Je, ni kwanini watoto wa miaka 6 hupata hedhi?

Madaktari wanasema kuna sababu nyingi za kubaleghe mapema

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Madaktari wanasema kuna sababu nyingi za kubaleghe mapema
    • Author, deepali jagtap, Sushila Singh
    • Nafasi, Mwakilishi wa BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

"Nina uoga kumuona mwanagu wa kike wa miaka sita anabadili umbo lake. Anakuwa na hasira kwa vitu vidogo .mabadiliko haya yananipa wasiwasi.”

Haya ni maneno ya Archana(sio jina halisi),ni mkaazi wa kijiji cha Satara katika mkoa wa Maharashtra akisimulia mabadiliko anayoyaona kwa binti yake.

Ni familia inayoishi mashinani ,akiwa na mumewe ambaye ni mkulima wamebarikiwa Watoto wawili kifungua mimba ni msichana. Mtoto wake wa kike alianza kuona mabadiliko ya kiutuzima kwa mtoto wake na kuamua kumpeleka hospitali kupata ushauri wa daktari.

Naye Rashi mkaazi wa Delhi nchini India pia alianza kuona mabadiliko katika mwili wa mtoto wake wa kike ambapo alidhani ni kawaida. Mtoto wake wa miaka sita kuwa na uzani wa kilo 40 ,alifurahia kuwa ana afya bora.

Lakini mambo yakabadilika siku moja msichana wa Rashi alianza kuvuja damu. Alipomtafutia matibabu alijulishwa wazi kuwa binti yake ameanza kupata hedhi.

Kubalehe huanza kati ya miaka 8 hadi 13 kwa wasichana na 9 hadi 14 kwa wavulana.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kubalehe huanza kati ya miaka 8 hadi 13 kwa wasichana na 9 hadi 14 kwa wavulana.

Mambo ambayo huwatia wasiwasi wanawake

Imekuwa vigumu kukubali nilichoambiwa na daktari. Anasema Rashi,”msichana wangu haelewi kinachotokea.”

Kwa upande mwengine ,Archana alimshauri amuone mtaalam wa masuala ya uzazi ambaye alimkagua mwanae.

Archana alimleta msichana wake na baada ya vipimo tuliona ana dalili za kubaleghe. Umbile lake linafanana na mtoto wa miaka 14 hadi 15.hedhi yake huenda ikaanza muda wowote kutoka sasa,”alisema dkt. Sushil Garud wa hospitali ya Motherhood ,Pune.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Dkt.Sushil anasema kuwa viwango vya homoni kwa wasichana ni mara tatu ya umri wao ,na kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha hili.

"Archana anasema kuna vikebe vya dawa ya kuua wadudu vya 5kg ambavyo mtoto wake alikuwa akichezea .huenda ikawa ni chanzo kikuu cha homoni zake kubadilika ,”daktari alitoa maoni.

Dkt.Sushil alisema kuwa kuna mabadiliko ya mapema katika mwili wa mtoto kwa jina Precociouspuberty kwa lugha ya matibabu yaani kupevuka haraka.

Kwa mujibu wa tovuti ya National Center for Biotechnology Information (NCBI), kubaleghe ni sehemu ya maisha ambapo mwili na akili hukumbwa na mabadiliko makubwa ya kukua kutoka utotoni kuelekea ujanani na hatimae utu uzimani. Kubalehe huanza kati ya miaka 8 hadi 13 kwa wasichana na miaka 9 hadi 14 kwa wavulana.

Mtaalamu wa uzazi dkt.S.N.Basu amesema wasichana hubaleghe haraka ukilinganisha na wanaume.

"Hapo awali, tuliona kuwa wasichana wanapata hedhi kati ya mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu baada ya mabadiliko ya kimwili. Sasa wasichana wanapata hedhi ndani ya miezi mitatu hadi minne,” alisema Dkt. Vaisakhi Rustegi.

Vaisakhi Rustegi ni mtaalamu wa magonjwa ya watoto na endocrinologist ambaye hutibu matatizo ya homoni kwa vijana . Alielezea kuwa hivi sasa wavulana wanamea ndevu na masharubu ndani ya mwaka mmoja na nusu tangu kuanza kubaleghe, jambo ambalo hapo awali lilikuwa linachukua miaka minne.

Binti wa Archana na Rashi kwa sasa wanapata matibabu.

Utafiti wa ICMR-NIRRCH wa wasichana 2,000 umebaini kuwa akina mama hawawezi kutambua dalili za kubalehe kwa binti zao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utafiti wa ICMR-NIRRCH wa wasichana 2,000 umebaini kuwa akina mama hawawezi kutambua dalili za kubalehe kwa binti zao.

Sababu za kubaleghe mapema ni zipi?

Kulingana na takwimu za NCBI…kubaleghe kwa watoto husababisha mabadiliko ya mwili na akili na mabadiliko hayo huwapa msongo wa mawazo.

Dkt. Suchitra Sarve kutoka Idara ya Utafiti wa Afya ya Watoto katika Baraza la Utafiti wa Matibabu la India, Maharashtra, alisema kuwa visa vya Watoto kupevuka haraka vimeongezeka katika utafiti wake.

Utafiti uliofanywa na ICMR-NIRRCH kwa wasichana 2,000 ulibaini kuwa kina mama wengi hawawezi kutambua dalili za kubalehe kwa mabinti zao. Shirika hili linachunguza sababu na hatari za kupevuka haraka kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka tisa.

Daktari kutoka Mumbai, Dkt. Prashanth Patil, alisema kuwa sumu za kemikali za kilimo ni sababu ya mabadiliko ya kimwili kwa binti ya Archana mwenye umri wa miaka sita. Ingawa hii ni sababu nadra, anasema kuwa dawa za kuua wadudu zinaweza kusababisha kubalehe mapema kwa sababu zinahusiana na mabadiliko ya homoni.

“Wakulima hutumia aina mbalimbali za dawa za kuua wadudu ili kulinda mazao. Dawa hizi huingia mwilini kwa njia ya pua na mdomo. Pia huingia mwilini kupitia chakula. Zinaathiri tezi inayodhibiti homoni kwenye ubongo,” alisema Dkt. Avinash Bhondve, rais wa zamani wa Chama cha Madaktari wa India, Mumbai.

Mbali na hayo, wakulima hutumia homoni ili kuongeza kasi ya ukuaji wa mboga au kuongeza maziwa kutoka kwa ng’ombe na mbogo. Hii pia ina madhara kwa mwili, alisema.

Madaktari wanasema kuwa unene kupita kiasi kwa watoto wakati wa Corona pia ni sababu ya kubalehe mapema

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Madaktari wanasema kuwa unene kupita kiasi kwa watoto wakati wa Corona pia ni sababu ya kubalehe mapema

‘hedhi huanza wakati wowote’

Kufikia sasa madaktari hawajabaini kisababishi cha kubaleghe mapema japokuwa utafiti unaendelea.

Kwa mfano katika hospitali ya BJ Wadia iliyoko Mumbai iliandaa kambi ya kubaleghe mapema 2020 kwa ushirikiano na ICMR,wasichana wa miaka 6 hadi 9 walifanyiwa uchunguzi.

"Wasichana 60 walio na umri kati ya miaka 6 hadi tisa wameonyesha dalili za mapema za kubalehe .wengine wanapata hedhi ,”alisema dkt. Sudharai,ambaye anafanya kazi katika kitengo cha Watoto katika hospitali hiyo.

Dkt. Sudharao kutoka BJ Wadia Hospital alisema kuwa unene wa mwili pia ni sababu ya mapema kubalehe. Utafiti umeonyesha kuwa unene wa watoto umeongezeka wakati wa janga la Corona, hivyo kuongeza tatizo hili.

Madaktari wanasema kunenepa kupita kiasi, kuangalia sana TV au skrini ya simu, na ukosefu wa mazoezi huchangia kubalehe mapema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Madaktari wanasema kunenepa kupita kiasi, kuangalia sana TV au skrini ya simu, na ukosefu wa mazoezi huchangia kubalehe mapema.

Tafiti zilizofanywa

Sambamba na unene kupita kiasi ,utumizi wa rununu ,televisheni au kuangalia kioo na kutofanya mazoezi pia zimetajwa kusababisha kubaleghe mapema ,wataalam wa afya wamesema.

Aidha utafiti unaendelea ili kujua kinachosababisha Watoto kubaleghe mapema .Dawa za kuua wadudu ,viungo vya kuhifadhi chakula ,uchafuzi wa mazingira huenda unachangia.Pia vinasaba vya mtu pia huchangia kupevuka upesi,Basu anaeleza.

Dkt. Vaisakhi alisema kuwa kwa miaka miwili au mitatu iliyopita, ameshuhudia visa vitano hadi sita za watoto wa kike wanaopata hedhi kila siku kwenye kliniki yake.

Madaktari pia wanasema kuwa kina mama wengi wameripoti kuwa mabinti zao huanza mabadiliko ya maumbile mwezi Aprili na wanaanza kupata hedhi mwezi Juni na Julai.Pia Watoto wa kiume wameanza kuonyesha dalili kama hizo.

Pia kuangalia skrini kwa muda mrefu huchangia kubaleghe kwa haraka.

Homoni ijulikanayo melatonin husaidia ubongo kupata usingizi na pia kupunguza homoni za jinsia.hata hivyo kutumia simu,tv au skrini huathiri mtu kupata usingizi .hali hiyo hutatiza homoni ya melatonin na kupelekea homoni za jinsia kuongezeka kwa haraka, alielezea Dkt. Vaisakhi.

Wataalamu pia wanasema kuwa kemikali zilizomo kwenye kitakasa mkono zinaweza kuingia mwilini kupitia ngozi na kuathiri homoni.

Dkt SN Basu amesema mwili wa binadamu una homoni yakisspeptin ambayo hukuza kubalehe kwa mapema.Inaaminika kutatiza usawa wa homoni na kusababisha kubalehe.lakini haya yote yanaendelea kujadiliwa.

Mabinti wa Archana na Rashi wamedungwa sindano ili kuzuia hedhi hadi watakapofikia umri sahihi. Daktari anasema kuwa wasichana wa umri huo hawajaiva vya kutosha wala hawana ufanisi wa kudumisha usafi wakati wa hedhi.

Vilevile, madhara ya kubalehe mapema yanaonekana kisaikolojia, kwani wasichana wengine wanaweza kuonekana tofauti na wenzao, jambo linaloweza kuleta changamoto za kijamii na kihisia.

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Seif Abdalla