'Je, Israel inaweza kuishinda Hamas na kuhakikisha amani Gaza?'

Chanzo cha picha, Reuters
Vita vya Gaza kati ya Wapalestina na Israel, ambavyo vimeingia mwezi wake wa pili, vinaendelea kugonga vichwa vya habari duniani.
Tunaanzia kutoka kwenye ukurasa wa makala za maoni katika gazeti la Uingereza la The Times, na makala ya mwandishi Anshel Pfeffer yenye kichwa cha habari "Je, Israel inaweza kuishinda Hamas na kuhakikisha amani Gaza?.
Mwandishi anaanza makala yake kutoka kwa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Jumapili jioni, na kundi la waandishi wa habari wa Israeli kuwajulisha juu ya hali ya hivi karibuni katika vita mjini Gaza.
Mwandishi huyo anasema kuwa Netanyahu alionekana kuwa "mcheshi" na "asiye wazi" alipoulizwa kuhusu mipango ya Israel baada ya vita. Alijibu kuwa Israel itadumisha "udhibiti wa usalama" juu ya Ukanda wa Gaza baada ya kuiondoa Hamas, na kuongeza kuwa "haioni Israeli ikiwa haina jukumu kamili la usalama huko Gaza."
Anshel anashangaa jibu hili linamaanisha nini; Je, inamaanisha kwamba vikosi vya Israel na vifaru vitasalia ndani ya Gaza baada ya mapigano kumalizika? Au inamaanisha kuanzisha eneo la kijeshi kwenye mpaka wa Gaza? Je, vikosi vyote vya ardhini vitaondolewa na kurudishwa baadaye ikiwa Hamas itatokea tena? Kama ni hivyo, ni nani atakayechukua jukumu la Ukanda wa Gaza na idadi ya watu wake zaidi ya milioni mbili baada ya Hamas? Inaonekana kuwa Netanyahu hana maelezo zaidi.
Mwandishi anaamini kuwa Netanyahu yuko katika hali ya kutatanisha. Tangu Oktoba 7, umaarufu wa wake umekuwa ukipungua kulingana na kura za maoni, na mapambano yake ya kudumisha msimamo wake yatategemea iwapo muungano wake wa mrengo wa kulia ubaki upande wake. Kwa hivyo, Netanyahu hataongeza wazo la Mamlaka ya Palestina kuchukua utawala wa Ukanda wa Gaza; hii itahatarisha idadi kubwa ya watu ambao serikali yake bado inafurahia uwepo wao bungeni.
Kwa upande mwingine, ikiwa ataidhinisha baadhi ya mipango ya washirika wake wa mrengo wa kulia kuanzisha uwepo wa kudumu wa Israeli huko Gaza, ataukasirisha utawala wa Biden, ambao unaipa Israel msaada muhimu wa kijeshi na kidiplomasia. Netanyahu hakutaja chochote kuhusu mkakati wa Israel wa kuondoka Gaza.
Mwandishi huyo anaongeza kuwa matumaini pekee ya Netanyahu sasa ni kwamba Israel inaweza kupata ushindi wa haraka wa kijeshi dhidi ya Hamas, ambayo yatafufua matarajio yake ya kisiasa yaliyofifia.
"Mamlaka ya Palestina haina uwezo wa kusimamia sekta hiyo."
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa mujibu wa kura za maoni, asilimia 85 ya Waisraeli wanaunga mkono kuingia kwa jeshi ili kuharibu uwezo wa kijeshi wa Hamas na kuilazimisha kuachia madaraka Gaza. Lakini hakuna makubaliano juu ya nini kinapaswa kutokea baadaye.
Mwandishi anaongeza kuwa kuna mazungumzo, hasa kutoka kwa wanasiasa wenye wam rengo wa kuli, juu ya "kurudi" kwa Ukanda wa Gaza na kujenga upya makazi ya Israeli ambayo yaliondolewa na serikali ya Ariel Sharon mnamo 2005 wakati Israeli ilijiondoa kutoka Gaza.
Anshel anaamini kuwa ndoto za kujenga upya makazi ya walowezi wa Israel huko Gaza hazizingatii raia milioni mbili wa Palestina wanaoishi huko katikati ya vifusi. Bila kusahau kutengwa kimataifa na mwisho wa uhusiano wa Israeli na tawala za Kiarabu zenye misimamo ya kadri.
Mwandishi anataja suluhisho linalopendelewa la upinzani wa Israeli, ambalo ni kuhamisha udhibiti wa Ukanda wa Gaza kwa Mamlaka ya Palestina, lakini haoni wazo la wazi la jinsi Mamlaka ya Palestina inaweza kuwa na uwezo wa kurejesha uwepo wake huko sasa.
Mwandishi anasema kuwa Mamlaka ya Palestina haina uwezo, vikosi vya usalama, au miundombinu ya kiraia ya kutawala Gaza.
Anshel anahitimisha makala yake kwa kusema kwamba ikiwa Israel itajiondoa kutoka Gaza baada ya kumalizika kwa mashambulizi yake ya ardhini na kufanikiwa kudhoofisha uwezo wa Hamas wa kutawala, kikosi cha kimataifa cha kulinda amani kitahitajika kwa kipindi cha mpito kinachoongezwa kwa miezi kadhaa, kabla ya Mamlaka ya Palestina kuwa tayari kuchukua jukumu. Lakini hadi sasa, hakuna nchi ya - Kiarabu au ya Magharibi – iliyojitole kutoa vikosi vyake kwa ajili ya operesheni Inayoendelea Gaza.
"Taifa la Palestina bado ni wazo hatari."
Tukiangalia gazeti la Israel la The Jerusalem Post, ambalo lilichapisha makala ya maoni ya mwandishi Moshe Philips yenye kichwa cha habari "Taifa la Palestina bado ni wazo hatari."
Mwandishi anasema licha ya shambulio la ghafla la Hamas mnamo Oktoba 7, Rais wa Marekani Joe Biden bado anashinikiza kuundwa kwa taifa huru la Palestina la Kiarabu pamoja na taifa la Kiyahudi. Kwa bahati mbaya, haonekani kuelewa kwamba Oktoba 7 imebadilisha kila kitu.
Moshe anaongeza kuwa utata juu ya kuanzishwa kwa taifa la Palestina unahusu masuala mawili makuu: nia ya Waarabu wa Palestina na mipaka halisi ya taifa hili.
Kwa mtazamo wa mwandishi, Waarabu wa Palestina wameshindwa mara mbili kuthibitisha nia yao nzuri ya kuishi kwa amani pamoja na Israeli.
Mwandishi anaongeza kuwa jaribio la kwanza lilikuwa katika kipindi cha kati ya 1993-1995, wakati Israeli ilisaini Mkataba wa Oslo na "kukabidhi zaidi ya asilimia 40 ya Yudea na Samaria" (Ukanda wa Magharubi) kwa Mamlaka ya Palestina.
Moshe anaamini kuwa tabia ya aliyekuwa Rais wa Mamlaka ya Palestina, Yasser Arafat, na mrithi wake, Mahmoud Abbas, ilipaswa kuonyesha kwamba ilikuwa salama kuwapa taifa kamili.
Mwandishi anaendelea kusema kwamba Arafat alionyesha kinyume kabisa. Anaelezea baadhi ya mifano ya hili na kusema: "Mamlaka ya Palestina iliwahifadhi na kuwalipa magaidi, ilifadhili mashambulizi ya kigaidi kupitia Brigedi za Al-Aqsa Martyrs zilizo na uhusiano na Fatah, ilichochea chuki dhidi ya Wayahudi kupitia vyombo vya habari, na kufanya biashara kubwa ya silaha, kama vile Operesheni Karen A." Watu ambao wanataka amani hawahitaji tani za roketi haramu, bunduki na mabomu."
Jaribio la pili la nia ya Wapalestina ni kujisalimisha kwa Israel kwa Gaza. Moshe anashangaa nini udhibiti wa Waarabu wa Palestina juu ya Gaza unamaanisha, na anasema: "Walijenga jeshi la kigaidi, na kudondosha makombora kutoka juu ya anga la Israeli."
Vipi kuhusu mipaka halisi ya nchi iliyopendekezwa?
Mwandishi anasema kuwa kila ramani iliyopendekezwa kwa "suluhisho la mataifa mawili" inahitaji kuondolewa kwa Israeli kwenye mipaka ya 1949-1967, ambayo iko maili tisa.
Sababu ya hii inatokana na kwamba miji ya Mamlaka ya Palestina kama Tulkarm na Qalqilya iko maili tisa kutoka Bahari ya Mediterania - na Mamlaka ya Palestina haitaacha miji hiyo.
Pia anaongeza kuwa uondoaji huu unamaanisha kuwa sekta kuu ya kimkakati ya Israeli haiwezi kuzuilika. Miji mikubwa nchini Israel na uwanja wa ndege wa Ben Gurion vitalengwa kirahisi na makombora ya "magaidi waliowekwa upande wa Palestina" wa mpaka, alisema.
Kwa mtazamo wa Moshe, suala la usalama wa Israeli sio suala pekee. Kuna ukweli muhimu wa kihistoria, kama taifa la Kiarabu la Palestina lililoanzishwa mnamo 1922, wakati Waingereza walitenganisha asilimia 78 ya eneo la Palestina kutoka nchi nyingine, na kubadilisha jina la eneo hilo kuwa "Mashariki ya Jordan". Baadaye, walilibadilisha kuwa "Jordan".
Mwandishi anaamini kuwa kubadilisha jina hakubadilishi utambulisho wa raia wake. Idadi kubwa ya Wajordan ni Waarabu wa Palestina. Kwa maneno mengine, Jordan tayari ni taifa la Palestina.
Moshe anaongeza kuwa kikwazo pekee cha kuanzishwa kwa taifa la Palestina ni mfalme wa Jordan, ambaye anakataa kufanya hivyo, kama alivyoelezea.
Mwandishi anasema kwamba kwa upande wa Israeli, kwa mfano, madai ya kihistoria, kidini na kisheria ya Wayahudi kwa ardhi ya Israeli yana nguvu zaidi kuliko madai ya Waarabu wa Palestina.
Mwisho, anaongeza kuwa Rais wa Marekani Joe Biden lazima atambue ukweli huu. Lazima akubali ukweli kwamba ulimwengu umebadilika, na kwamba "suluhisho la mataifa mawili" leo linamaanisha hali ambayo Israeli itatishiwa na kurudia kwa uzoefu wa Oktoba 7, na hili ni jambo ambalo hakuna mtu mwenye busara anayeweza kukubali
Kusitisha mapigano ya kibinadamu ni "uhalifu wa kivita"

Chanzo cha picha, Getty Images
Tunasalia katika gazeti la Jerusalem Post, na kusoma makala ya mwandishi Daniel Pomerantz, ambayo anaelezea kwa nini usitishaji mapigano huko Gaza ni "uhalifu wa kivita."
Mwandishi anaanza makala yake kwa kuzungumzia kuhusu mwanajeshi wa Israel Uri Majidish, ambaye jeshi la Israeli lilisema liliweza kumuachia huru wiki iliyopita baada ya "wapiganaji wa Hamas kumteka nyara tarehe 7 Oktoba."
Mwandishi huyo anaongeza kuwa kampeni ya kijeshi inayoongozwa na Israel ya "kutokomeza harakati za Hamas" ni kumbukumbu ya Marekani kuwalenga al-Qaeda baada ya matukio ya Septemba 11, na kwamba lengo lililotangazwa la kampeni hii sio tu kuwakomboa mateka, bali pia kuangamiza harakati za Hamas.
Wakati jeshi la Israel likiendelea na vita vikali vya ardhini katika Ukanda wa Gaza, mashirika kadhaa ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, vinatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.
Kwa mtazamo wa mwandishi, inaonekana kwamba sehemu kubwa ya ulimwengu imepuuza hoja ya msingi, "ambayo ni kwamba Waisraeli ni wanadamu pia," na kwa hivyo usitishaji huu wa mapigano "unaweza kukiuka sheria za kimataifa," kama alivyoelezea.
Mwandishi huyo anamnukuu waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton akisema, "Watu ambao wanadai usitishaji mapigano sasa hawaielewi Hamas, na hii itakuwa zawadi kwa Hamas, kwani watajipa silaha ili kuweza kuzuia shambulio lolote linalowezekana kufanywa na Waisraeli."
Mwandishi anaelezea kwamba kile Clinton anasema kinamaanisha kuwa usitishaji mapigano "utawaathiri Waisraeli," ukweli ambao unafanya kusitishwa kwa operesheni za jeshi la Israeli "kuwa suala gumu kimaadili."
Daniel anaamini kwamba kuachiliwa kwa askari Majidish "kulibadilisha kila kitu." Ukombozi wake umethibitisha kuwa "harakati za jeshi la Israeli ni njia bora ya kuwaokoa mateka," ambayo inamaanisha kuwa kila dakika ambayo jeshi la Israeli linachelewesha opresheni yake ya kijeshi ni dakika nyingine ambayo Waisraeli wasio na hatia wanabaki mateka, anasema.
Mwandishi pia anaamini kwamba chini ya hali hizi, wito wowote wa kuacha mashambulizi kwa jeshi la Israeli ni "mwaliko wa kuendelea na mateso ya Waisraeli, na hakuna kitu cha kibinadamu katika hilo."
Anaongeza kuwa sio tu kwamba usitishaji mapigano wa "kibinadamu" utakuwa wa kimaadili na ukatili kwa wafungwa wa Israeli na familia zao, lakini pia inaweza kusemwa kuwa ni "uhalifu wa kivita," alisema.
Anaendelea kusema kuwa kuwachukua mateka kunachukuliwa kama "ukiukaji mkubwa" wa sheria kadhaa za kimataifa, na kwa hivyo kuingilia kati kuzuia kurudi kwa mateka hawa pia ni "uhalifu wa vita."
Mwandishi anaainisha baadhi ya vifungu vya Mkataba wa Kimataifa dhidi ya utekaji nyara na anasema kwamba Kifungu cha 3 cha Mkataba kinahitaji "kuachiliwa na kuondoka kwa mateka,".
Vipi kuhusu watu wa Gaza?
Mwandishi anaamini kwamba Gaza "haiathiriwi na uhaba wa vifaa vya kibinadamu," pekee bali pia "inakabiliwa na mgogoro wa kibinadamu," na anasema kuwa kuelewa dhana hii ni ufunguo wa kuelewa Gaza.
Mwandishi anasema kuwa mnamo Oktoba 11, mtambo pekee wa umeme huko Gaza uliacha kufanya kazi kwa sababu ya ukosefu wa mafuta, na licha ya hayo, Hamas ilifyatua zaidi ya roketi 8,000 zinazotumia mafuta huko Israeli, na kwa maoni ya mwandishi, Hamas "inaiba rasilimali zote ambazo ulimwengu hutoa kwa Gaza." Karibu kutumika kwa malengo ya kijeshi," anasema.
Mwandishi anahitimisha makala yake kwa kusema kwamba suluhisho pekee la kibinadamu ni "kuiwajibisha Hamas kwa matendo yake," na kwamba chochote chini ya hayo kitajumuisha "uhalifu wa vita dhidi ya Israeli," pamoja na ukiukaji wa kanuni za msingi za maadili ya binadamu, kama alivyoelezea.














