Uingereza inaweza kupigana kwa muda gani ikiwa vita vitazuka?

.
Muda wa kusoma: Dakika 5

Vita kamili vya Urusi dhidi ya Ukraine hivi karibuni vitaingia mwaka wake wa tano. Matukio ya ajabu ya kile kinachoitwa "vita vya mseto" yanaongezeka huko Uropa, na hivyo kuongeza mvutano.

Na nchini Uingereza, wakuu wa kijeshi wameonya kwamba lazima tujiandae kwa vita ikiwa tunataka kuviepuka. Lakini ikiwa jambo lisilofikirika lingetokea, na vita na Urusi vikazuka, je, Uingereza inaweza kupigana kwa zaidi ya wiki kadhaa?

"Hatuna mpango wa kuingia vitani na Ulaya. Lakini kama Ulaya inataka na kuanza, tuko tayari hivi sasa." Ndivyo alivyosema Rais wa Urusi Vladimir Putin tarehe 2 Disemba, akizishutumu nchi za Ulaya kwa kuzuia juhudi za Marekani kuleta amani nchini Ukraine.

Ili kuwa wazi, hakuna uwezekano mkubwa kwamba Uingereza ingeweza kujikuta katika vita na Urusi peke yake, bila kuungwa mkono na washirika wa Nato.

Lakini maneno ya Putin yalikuwa ukumbusho wa kusikitisha kwamba vita kati ya Urusi na nchi za Nato, ikiwa ni pamoja na Uingereza, haviko mbali kama watu walivyotarajia.

Pia unaweza kusoma

Jinsi vita vinaweza kuonekana katika nyakati hizi za teknolojia

"Naam hilo sio suala la kawaida . Sina mtandao kwenye simu yangu." "Mimi pia siko mtandaoni. Nini kinaendelea?" Hali hiyo, kwa nadharia, ni njia moja tu tunaweza kujua kwamba vita na Urusi vimeanza, au vilikuwa karibu.

(Ninapaswa kuongeza kuwa kunaweza pia kuwa na sababu zingine, nzuri kabisa za upotezaji wa mtandao)

Ukatizaji huo wa mtandao unaweza kufuatiwa na kutoweza kufanya malipo ya benki kwa vitu muhimu kama vile chakula na mafuta.

Usambazaji wa chakula ungetatizwa, usambazaji wa umeme ungeathiriwa.

.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Hatuna mpango wa kwenda vitani na Ulaya. Lakini ikiwa Ulaya inataka, na kuanza, tuko tayari hivi sasa,' Putin alisema
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuna njia nyingi za kupigana vita, na sio tu wimbi la uharibifu la ndege zisizo na rubani , mabomu na makombora ambayo yanajulikana sana kwa raia wa Ukraine.

Jamii yetu ya kisasa, inayoendeshwa na teknolojia inategemea sana mtandao wa nyaya na mabomba ya chini ya bahari ambayo huunganisha Uingereza na dunia nzima, inayobeba data, miamala ya kifedha na nishati.

Shughuli za siri za meli za kijasusi za Kirusi, kama vile Yantar, zinaaminika kuwa zilitafuta nyaya hizi kwa hujuma inayoweza kutokea wakati wa vita, ndiyo maana Jeshi la Wanamaji la Kifalme hivi karibuni limewekeza katika kundi la ndege zisizo na rubani za chini ya maji zilizo na vitambuzi vilivyounganishwa.

Katika vita, vitendo hivi vilivyofichika, visivyoonekana, pamoja na jaribio lisiloepukika la "kupofusha" satelaiti za Magharibi katika anga za juu, zingezuia kwa kiasi kikubwa uwezo wa Uingereza wa kupigana, pamoja na uwezekano wa kusababisha uharibifu kwa mashirika ya kiraia.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nchini Uingereza, wakuu wa kijeshi wameonya kwamba lazima tujiandae kwa vita ikiwa tunataka kuiepuka

Katika mkutano wa hivi majuzi mjini London ulioitwa Kupambana na Vita Virefu, ulioandaliwa na Taasisi ya Royal United Services (Rusi), taasisi ya wataalam ya Whitehall, maafisa wa kijeshi na kisiasa walikutana kujadili ikiwa vikosi vya sasa vya Uingereza vitakuwa na uwezo wa kuendeleza mzozo wa muda mrefu kabla ya kuishiwa na kila kitu kutoka kwa wanajeshi, risasi hadi vipuri.

"Bado kuna ushahidi mdogo kwamba Uingereza ina mpango wa kupigana vita vya zaidi ya wiki chache," anasema Hamish Mundell wa Rusi. "Uwezo wa matibabu ni mdogo. Mabomba ya kurejesha hifadhi ni ya polepole... Mpango wa Uingereza wa matokeo ya majeruhi wengi unaonekana kutegemea kutochukua majeruhi."

Kwa maneno machache ya kawaida ya Uingereza, anasema: "Hii inaweza kuchukuliwa kuwa dhana ya kupanga yenye matumaini."

Anaongeza kuwa ili kupigana vita virefu unahitaji usaidizi sahihi. "mpangilio wa zana za kwanza na za pili na hata za tatu; wanajeshi, majukwaa na minyororo ya vifaa ambayo inaweza kukabiliana na hasara na kuendeleza mapambano. Hata hivyo kina hiki hakipo katika muundo wa sasa wa jeshi la Uingereza."

Jeshi la Urusi lenye 'kiwango cha chini'

"Kuna upungufu wa risasi, silaha, magari, ulinzi wa anga, na maafisa, na uwezo mdogo wa kuzalisha vitengo au majeruhi," anasema Justin Crump, Mkurugenzi Mtendaji wa Sibylline, kampuni ya kibinafsi ya kijasusi.

Mafunzo mawili makubwa ya kijeshi kutoka kwa vita vya Ukraine ni kwamba ndege zisizo na rubani sasa ni muhimu kwa vita vya kisasa, katika kila ngazi, na pili, "misa", au idadi kubwa ya wanajeshi na vifaa vya kijeshi, ni muhimu.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Kuna upungufu vifaa vya kijeshi kama vile risasi, magari, ulinzi wa anga, na wanajeshi," anasema Justin Crump.

Jeshi la Urusi kwa ujumla lina kiwango cha chini cha ubora. Wanajeshi wake hawana vifaa vya kutosha, wanaongozwa vibaya na wanalishwa vibaya. Matarajio ya maisha yao katika "eneo hatari la ndege zisizo na rubani" mashariki mwa Ukraine ni mafupi.

Idara ya Ujasusi ya Ulinzi ya Uingereza inakadiria kuwa tangu kuanza kwa uvamizi kamili mnamo Februari 2022 jeshi la Urusi limepata hasara zaidi ya maafisa milioni 1.1 - ambao wameuawa, kujeruhiwa, kukamatwa au kutoweka.

Hatahivyo makadirio ya kihafidhina yanaweka idadi ya Warusi waliouawa kuwa 150,000. Ukraine pia imepata maafa makubwa lakini idadi ni ngumu kubaini.

Lakini Urusi imeweza kutumia kundi kubwa la wanajeshi kiasi kwamba hadi sasa imeweza kuchukua nafasi ya makadirio ya vifo vyao vya kila mwezi vya 30,000 katika uwanja wa vita .

Uchumi wa Urusi pia umekuwa kwenye mkondo wa vita kwa zaidi ya miaka mitatu sasa: mwanauchumi amewekwa jukumu la Wizara ya Ulinzi, wakati viwanda vyake vinatengeneza zaidi ndege zisizo na rubani, makombora na vifaru.

Kulingana na ripoti ya hivi majuzi ya Taasisi ya Kiel ya Uchumi wa Dunia, Urusi imekuwa ikitengeneza kila mwezi karibu vifaru 150, magari 550 ya kivita mapigano , ndege 120 za Lancet na zaidi ya vipande 50 vya mizinga.

Uingereza, na washirika wake wengi wa Magharibi, hawako popote karibu kufikia hilo.

Wachambuzi wanasema itachukua miaka kadhaa kwa viwanda vya Ulaya Magharibi kukaribia uzalishaji wa silaha wa Urusi kwa wingi.

"Vita vya ardhini nchini Ukraine vimeonyesha bila shaka kwamba wingi ni muhimu kabisa kwa mtu yeyote ambaye atakabiliana na Urusi ardhini," anasema Keir Giles, mtaalam wa Urusi katika jumba la wataalam la Chatham House.

"Na kuwa na akiba kubwa zaidi kwa idadi kuliko vikosi vya kawaida vya jeshi kumeonyeshwa kuwa muhimu."