Je, Israel itaiburuza Marekani kwenye vita vikali huko Mashariki ya Kati?

meli

Chanzo cha picha, AFP

Inaonekana kwamba njia za mawasiliano bado ziko wazi kati ya pande zinazohusika katika mzozo wa eneo la Mashariki ya Kati na bado zina uwezo wa kudhibiti kasi ya matukio tete katika eneo hilo.

Israel, bila tangazo rasmi, ilijibu shambulizi la Iran alfajiri ya Ijumaa na inaonekana ilitumia ndege tatu zisizo na rubani ambazo kuna uwezekano mkubwa zilirushwa kutoka ndani ya ardhi ya Iran.

Hii ilikuja siku chache baada ya jibu la Irani, kwa shambulio la Israel kwenye ubalozi mdogo huko Damascus na Iran ilishambulia kwa zaidi ya droni 300 na makombora.

Mashambulizi hayo bado hayajasabisha machungu, kwani si Iran wala Israel iliyoripoti uharibifu mkubwa kutokana na mashambulizi hayo.

Wengine hata walielezea kama mchezo wa kuigiza. Je, Marekani inafanya kazi kwa siri nyuma ya pazia?

Ni wazi kwamba Washington iliweza kwa namna fulani kutuliza makabiliano kati ya Israel na Iran, lakini vita vya Gaza bado vinaendelea, hasa kwa vile Israel ingali inatishia kuvamia Rafah yenye wakazi wengi.

Mashambulizi ya Iran yalikwenda umbali wa takriban kilomita 1,200, kufikia vilindi vya Israeli

Chanzo cha picha, Reuters

Je, vita vya Gaza vinaweza kutenganishwa na mzozo wa Mashariki ya Kati?

Lengo la kijeshi la Iran na washirika wake katika ukanda huenda usitatue matatizo ya msingi. Mbinu hii imeonekana kutofaa kwa sababu Gaza ni sehemu ya Mashariki ya Kati. Je, Washington inatambua kwamba ufunguo wa utulivu katika eneo hilo ni usitishaji vita huko Gaza?

Operesheni za kijeshi na makabiliano ya moto na maneno yalipunguzwa sana kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, ambayo yalisababisha makubaliano ya kubadilishana kati ya Israel na Hamas, yaliyopatanishwa na Misri na Qatar, mwishoni mwa 2023.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hata hivyo, pamoja na Marekani kukubaliana kwa kiasi kikubwa na msimamo wa Israel, matamshi ya maafisa katika utawala wa Biden yanaonesha kwamba Ikulu ya White House inataka kutopanua vita, lakini haichukui hatua yoyote ya kivitendo kukomesha vita vya Gaza.

Biden anajaribu kusawazisha misimamo na kutumia nguvu ya kutosha kulinda maslahi ya Marekani, kwa njia ambayo haileti makabiliano makubwa zaidi.

"Biden hataishinikiza Israel hadharani," anasema Trita Parsi wa The Nation.

Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya majeruhi huko Gaza, ambayo ilizidi watu 100,000 waliokufa, kujeruhiwa na kupotea, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, Rais wa Marekani alizungumza, kwa mujibu wa tovuti ya Politico, kuhusu usimamizi mbaya wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika vita hivyo huko Gaza na kusema, “Nafikiri anachofanya si sahihi. Sikubaliani na mtazamo wake.”

Kauli hizi hazikutosha kusitisha uungwaji mkono wa kijeshi, kwani Biden alisafirisha zaidi ya tani 10,000 za silaha kwa Israel, mara mbili alipita Congress ili kuharakisha uhamishaji wa silaha, na alitumia kura yake ya turufu mara nne katika Baraza la Usalama kuzuia maamuzi, pamoja na usitishaji mapigano. .

Kwa mujibu wa The Nation, alijadili jinsi ya kuwahamisha kabisa Wapalestina milioni 2.3 kutoka Gaza hadi jangwa la Sinai, licha ya msimamo uliotangazwa wa Marekani kupinga kuhama makazi yao.

Licha ya yaliyoripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani kuhusu kuibuka dalili za mgawanyiko kati ya Washington na Israel kuhusiana na mbinu iliyotumika katika vita hivyo, afisa huyo wa Ikulu ya Marekani amesema: Tunaendelea kuiunga mkono Israel na haki yake ya kujilinda bila ya masharti, kwani masharti sio sehemu ya sera yetu.

Taarifa hii inakuja licha ya kile washirika wa Biden wanasema ndani. Chama cha Democratic kilisema kuwa serikali inapaswa kunyima silaha kutokana na Israel kushindwa kuepusha vifo vya raia.

Seneta Chris Van Hollen alisema, "Tunahitaji kuunga mkono maneno kwa vitendo, na utawala wa Biden lazima utumie ushawishi wake ipasavyo kabla ya kutoa mwanga wowote wa kijani kutuma mabomu zaidi."

Lakini tofauti kati ya maneno na vitendo bado ni kubwa. Biden alimwomba Netanyahu kutuma timu ya maafisa wa usalama mjini Washington ili kujadili pendekezo la Marekani la kupunguza idadi ya majeruhi wakati wa kuivamia Rafah, ambayo ina watu wengi waliokimbia makazi na raia.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Israel ilitumia sana mabomu yenye uzito wa tani 2,000 huko Gaza, hasa katika shambulio la mabomu kwenye kambi ya Jabalia Oktoba 31, na kusababisha mauaji ya watu 100, kwa mujibu wa duru za Umoja wa Mataifa.

"Hii inawafanya maafisa wote wa kisiasa na kijeshi nchini Marekani kushiriki katika uhalifu wa kivita wa Israel," alisema Josh Paul, afisa wa zamani wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ambaye alijiuzulu wadhifa wake kupinga uhamishaji wa silaha kwa Israel bila masharti.

Marekani pia inatambua kwamba kivuko cha Rafah kinajumuisha kivuko kikubwa cha misaada ya kibinadamu, na ongezeko lolote la mapigano litazidisha janga hilo, lakini juhudi za Ikulu ya White House zilikuwa na mipaka ya kuahirisha uvamizi wa Rafah, na sio kuzuia. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, uvamizi huu unatarajiwa mwezi Mei.

Rais wa Marekani, Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

Chanzo cha picha, Reuters

Je, vitendo vya Ikulu ya Marekani vinafungua njia ya upanuzi wa vita?

Tangu Oktoba 7, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, vita vimekuwa kwa Israel kana kwamba havina mwisho. Mbinu ya Israel imekuwa tishio la moja kwa moja kwa malengo yaliyotangazwa ya Biden. Israel inaonekana kutaka kupanua vita kutoka Gaza hadi Lebanon na pengine Yemen na hata Iran.

Kupanua vita kwa ajili ya Marekani si kwa maslahi yake.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller alithibitisha kwamba mojawapo ya vipaumbele vya Waziri wa Mambo ya Nje Anthony Blinken ni kuwashawishi washirika na wengine katika eneo hilo kutumia ushawishi wao kuzuia ongezeko lolote. Alikiri kuwa hii ndiyo hatari halisi na kuweka wazi kuwa hakuna maslahi ya mtu yeyote kwa mzozo huo kuenea zaidi ya Gaza.

Lakini data ya msingi haiendani kabisa na taarifa hizi.

Marekani iliwakusanya washirika wake kuiunga mkono Israel kiusalama, kijeshi na kisiasa, lakini wakati huo huo iliionya Iran na washirika wake dhidi ya kuwaunga mkono Wapalestina kijeshi au kisiasa ili kuepuka kupanua vita. Hata hivyo, pamoja na ushawishi wake, haikuweza kusimamisha vita vya Gaza, au pengine haikutafuta kufanya hivyo.