Miji ghali zaidi duniani kuishi 2022

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mji wa New York nchini Marekani ni kati ya miji inayoongoza orodha hiyo

Miji ghali zaidi duniani ni New York na Singapore, kulingana na utafiti wa kila mwaka wa Kitengo cha Ujasusi cha Economist (EIU).

Ni mara ya kwanza New York inaongoza orodha hiyo. Nambari ya kwanza ya mwaka jana, Tel Aviv, sasa iko katika nafasi ya tatu.

Kwa ujumla, wastani wa gharama ya kuishi katika miji mikubwa zaidi duniani imeongezeka kwa 8.1% mwaka huu, uchunguzi wa EIU unaripoti.

Vita nchini Ukraine na athari za Covid zilitambuliwa kama sababu za ongezeko hilo.

Mfumuko wa bei ulikuwa wa juu sana Istanbul - na bei ilipanda kwa 86% - Buenos Aires (64%) na Tehran (57%).

Mfumuko wa bei wa juu nchini Marekani ulikuwa mojawapo ya sababu za New York kuongoza orodha.

Los Angeles na San Francisco pia ziliingia kwenye orodha 10 bora - mapema mwaka huu, mfumuko wa bei wa Marekani ulikuwa wa juu zaidi katika zaidi ya miaka 40.

Dola ilioimarika pia ilikuwa sababu ya umaarufu wa miji ya Marekani.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Moscow na St Petersburg zilitoka nafasi ya 88 na 70 na kupanda daraja, hadi nafasi za 37 na 73 mtawalia, ikiwa ni matokeo ya vikwazo vya Magharibi kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Utafiti huo unalinganisha gharama katika dola za Marekani kwa bidhaa na huduma katika miji 173. Kyiv haikujumuishwa katika orodha ya mwaka huu.

EIU ililinganisha zaidi ya bei 400 za watu binafsi katika bidhaa na huduma 200 kutoka miji 172 kote ulimwenguni.

Upasana Dutt, anayehusika na kuongoza utafiti huo, alisema vita vya Ukraine, vikwazo vya Magharibi kwa Urusi na sera za sifuri za Uchina "zimesababisha shida za usambazaji wa bidhaa".

"Hilo, pamoja na kupanda kwa viwango vya riba na mabadiliko ya viwango vya ubadilishaji, vimesababisha shida ya gharama ya maisha ulimwenguni kote," Bi Dutt aliongeza.

Alisema wastani wa kupanda kwa bei katika miji 172 katika uchunguzi wa EIU imekuwa "nguvu zaidi ambayo tumeona katika miaka 20 ambayo tuna data ya kidijitali".

Miji ghali zaidi Duniani 2022..

1 = New York

1 = Singapore

3 = Tel Aviv

4 = Hong Kong

4 = Los Angeles

6 = Zurich

7 = Geneva

8 = San Francisco

9 = Paris

10 = Sydney

10 = Copenhagen

Miji yaenye gharama ya Chini zaidi kuishi Duniani

161 = Colombo

161 = Bangalore

161 = Algiers

164 = Chennai

165 = Ahmedabad

166 = Almaty

167 = Karachi

168 = Tashkent

169 = Tunis

170 = Tehran

171 = Tripoli

172 = Damascus

Source: EIU's World Cost of Living index