Tetesi za soka Ulaya Jumapili 23.06.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wanakaribia kumsajili Dominic Calvert-Lewin, Wolves wanakataa ofa ya Newcastle kwa Max Kilman, na Douglas Luiz anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Juventus.
Newcastle United wanakaribia kuinasa saini ya mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 27, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Everton. (Guardian)
Newcastle pia wametoa ofa ya fedha pamoja na mchezaji kwa beki wa kati wa Wolves Muingereza Max Kilman, 27. (Telegraph – Subscription Required }
Wolves tayari wamekataa ofa ya Kilman kutoka Newcastle ambayo pia iliuliza kuhusu kumsajili winga wa Ureno Pedro Neto, 24. (HITC).

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa Aston Villa Douglas Luiz anakaribia kuhamia Juventus na anatazamiwa kufanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo nchini Marekani, ambapo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko kwenye majukumu ya Copa America na Brazil. (Gianluca di Marzio – in Italy }
Manchester City na Manchester United zilichukua hatua za kuchelewa kumsajili Michael Olise, ambaye anatarajiwa kujiunga na Bayern Munich, huku zote zikiangalia uwezekano wa kumruhusu winga huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 kusalia na Crystal Palace kwa mkopo kabla ya kujiunga nao msimu ujao (Mirror).
Mshambulizi wa Uingereza Marcus Rashford, 26 ameapa kurekebisha uhusiano wake uliovunjika na Erik ten Hag baada ya Manchester United kuthibitisha kuwa Mholanzi huyo atasalia kama meneja. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wanajiandaa kupokea ofa nyingine kutoka kwa Manchester United kwa ajili ya mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21, baada ya hapo awali kukataa kandarasi iliyopunguzwa bei. (Mail)
Everton wako kwenye mazungumzo na Newcastle kuhusu kumsajili winga wa Gambia Yankuba Minteh, 19. (HITC),
Newcastle wamekataa nia ya awali kutoka kwa Liverpool ya Minteh, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Feyenoord chini ya mkufunzi mpya wa Liverpool Arne Slot. (Football Insider),
Aston Villa wameuliza kuhusu kupatikana kwa kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Brais Mendez, 27. (Express).

Chanzo cha picha, Reuters
Tottenham hawana nia ya kusalimu amri kwa Real Madrid au klabu nyingine yoyote inayotarajia kumsajili beki wa Argentina Cristian Romero, 26, msimu huu wa joto. (Football Insider).
Brighton wana nia ya kumsajili winga wa Uturuki Baris Alper Yilmaz, 24, kutoka Galatasaray. (Telegraph – Subscription Required }.
Juventus wanaweza kumpeana mshambuliaji wa Italia Federico Chiesa, 26, kama sehemu ya mpango unaowezekana wa kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 22. (La Gazzetta dello Sport – In Italia }

Chanzo cha picha, Marc Atkins/Getty
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mshambulizi wa Uholanzi Xavi Simons ameiambia Paris St-Germain kwamba anataka kuondoka msimu huu wa joto, huku Bayern Munich wakijaribu kupata mkataba wa mkopo na wajibu wa kununua, huku RB Leipzig wakitumai kumsajili tena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye alikuwa akihudumu kwa mkopo msimu uliopita. (Fabrizio Romano)
Beki wa Ujerumani Joshua Kimmich hana uwezekano wa kuongeza mkataba wake na Bayern Munich zaidi ya 2025 na klabu hiyo ya Ujerumani iko tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 msimu huu wa joto. (Sky Sport Germany).
Jaribio la Leeds kutaka uhamisho wa Joe Rodon kutoka Tottenham kuwa wa kudumu linakaribia kuporomoka kwani kuna uwezekano mkubwa wa kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, huku Leicester, Ipswich na Southampton zikiwa na nia ya kumnunua beki huyo wa Wales, 26. (Football Insider).
Manchester United wako tayari kusubiri miezi tisa mingine kwa Dan Ashworth kuanza kazi kama mkurugenzi wao mpya wa michezo. (Sun)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












