Kijiji kilichopotea ambapo wanawake wanahatarisha maisha yao milimani na wanaume wanakaa nyumbani wakilima

Sakina (kushoto), Thai Bibi (katikati) na Annar (kulia).

Chanzo cha picha, TASEER BEYG

Maelezo ya picha, Wafugaji watatu wa mwisho wa Wakhi: Sakina (kushoto), Thai Bibi (katikati) na Annar (kulia).

Kwa karne kadhaa, wachungaji wa Wakhi nchini Pakistani walisafiri hadi maeneo ya mbali milimani kuchunga mifugo yao. Mapato yaliyopatikana yalikuwa muhimu kubadilisha jamii yao.

Yalisaidia kulipia huduma za afya, elimu, na barabara ya kwanza iliyojengwa nje ya bonde lao na kuunganishwa na dunia nzima.

Lakini mtindo huu wa maisha inatoweka.

Makala maalum ya BBC 100 Women yaliungana nao katika moja ya safari zao za mwisho kwenye maeneo ya wafugaji.

Safari yetu ya kwenda kwenye mbuga za Pamir ni ya dhiki. Njia za milima miinuko ya juu kwenye njia zilizopinda: ukikosea hatua moja tu, mambo yako kwisha!

Wanawake wanapiga miluzi na kupiga kelele kuwaelekeza kondoo, mbuzi wasitoke kwenye njia nyembamba na kuanguka chini ya mlima.

"Zamani kulikuwa na ng'ombe wengi zaidi kuliko sasa," anasema Bano, mwenye umri wa miaka 70. "Wanyama walianguka kutoka hapa hadi kule na kutoweka. Wengine walirudi na wengine hawakurudi."