Faida tano kuu za maji ya kunywa kiafya

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Sote tunajua ni muhimu mwili wako kuwa na maji, lakini kwa nini?

Tulimuuliza mtaalamu wa lishe Nicola Shubrook atueleze faida tano kuu za kunywa maji ya kutosha.

Maji ni nini?

Maji ni kioevu kisicho na rangi kinachojumuisha hidrojeni na oksijeni (H20).

Ni muhimu kwa maisha, ingawa hakina kalori.

Kunywa kiasi cha kutosha cha maji, au mwili wako kuwa na maji, ni kanuni ya kwanza ya afya na lishe.

Miili yetu inaweza kudumu kwa wiki nzima bila chakula, lakini ni siku tu unaweza kuhimili bila maji.

Inaleta maana tunapojua kwamba mwili wetu umeundwa na takriban 60% ya maji na kwamba upungufu wa maji mwilini unaweza kuwa na matokeo ya kimwili na kiakili.

Faida za maji

Mchanganyiko halisi wa ya glasi yako ya maji inategemea chanzo chake.

Maji ya madini na maji ya chemchemi, ambayo kwa kawaida hutoka kwenye hifadhi na chemchemi za chini ya ardhi, yanaweza kutoa virutubisho vya ziada katika mfumo wa madini kama vile kalsiamu na magnesiamu.

Je, ni faida gani 5 kuu za kiafya za maji ya kunywa?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

1. Inabororesha kumbukumbu

Utafiti umeonyesha kuwa hata upungufu wa maji mwilini kidogo unaweza kuathiri kumbukumbu na hali ya kila mtu kutoka kwa watoto hadi wazee.

Upungufu wa maji huathiri ubongo, na pia mwili, na utafiti umeonyesha kuwa hata upungufu wa maji mwilini unaweza kuathiri vibaya hali na kuongeza wasiwasi.

Ukosefu wa maji pia unaweza kuongeza hatari ya maumivu ya kichwa au kipandauso kwa baadhi ya watu.

2. Inaweza kusaidia kudumisha uzito

Ubongo hauelezi tofauti kati ya njaa na kiu, kwa hivyo mara nyingi tunachanganya kiu na " tamaa ya sukari." 

Wakati mwingine unapotamani kitu kitamu, jaribu glasi ya maji kwanza.

Mwili kuwa na maji pia inaweza kusaidia kudumisha uzito.

Utafiti umeonyesha kuwa kunywa maji kabla ya mlo kunaweza kukufanya ujisikie umeshiba na hivyo kukuza kupunguza uzito kwa kukandamiza hamu yako ya kula.

Hili ndilo linalojitokeza kutokana na utafiti wa 2015 ambapo laini vyepesi vilibadilishwa na maji.

Matokeo yalionyesha kuwa inaweza kusababisha kupunguza uzito zaidi na kupinga insulin isiingie.

3. Inaweza kuboresha utendaji wa mwanariadha

Utafiti mwingi umefanywa juu ya madhara ya kupungua kwa maji mwilini wa wanariadha, na matokeo yake yamehitimisha kwamba upungufu wa maji mwilini huathiri tu utendaji wa mwanariadha, lakini pia kisaikolojia.

4. Huenda ikazuia kuvimbiwa

Maji husaidia "kufanya mambo" katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, hivyo kukaa na maji kunaweza kusaidia kuzuia kuvimbiwa kwa watoto, watu wazima, na wazee.

Inaweza kuonekana kuwa maji yana faida sana.

5. Inaweza kusaidia afya ya mfumo wa mkojo

Upungufu wa maji mwilini unaweza kuongeza hatari ya kutokea au kujirudia kwa mawe kwenye figo kwa baadhi ya watu.

Uchunguzi umeonyesha pia kwamba kunywa maji ya kutosha kunaweza kupunguza hatari ya magonjwa ya kibofu na ya mkojo, ikiwa ni pamoja na kufura kwa kibofu cha mkojo ambako kawaida husababishwa na maambukizi ya kibofu kwa wanawake.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni kiasi gani cha maji kinachopendekezwa?

NHS (Huduma ya Afya ya Umma ya Uingereza) inapendekeza mtu mzima kunywa wastani wa glasi 6-8 za maji kila siku.

Hii ni pamoja na maziwa yenye mafuta kidogo, vinywaji visivyo na sukari kidogo au sukari, chai na kahawa.

Hata hivyo, hii inaweza kutofautiana kulingana na umri wako, jinsia na kiwango cha shughuli.

Kwa mfano, unaweza kuhitaji maji zaidi ikiwa unafanya mazoezi au ikiwa kuna joto jingi.