Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 10.05.2024
Chelsea watafanya tathmini ya mwisho wa msimu kufuatia mchezo wao wa mwisho wa ligi msimu huu dhidi ya Bournemouth, ambapo wataamua mustakabali wa meneja Mauricio Pochettino. (Telegraph)
Arsenal inamtazama mlinda lango wa zamani na mchezaji wa kimataifa wa Poland Wojciech Szczesny, 34, pamoja na mlinda lango wa Brighton Muingereza Jason Steele na kipa wa Ajax Mjerumani Diant Ramaj wakitafuta atakayeziba nafasi ya Mwingereza Aaron Ramsdale, 25, ambaye anatarajiwa kuondoka The Gunners. (Standard)
Arsenal pia wanafikiria kumnunua kipa wa Everton na England Jordan Pickford, 30 katika dirisha la usajili la majira ya joto. (Teamtalk).
The Gunners wanalenga kusajili beki, kiungo na mshambuliaji huku wakipania kuimarisha kikosi cha meneja Mikel Arteta. (Standard)
Graham Potter amekataa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa Ajax , baada ya kuibuka mshindani mkuu wa kuchukua nafasi ya kuongoza miamba hao wa Uholanzi. (Usajili unahitajika)
Mshambulizi wa Manchester United Nikita Parris alikataa uhamisho wa kuhamia North Carolina Courage nchini Marekani mwezi Aprili huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 akitaka kucheza fainali ya Kombe la FA kwa upande Wanawake Jumamosi dhidi ya Tottenham. (Usajili unahitajika)
Bayern Munich wamekuwa wakijadili uwezekano wa kumteua kocha wa zamani wa Ujerumani Hansi Flick kama meneja wao mpya, huku kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 akiwa tayari kurejea katika wadhifa wake wa zamani kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel anayeondoka. (Sky Sports Ujerumani)
Beki wa Manchester City na Brazil Yan Couto, 21, ambaye yuko kwa mkopo Girona, anazivutia Bayern Leverkusen , Juventus na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya England kwa uhamisho wa majira ya joto. (Sports)
Eintracht Frankfurt wanataka euro 50-60m kwa mlinzi wa Ecuador mwenye umri wa miaka 22 Willian Pacho, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool. (Sky Sports Ujerumani)
Kampuni ya Marekani ya MSP Sports Capital, ambayo ilionyesha nia ya kuinunua Tottenham mwaka jana, inasemekana kuwa inasubiriwa kwa hamu na Toffees ikiwa dili la 777 Group litasambaratika. (Football London)
Newcastle United wamefanya mazungumzo ya juu na Dougie Freedman wa Crystal Palace na Johannes Sports, ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa kimataifa katika 777 Group kuhusu nafasi ya ukurugenzi wa michezo. (Sky Sports)
Manchester City wamekubali mkataba wa kumsaini kiungo wa kati wa Marekani Cavan Sullivan, 14, ambaye amejiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya Philadelphia Union, baada ya kufikisha umri wa miaka 18. (ESPN).
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah