Moqtada al-Sadr: Takriban watu 15 wameuawa katika mapigano jijini Baghdad

Sadir
Maelezo ya picha, Wafuasi wa n Moqtada al-Sadr wakivamia kasri ya rais baada ya kustaafu

Takriban watu 15 wameuawa katika makabiliano baina ya vikosi vya usalama na wafuasi wa kiongozi wa kidiniwa Shia mwenye mamlaka makubwa yaliyoendelea usiku kucha katika mji mkuu Baghdad.

Ghasia hizo zimeibuka baada ya Bw Sadr kutangaza kujiuzulu siasa

Maafisa wanasema watu wengine wengi wamejeruhiwa baada ya wafuasi wa Muqtada al-Sadr kuvamia kasri ya rais.

 Waziri Mkuu wa Iraq wa muda ametoa wito wa kuwepo kwa hali ya utulivu na jeshi limetangaza amri ya kutotoka nje usiku baada ya fujo kuzuka katika miji kadhaa.

Sadr ni mtu mwenye mamlaka zaidi wa Iraq, ambaye amekuwa akihusika na mzozo wa muda mrefu wa kuunda serikali.

Moqtada al-Sadr, ambaye ni kiongozi wa ngazi ya juu wa kidini wa madhehebu ya Shia mwenye wafuasi mamilioni, alitangaza uamuzi wake kwenye Twitter.

Watu kadhaa waliripotiwa kuuawa katika makabiliano baada ya wafuasi wake kuvamia kasri la rais.

Mamia wamekuwa wakikita kambi nje ya jengo la bunge kwa wiki kadhaa baada ya kulivamia kupinga mkwamo wa kisiasa.

Tangazo la kujiuzulu kwa Bw Sadr limekuja siku mbili baada ya kuziita pande zote za kisiasa na watu waliohusika katika maisha ya kisiasa kufuatia uvamizi ulioongozwa na Marekani kuondoka uongozini.

Muungano wake ulishinda vingi kati ya viti katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, lakini wabunge wake baadaye walijiuzulu kutokana na mkwamo wa kisiasa kati yao na kikundi kingine hasimu cha Kishia kuhusu uteuzi wa Waziri mkuu mpya.

Sadir
Maelezo ya picha, Wafuasi wa Moqtada al-Sadr walilivamia bunge mara mbili hivi karibuni
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wafuasi wa Bw Moqtada al-Sadr hivi karibuni walivamia mara mbili bunge, alisema katika taarifa : "Ilibidi niamue kutoingilia katika masuala ya kisiasa, lakini sasa ninatangaza tangazo langu la mwisho la kustaafu na kufunga taasisi zote za [Kiadr ] ." Baadhi ya maeneo ya kidini yanayohusika na vugu vugu lake yataendelea kufunguliwa.

Shirika la habari la Iraq -INA, baadaye liliripoti kwamba Bw Sadr pia alitangaza mgomo wa chakula hadi pale ghasia na matumizi ya silaha vitakapositishwa

Bw Sadr, mwenye umri wa miaka 48, amekuwa mtu mwenye mamlaka makubwa katika umma wa Iraqi na katika maisha ya kisiasa kwa miongo miwili.

Jeshi lake la Mehdi Army lilijitokeza kama mojawapo ya wanamgambo wenye nguvu zaidi waliopigana na Marekani na vikosi vya washirika wao -serikali ya Iraqi baada ya uvamizi ambao walimpindua mtawala wa zamani Saddam Hussein.

Baadaye alilipatia jina jipya kama vikosi vya amani (Peace Brigades) , na wakasalia kuwa ndio wapiganaji wakubwa ambao kwa sasa wanaunda sehemu ya vikosi vya Iraqi.

Ingawa jeshi la Mehdi lilikuwa na uhusiano na Iran, Bw Sadralijitenga na majirani wa Iraq Washia na alijionyesha kama mtaifa anayetaka kumaliza ushawishi wa Marekani na Iran katika masuala ya ndani ya Iraq.

Hasimu wake wanasiasa wa Kishia nchini Iraqi, mfumo wa uratibu, ambao vugu vugu la Bw Sadr limekuwa na ugomvi nao unajumuisha zaidi vyama vinavyoungwa mkono.

Bw Sadr, mmoja wa watu wanaotambuliwa zaidi nchini Iraqi akiwa na kilemba chake cheusi, macho yenye rangi nyeusi, na mweney umbo kubwa la mwili aliwaongoza Wairaqi wa kawaida waliokuwa wameathiriwa na ukosefu wa hali ya juu wa ajira, uhaba wa umeme wa mara kwa mara na ufisadi.

Ni moja wa watu wachache ambao wangeweza kuwakusanya mamia kwa maelfu ya wafuasi kuingia mitaani, na kuwaondoa tena. Mamia wamekuwa wakipiga kambi nje ya bunge tangu walipolivamia mara mbili katika mwezi Julai na Agosti kupinga mkwamo wa kisiasa.