Khamenei aweka masharti matatu kwa ushirikiano wa Iran na Marekani kuafikiwa

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Ali Khamenei
Muda wa kusoma: Dakika 4

Ali Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anasema kuwa Iran na Marekani zina "tofauti za kutoelewana" na "migogoro ya kimaslahi," lakini akaongeza kuwa "ushirikiano" kati ya nchi hizo mbili unawezekana ikiwa masharti fulani yatatimizwa.

Bwana Khamenei akizungumza katika mkesha wa mwaka wa kukaliwa kwa mabavu ubalozi wa Marekani mjini Tehran amesema: "Iwapo Marekani itaacha kabisa uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni, itaziondoa kambi zake za kijeshi katika eneo hilo, na kuacha uingiliaji wake, suala hili linaweza kuchunguzwa."

Hata hivyo kiongozi huyo wa Iran amesisitiza kuwa ombi la Wamarekani la kutaka ushirikiano na Iran halitazingatiwa katika siku za usoni, bali katika siku za baadaye.

Saa chache kabla ya hotuba ya Bw. Khamenei, mahojiano na Rais wa Marekani Donald Trump yalipeperushwa ambapo alisema Iran inatazamia kufikia makubaliano na Marekani.

"Bila shaka hawasemi hivyo na hawapaswi kusema hivyo. Hakuna mpatanishi mzuri angesema hivyo. Lakini Iran inatazamia sana kufanya makubaliano," Bw. Trump alisema katika mahojiano na mtandao wa Marekani wa CBS.

Saa chache kabla ya hotuba ya Bw. Khamenei, mahojiano na Rais wa Marekani Donald Trump yalipeperushwa ambapo alisema Iran inatazamia kufikia makubaliano na Marekani.

"Bila shaka hawasemi hivyo na hawapaswi kusema hivyo. Hakuna mpatanishi mzuri angesema hivyo. Lakini Iran inatazamia sana kufanya makubaliano," Bw. Trump alisema katika mahojiano na mtandao wa Marekani wa CBS.

Katika hotuba ya leo, Bw. Khamenei amesema: "Matamshi ya wale wanaozingatia kusema "Kifo kwa Marekani" kuwa sababu ya uadui wa Marekani dhidi ya taifa la Iran ni kubatilisha historia. Kauli mbiu hii si suala ambalo Marekani italipinga taifa letu kwa njia hii. Suala kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ni mzozo wa kimaslahi .

Pia unaweza kusoma
..

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Saa chache kabla ya hotuba ya kiongozi huyo wa Iran, mahojiano na Rais wa Marekani Donald Trump yalipeperushwa, akisema Tehran inatazamia kufikia makubaliano na Marekani.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Aliongeza: "Asili ya kiburi cha Marekani ni kwamba haikubali chochote isipokuwa kujisalimisha; hivi ndivyo marais wote wa Marekani walitaka, lakini hawakusema, lakini rais wa sasa alisema na kwa kweli alifichua utendaji wa ndani wa Marekani."

Wakati wa hotuba ya Bw. Khamenei leo, waliohudhuria waliimba kauli mbiu za "Kifo kwa Marekani" na "Kifo kwa Uingereza."

Bwana Khamenei hakurejelea moja kwa moja mazungumzo kati ya Iran na Marekani katika matamshi yake, lakini alisema kwa maoni yake, "tofauti kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu si tofauti ya kimbinu , bali ni tofauti ya kiasili."

Katika siku za hivi karibuni nchi mbili za Oman na Qatar ambazo zilikuwa wapatanishi baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na serikali za Magharibi zimezitaka Iran na Marekani kurejea katika meza ya mazungumzo.

Katika mahojiano na mtandao wa Al Jazeera wa Qatar, ambayo yalitangazwa kwa ukamilifu siku ya Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi alisema kuwa Tehran haina haraka ya mazungumzo na kusisitiza kwamba ziara ya hivi karibuni ya naibu wake, Majid Takht-Ravanchi, mjini Muscat "haina uhusiano wowote na Marekani na hakuna mabadilishano ya ujumbe yamefanyika kuhusiana na suala hilo."

Kabla ya vita vya siku 12, Iran na Marekani zilifanya duru tano za mazungumzo yaliyopatanishwa na Qatar, lakini siku mbili kabla ya duru ya sita ya mazungumzo, Israel na kisha Marekani ziliishambulia Iran.

Majid Takht-Ravanchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, ambaye alikuwepo kwenye mazungumzo hayo, alisema wiki iliyopita kwamba Bw. Trump alimwambia Ali Khamenei katika barua kwamba ndani ya siku 60 za mazungumzo, tutafikia makubaliano au kutakuwa na vita.

Marekani inasema Iran haipaswi kuendelea kurutubisha madini ya uranium, lakini Iran imetangaza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani na kwamba haitaacha kurutubisha madini ya uranium.

Katika mahojiano yaliyotangazwa jana usiku kwenye mtandao wa Marekani wa CBS, Bw.Trump alisema kuwa ana uhakika kuwa Iran haina tena uwezo wa nyuklia baada ya mashambulizi ya anga ya Marekani.

Kuhusiana na ukubwa wa uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Uharibifu ni mkubwa, majengo yaliharibiwa, vifaa na mashine zetu ziliharibiwa, lakini teknolojia haijaharibiwa. Teknolojia haiwezi kuharibiwa kwa mabomu."

Rais wa Iran Masoud Pezzekian, katika ziara yake ya hivi majuzi katika Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, alisema kuwa serikali inaunga mkono "kwa nguvu zake zote uendelezaji na uimarishaji wa uwezo wa nyuklia" na kusisitiza kwamba inawezekana kujenga upya vituo vilivyoshambuliwa.