'Nilibakwa na afisa wa polisi'

g
Maelezo ya picha, Lauren alisema ingawa mbakaji wake sasa yuko jela hawezi "kusahau na kuendelea na maisha kama kawaida"

Lauren Taylor alikuwa na umri wa miaka 16 tu alipobakwa na afisa wa Polisi wa jiji la London mnamo 2010.

Adam Provan alikuwa karibu mara mbili ya umri wake lakini alimdanganya, akimwambia kwamba alikuwa na umri wa miaka 22 na kuahidi kwenda naye kwenye sinema.

Lakini kwanza, alinieleza kuwa alitaka waende kutembea katika bustani huko Romford, London mashariki. Badala yake, alimpeleka kwenye pori na kumbaka.

Zaidi ya muongo mmoja baadaye, Provan amehukumiwa katika Mahakama ya Taji ya Wood Green kwa uhalifu huo.

Afisa huyo wa zamani wa polisi ya jiji la London au Met, 44, kutoka Newmarket huko Suffolk, alifungwa jela miaka 16 na mingine minane kwa kosa la kuwa na leseni iliyoongezewa muda kinyume cha sheria,na makosa mawili ya ubakaji dhidi ya Lauren, pamoja na makosa sita ya kumbaka afisa mwenzake wa polisi wa kike kati ya 2003 na 2005.

Lakini imechukua miaka kadhaa - na kesi tatu - kupata haki kwa wanawake.

"Niliishiwa na nguvu kutokana na hofu, nadhani," Lauren alisema. "Hivyo ndivyo nilivyofanikiwa kupitia kiwewe kizima na kufika nyumbani salama - ilikuwa ni kujifanya sipo, kujifanya kuwa si mimi. Haikuwa ikinitokea."

Lauren alisema Provan alijifanya kana kwamba hakuna kilichotokea baada ya kumbaka, kumnunulia maziwa yaliyotiwa ladha (milkshake) na baadaye kumbaka tena.

Ilichukua miaka sita kwake kuhisi kuwa na uwezo wa kuripoti uhalifu huo kwa polisi.

g

Chanzo cha picha, MET HANDOUT

Maelezo ya picha, Lauren alikuwa na umri wa miaka 16 pekee wakati afisa wa polisi Adam Provan alipombaka

Kesi ya kwanza ya Provan iliishia kwenye mahakama ya Hung na katika kesi yake ya pili 2018 alipatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaji na alifungwa jela miaka tisa. Alifukuzwa kazi katika polisi ya London (Metropolitan) mnamo 2019, lakini hatia yake ilibatilishwa baada ya kukata rufaa.

Hata hivyo, kulikuwa na mwanamke mwingine ambaye alikuwa amehudhuria mahakamani na kusikiliza taarifa ya athari ya Lauren.

Alikuwa afisa wa Polisi wa London kama Provan. Na alikuwa amembaka pia.

Wakati wa kesi ya tatu mwaka huu mahakama ilisikia kwamba afisa huyo wa kike aliwaambia wakuu wa Met Provan alimbaka na kumdhulumu miaka mingi kabla ya kesi ya Lauren, lakini aliambiwa anyamaze kuhusu hilo kwa ajili ya kazi yake.

w

Chanzo cha picha, MET POLICE

Maelezo ya picha, Hapo awali Provan alifungwa jela miaka tisa kwa ubakaji wa Lauren, lakini hukumu yake ilifutwa

Mwanamke wa pili aliiambia mahakama katika taarifa ya athari za mwathiriwa kuwa "alikuwa mwathiriwa, lakini nilihisi kama mshukiwa", na kuongeza " kuwa alihisi kuonewa na kudhulumiwa" kazini.

Jaji Lucas alisema alishugulikiwa na polisi kwa namna "ya kuzimu" na "ya kushtua".

'Ukweli ulinifanya niendelee'

Licha ya uzoefu wa kubakwa mwanamke mwingine kwa jina Lauren alisema anawashukuru maafisa wengine wa polisi kwani uhusiano wao umekuwa mzuri sana na anawashukuru kwa msaada wao.

Lauren ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 29, ana haki ya kisheria ya kubaki mwathirika wa unyanyasaji wa kingono bila asiiyetambuliwa kwa jina, lakini anataka kushirikisha masaibu yake ili kuwahimiza watu wengine waliopitia unyanyasaji kama alioupitia kujitokeza.

"Kugundua kuwa alikuwa afisa wa polisi ilinisikitisha ," alisema. "Ilinichukua ujasiri na nguvu nyingi kwenda polisi.

g
Maelezo ya picha, Lauren alisema ukweli ndio "kitu pekee kilichonifanya niendelee"

Katika taarifa yake ya athari ya mwathiriwa iliyosomwa kwa mahakama, alielezea kuwa mahusiano yake yamevunjika kutokana na ubakaji na athari za kutoa ushahidi, na bado anapitia "kumbukumbu mbaya na kukanganyikiwa mara kwa mara".

Ingawa "anashukuru" Provan amerejea jela, ana hasira ilibidi apitie kesi nyingine.

"Kusema ukweli, sijisikii kama nimekuwa na nguvu sana. Lakini ninahisi kama mtu pekee anayeweza kufanya chochote kuhusu hilo ni mimi," alisema.

"Najua ukweli, na hilo ndilo jambo pekee lililonifanya niendelee."

'Haki ya ukatili’

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Akitoa hukumu kwa Provan, Jaji Lucas alimwambia mshtakiwa kuwa alionyesha "haki ya kujamiiana bila huruma".

Jaji alisema alisikitishwa na jinsi polisi ya London ilivyoshughulikia malalamiko ya awali ya afisa huyo wa kike dhidi ya tabia ya Provan mwaka wa 2005, akisema wale waliokuwa kwenye kikosi hicho "walijali zaidi kumlinda mmoja wao kuliko kuchukulia makosa aliyoyafanya kwa uzito".

Wakati wa kesi majaji walifahamishwa kwamba tabia ya unyanyasaji ya Provan ilianza miaka ya 1990 na alidaiwa kuwasiliana na msichana wa miaka 16 baada ya kutoa maelezo yake kama shahidi mnamo 2003.

Afisa mwingine wa kike alilalamika mwaka 2005 kwamba Provan alimtumia jumbe za "kero" lakini suala hilo lilishughulikiwa kwa njia "isiyo rasmi", mahakama iliambiwa.

Hakimu Lucas alimwambia mshitakiwa: “Uvumilivu na uzito wa kosa lako uko wazi unapowekwa katika masharti haya magumu.

"Kwa matendo yako umeleta fedheha kwa jeshi la polisi."

Kamishna Msaidizi wa Polisi ya london, Louisa Rolfe, alielezea vitendo vya Provan kama "vya kusikitisha kabisa".

"Tunachunguza historia ya uhalifu na mwenendo wa Provan katika Met ili tuweze kuelewa kikamilifu ikiwa tungeweza kuchukua hatua mapema kumfikisha mahakamani, au kumzuia kujiunga na polisi," alisema.

"Tunaweza kuona tayari kulikuwa na wakati muhimu ambapo tuliwaangusha wanawake na hatukufanya kila tuwezalo kuwaunga mkono.

"Tumeiambia Ofisi Huru ya Maadili ya Polisi tunafanya uhakiki na kuwashauri kwamba tutatoa rufaa zinazofaa," alisema.