'Sikujua kuwa ubakaji ni kitu ambacho wanaume pia hupitia'

ALEX FEIS-BRYCE

Chanzo cha picha, ALEX FEIS-BRYCE

Alex Feis-Bryce alikuwa na umri wa miaka 18 wakati alipobakwa na mtu asiyemjua kwenye sherehe.

Hivi karibuni alijitokeza kama mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja, na akahama kutoka mji wao mdogo kwenda Manchester kusoma.

"Nadhani ilikuwa mara ya pili kwenda kwenye baa ya wapenzi wa jinsia moja. Mimi na rafiki yangu tulikutana na watu wengine ambao walitualika kwenye karamu ya nyumbani. Nilikuwa nataka kupata marafiki na kuwa wazi na watu. Nilikubali lakini rafiki yangu akabadilisha mawazo dakika za mwisho".

Alex alipelekwa kwenye nyumba moja anakoamini alipewa dawa za kulevya.

"Mtu ambaye alikuwa ana miliki nyumba aliniwekea dawa kwenye kinywaji na nikaanza kuhisi kisunzi. Alinipeleka chumbani na muda si mrefu alikuja pale na kunibaka. Nilihisi kana nimebanwa kitandani".

Alex alikubali kurudishwa hadi chuo kikuu kutoka kwa mtu huyo wakati anajaribu kunyamazisha kile kilichotokea.

"Kwa kweli nilifikiri ubakaji sio kitu kinachotokea kwa wanaume, kwa hivyo labda haikuwa kitu kilichonitokea. Nilifanywa nifikirie kuwa hili linatokea kwa wanawake tu, na hiyo ilifanya iwe ngumu zaidi kuendeleza mchakato au kuripoti kwa polisi kwasababu sikudhani nitaaminika", anasema.

ALEX FEIS-BRYCE

Chanzo cha picha, ALEX FEIS-BRYCE

Alex sasa ni mtendaji mkuu wa manusura Uingereza, katika shirika la kusaidia wanaume na wavulana ambao wamebakwa, kunyanyaswa kingono au kudhalilishwa.

Wakati waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia wana uwezekano mkubwa wa kuwa wa kike, utafiti wa Uhalifu kwa England na Wales unakadiria kuwa mmoja kati ya wanaume 100 alipata aina fulani ya unyanyasaji wa kijinsia au kujaribu kushambuliwa, katika mwaka hadi Machi 2020.

Mwaka jana, Reynhard Sinaga - "mbakaji mashuhuri zaidi katika historia ya sheria ya Uingereza" - alipatikana na hatia ya kuwadanganya wanaume 48 kutoka nje ya vilabu vya Manchester hadi kwenye gorofa yake, sio mbali sana na baa ambayo Alex alifikishwa.

Sinaga aliwatilia dawa za kulevya na kuwanyanyasa wanaume hao - huku akipiga picha za kitendo hicho.

Walionusurika katika utafiti uliofanywa Uingereza wanasema wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia mbili wanaweza kuwa na uwezekano wa kukumbwa na unyanyasaji wa kijinsia zaidi kuliko wanaume kwa ujumla.

Katika kura yao iliyoshirikisha wanaume 505 wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia mbili, asilimia 47 walisema wamewahi kunyanyaswa kijinsia, na zaidi ya theluthi moja wakisema wanahisi hawawezi kuzungumza na mtu yeyote juu ya kile kilichotokea.

Ni muhimu kutambua kwamba unyanyasaji mwingi wa kijinsia "hufanyika katika maisha ya ngono tuliyo nayo", Alex anasema.

Hatutaki kuingiza imani potofu kwamba wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja au jinsia mbili ni wazinzi zaidi au wanatafuta kitu fulani, lakini tunataka kukumbuka nafasi za watu ambao wanafanya mapenzi ya kawaida, ila wakashinikizwa hadi kufika mwisho na kuanza kushiriki mapenzi ya jinsi moja. Lakini muhimu zaidi ni kufanya utafiti bila unyanyapaa.

Mtu mmoja tu kati ya saba waliohojiwa katika utafiti wao uliofanywa Agosti iliyopita, ndio alikuwa ameripoti tukio la unyanyasaji wa kijinsia kwa polisi.

Kati ya wale ambao walifanya hivyo, karibu robo moja walihisi hawaamini au waliona kuwa malalamiko yao hayakuchukuliwa kwa uzito.

"Ni juu ya idhini. Kwa mfano, ngono yoyote ambayo sio ya kawaida au ya kawaida - ngono na zaidi ya mpenzi mmoja [kwa mfano] inaweza kunyanyapaliwa sana", Alex anasema.

Kwa hivyo, ikiwa mtu atakumbana na unyanyasaji wa kijinsia katika hali kama hizo atakuwa na uwezekano mdogo wa kuzungumza na polisi".

Kutokana na utafiti wetu tunajua kwamba wengi hawatajitokeza kamwe, na kuwaacha washughulikie kile kilichowapata bila msaada wa kitaalam. Lazima tuhakikishe simulizi ya umma juu ya unyanyasaji wa kijinsia inajumuisha waathirika wote, na kwamba kila aliyenusurika unyanyasaji wa kijinsia anaweza kupata msaada anaohitaji".

Lee

Chanzo cha picha, Getty Images

Lee ambaye [sio jina lake halisi] alikuwa na miaka 15 alipolazwa hospitalini baada ya kujidhuru mwenyewe akihangaika kukubalika hali yake ya kushiriki ngono.

Huko alinyanyaswa kingono na mshauri wa kiume kwa zaidi ya mwaka - uzoefu ambao anasema ulisababisha miaka mingi ya mfadhaiko wa akili.

"Kwa muongo mzuri ulioshuhudia uzoefu huo kwa viwango vingine vya utendaji wangu. Unyanyasaji wa kingono au vurugu ilikiwa kama kawaida na sikujitunza vizuri".

"Nilihitaji kutuliza kichwa changu lakini tiba ikawa machafuko na nikasababisha shida nyingine kwa mimi mwenyewe, kutumia dawa za kulevya na ngono kushughulikia usumbufu anbao mizizi yake ni jambo jingine".

"Na wakati alipoomba msaada, yeye mwenyewe pia hakujua ikiwa kile kilichompata kilikuwa unyanyasaji wa kijinsia".

Labda aliona kile alichonifanyia kama sio kibaya - hakunipiga ngumi wala kunipiga teke, hakunibaka na hiyo ilijitokeza kwamba hakuona kuna umuhimu wa kupata idhini yangu kufanya alichofanya.