… kuepuka baadhi ya maeneo ambayo ninahisi yamechukuliwa na baadhi ya maajenti wa Rwanda."
Na anashindwa kuelewa ni kwa nini Uingereza - nchi ambayo ilimchukua kama mtafuta hifadhi - inapeleka wale wanaohitaji msaada mahali palipo na rekodi mbaya ya haki za binadamu, chini ya mpango tata wa hifadhi ya Rwanda.
"Nadhani ni sera ya ajabu. Nijua jinsi inavyotisha wakati unakimbia mahali fulani na unatarajia kupata hifadhi ya aina fulani katika nchi ambayo umeichagua."
Serikali ya Rwanda inasisitiza kuwa makubaliano hayo na Uingereza yanatoa suluhisho la uhamiaji haramu, kuwapa watu usalama na fursa.
Pia mara kwa mara inapuuza wasiwasi juu ya rekodi yake ya haki za binadamu, ikisema hakuna mtu anayeweza kuhutubia Rwanda juu ya mada hiyo, ikiongeza kuwa ina mifumo ya haki na ya uwazi - na haijawahi kutoa maoni rasmi kuhusu kesi za Nsengumukiza na Akanga.
Jumuiya ya Madola yaombwa kuchuka hatua
Kwa mwanasayansi wa siasa wa Ubelgiji Prof Filip Reyntjens, mmoja wa wataalam wakuu katika eneo la Maziwa Makuu, hali ya Nsengumukiza na Akanga unaonyesha kile anachokiita "Wanyarwanda wawili".
Moja ni mzuri katika kusimamia misaada kutoka nje, kukabiliana na rushwa na kufanya vyema katika ngazi ya kiteknolojia ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika.
"Lakini kwa upande mwingine ... unakumbana na mazingira yasio na usawa, serikali ya chama kimoja, vikwazo vikubwa vya uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, kukamatwa kiholela kinyume cha sheria na, kutoweka na hata mateso ya wapinzani wa Rwanda katika mipaka yote ya nchi,” aliambia BBC.

Chanzo cha picha, AFP
Rwanda ya kwanza ndiyo inayovutia mataifa wafadhili, ambayo yanaiona kuwa historia ya mafanikio kwa wakazi wake milioni 13, ingawa imesalia kuwa miongoni mwa nchi 25 maskini zaidi duniani.
Rwanda iliruhusiwa kujiunga na Jumuiya ya Madola mwaka 2009, licha ya kundi lililoundwa kutetea haki za binadamu katika nchi wanachama kutoa wasiwasi. Ilitarajiwa uanachama wake ungeleta mabadiliko.
"Lakini kwa hakika hali haijaimarika kadri muda unavyosonga.
Kama kuna jambo lolote litakuwa baya zaidi leo kuliko wakati Rwanda ilipojiunga na Jumuiya ya Madola," Prof Reyntjens anasema, akinukuu ripoti ya mwaka huu ya shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu nchini Marekani la Freedom House ambayo inaorodhesha Rwanda kama nchi "isiyo huru", ikiwa na jumla ya alama 22/100.
Mnamo 2014, hata BBC Idhaa ya Kinyarwanda - ambayo ilianzishwa mwanzoni baada ya mauaji ya halaiki ya 1994 kama huduma ya kuokoa maisha - ilipigwa marufuku (na haijarudi hewani) kwenye masafa FM kufuatia filamu ya BBC Two kupinga kauli rasmi ya serikali kuhusu mauaji hayo.












