Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wafahamu majaji katika kesi ya mauaji ya kimbari ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Majaji 15 katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) watachunguza kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu mashtaka ya kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina wakati wa vita huko Gaza.
Kwa mujibu wa sheria za ICJ, nchi ambayo ni mwanachama wake na haina jaji wa utaifa wake kwenye inaweza kumteua jaji maalum. Hii ni kwa Israel na Afrika Kusini.
Israel imemchagua Aharon Barak, jaji mkuu wa zamani wa Mahakama Kuu ya nchi hiyo, ambaye ameonyesha kuunga mkono vita vya Israel dhidi ya Gaza.
Wakili wa Uingereza Malcolm Shaw - ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wataalamu wa juu duniani katika sheria za kimataifa - pia ataitetea Israel katika ICJ.
Chaguo la Afrika Kusini ni Jaji Dikgang Moseneke. Yeye ni Naibu Jaji Mkuu wa zamani wa Mahakama Kuu na amefanya kazi ya kisheria na kitaaluma nchini Afrika Kusini na nje ya nchi.
Profesa wa sheria za kimataifa, John Dugard, pia ataiwakilisha Afrika Kusini katika kesi ya ICJ. Yeye ni mwandishi wa zamani wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa na hapo awali aliwahi kuwa jaji katika ICJ.
Jaji Mkuu Joan Donoghue
Joan Donoghue ni mwanasheria wa Marekani na msomi wa sheria. Yeye ni rais wa sasa wa ICJ.
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo mwaka 2010 na kuchaguliwa tena mwaka 2014. Mnamo 2021, Jaji Mkuu Donoghue alichaguliwa na majaji wenzake wa ICJ kuhudumu kama rais. Ni mwanamke wa tatu kuchaguliwa katika mahakama ya ICJ na mwanamke wa kwanza wa Marekani kuchaguliwa kuwa rais. Jaji Donoghue aliwahi kuwa mshauri wa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na waziri wa zamani wa mambo ya nje Hillary Clinton na katika nyanja zote za sheria za kimataifa.
Makamu wa Rais Kirill Gevorgyan
Alichaguliwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki mnamo 2015, na amekuwa Makamu wa Rais wa Mahakama tangu 2021
Jaji Gevorgyan alichaguliwa kama mwanachama wa ICJ mnamo Februari 2015, na akawa makamu wa rais mnamo Februari 2021. Amekuwa afisa wa sheria katika wizara ya mambo ya nje ya Urusi tangu mwaka 2009. Ameiwakilisha Urusi mbele ya ICJ katika kesi kadhaa - hasa kesi iliyoletwa na Georgia juu ya ukiukaji wa Urusi wa Mkataba wa kuondoa Aina zote za Ubaguzi wa rangi mnamo 2008.
Jaji Abdulqawi Ahmed Yusuf
Alikuwa rais wa zamani wa mahakama hiyo kuanzia 2018 hadi 2021
Jaji Youssef ni raia wa Somalia na ana shahada ya uzamivu katika sayansi ya siasa na sheria za kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Geneva. Alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya ICJ mwaka 2009 na alichaguliwa tena kati ya mwaka 2018 na 2021. Alihudumu kama jaji maalum katika kesi iliyowasilishwa na ICJ na Djibouti dhidi ya Ufaransa kuhusu msaada wa pamoja katika kesi za jinai.
Jaji Julia Sebutinde
Alichaguliwa kuwa mjumbe wa Mahakama ya Haki kwa mara ya kwanza mwaka 2012, na alichaguliwa tena mwaka 2021
Alizaliwa Uganda mwaka 1954, Jaji Sibutende alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama mwanachama wa ICJ mwaka 2012 na kuchaguliwa tena mwaka 2021. Ana shahada ya udaktari wa heshima katika sheria kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh nchini Uingereza. Amewahi kushikilia nafasi kadhaa za mahakama na kisheria, akihudumu kama jaji katika Mahakama Maalum ya Sierra Leone kutoka 2005 hadi 2011.
Ameshughulikia kesi kadhaa za uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kesi dhidi ya Rais wa Liberia Charles Taylor, ambaye alituhumiwa kwa kufanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa urais wake.
Jaji Patrick Lipton Robinson
Amekuwa mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki tangu 2015
Robinson alizaliwa nchini Jamaica mwaka 1944 na amekuwa mwanachama wa ICJ tangu mwaka 2015. Alifanya kazi kama mshauri wa kisheria katika wizara ya mambo ya nje ya Jamaica na kwa miaka 26 alikuwa mwakilishi wa nchi hiyo katika Kamati ya Sita ya Sheria ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Alihusika katika uongozi wa juu katika kuandaa vifungu kadhaa vya sheria, ikiwa ni pamoja na ufafanuzi wa uchokozi na rasimu ya sheria ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Jaji Peter Tomka
Peter Tomka aliteuliwa kuwa Balozi wa Slovakia katika Umoja wa Mataifa mwaka 1994.
Jaji Ronnie Abraham
Alihudumu kama Rais wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuanzia 2015 hadi 2018
Jaji Mohamed Bennouna
Bennouna aliwahi kuwa mwakilishi wa kudumu wa Morocco katika Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1998 hadi 2001.
Jaji Xue Hanqin
Mwaka 2018, Xue aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
Jaji Dalveer Bhandari
Bhandari aliongoza Kamati ya Huduma za Kisheria ya Mahakama Kuu ya Delhi
Jaji Yūji Iwasawa
Alikuwa mwanachama wa mahakama mwaka 2018, na alichaguliwa tena mwaka 2021
Jaji Nawaf Salam
Nawaf Salam alihudumu kama balozi wa Lebanon na mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 2007 hadi 2017.
Jaji Hilary Charlesworth
Amekuwa mjumbe wa mahakama tangu 2021
Jaji Georg Nolte
Mwaka 2020, Georg Nolte alichaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Jaji Leonardo Nemer Caldeira Brant
Alichaguliwa kuwa jaji mwaka 2022
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi