Viwanja vya ndege bora zaidi Dunia, Afrika iko wapi?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Singapore imerejesha hadhi yake ya kuwa na uwanja wa ndege bora zaidi duniani baada ya kupoteza hadhi hiyo iliyokuwa imeshikiliwa kwa muda mrefu kwa Qatar kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kipindi cha kilele cha utekelezaji wa masharti ya kutosafiri.

Uwanja wa ndege wa Doha, Hamad International Airport ilichukua nafasi ya pili huku uwanja wa ndege wa Haneda wa Tokyo ukichukua nafasi ya tatu.

Paris Charles de Gaulle ulichukuliwa kuwa uliofanya vizuri zaidi Ulaya baada ya kupanda juu kwa nafasi moja hadi nambari 5 huku uwanja wa kimataifa wa Seattle Tacoma ukichukua nafasi bora zaidi eneo la Amerika Kaskazini.

Orodha ya Uwanja wa Ndege Bora mwaka 2023:

  • Singapore Changi
  • Doha Hamad
  • Tokyo Haneda
  • Seoul Incheon
  • Paris Charles De Galle
  • Istanbul
  • Munich
  • Zurich
  • Tokyo Narita
  • Madrid Barajas

Orodha ya Uwanja wa Ndege Bora Afrika kwa 2023:

.

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Cape Town
  • Durban King Shaka
  • Johannesburg
  • Casablanca
  • Mauritius
  • Marrakech
  • Addis Ababa
  • Kigali
  • Nairobi
  • Bloemfontein
.

Chanzo cha picha, ARR