Enzi ya magari yanayopaa inaonekana kukaribia - lakini changamoto kubwa bado hazijatatuliwa

.

Chanzo cha picha, Klein Vision

Enzi mpya ya magari yanayopaa inakaribia kuanza. Mnamo tarehe 12 Juni 2023, Utawala wa Shirikisho la Usafiri wa Anga (FAA) ulitoa Cheti Maalum cha usafiri wa Anga kwa modeli ya gari linalopaa iliyotengenezwa na Aeronautics, na kuruhusu gari hilo kwenda safari za maeneo machache kwa maonyesho, utafiti na maendeleo zaidi.

‘Advanced Air Mobility’ (AAM) ni neno linalotumika kwa ndege za abiria au zinazobeba mizigo ambazo kwa kiasi kikubwa zinajiendesha.

Mara nyingi hujulikana kama teksi za kwenye anga au ndege za wima za kupaa na kutua, magari haya kwa nadharia hutoa usafiri wa haraka na salama kutoka eneo moja hadi jingine.

Hakuna miundombinu halisi au msongamano wa magari wa ardhini utakaopunguza kasi hiyo.

Ingawa gari la kupaa angani bado ni kama ndoto, kutambuliwa kwa Alef na Shirika la FAA kunaashiria mabadiliko katika siku zijazo za usafiri wa angani.

Lakini bado kunaweza kuwa na changamoto nyingi za kusuluhisha kabla magari ya kupaa kuwa uhalisia katika miji kote ulimwenguni – sauti ya ghafla na ya mwendo wa kasi kwa ndege zisizo na rubani na magari yanayopaa wakati wa kupaa au kutua.

Waanzilishi wa gari la kupaa modeli ya Alef walianza kufanyia kazi dhana hii mwaka wa 2015 na waliunda mfano wao wa kwanza wa gari la kupaa la ukubwa kamili mwaka wa 2019: Model A.

Gari hili la abiria litatoshea watu wawili na kusafiri umbali wa maili 200 (322km) na safari ya ndege ya maili 110 (177km).

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Gari lenye kuvutia na dogo, limeundwa ili lifanane na gari la kawaida, halitahitaji njia ya kupaa au kutua, na linapaswa kutoshea kwenye nafasi ya kawaida ya kuegesha magari.

Mbinu ya kubuni gari la kupaa Model A inahusu utendakazi kama umbo: kampuni inadai kwamba teknolojia ya umiliki wa gari inaiwezesha kupaa wima na kubadilika kuwa ndege yenye seti mbili za mbawa, moja juu na kwa kawaida mbele kidogo ya nyingine, ikiwa na milango ambayo itabadilika kuwa mbawa, yote hayo ikiwa ni katika juhudi za kubadilisha usafiri wa kila siku.

Kufikia sasa, hata hivyo, ni wawekezaji wachache tu ambao wamefanikiwa kufika hatua ya gari la Model A ya kupaa katika maonesho ya mwaka 2019, kulingana na tovuti ya kampuni hiyo.

Lakini changamoto nyingi za kiteknolojia bado zimesalia.

"Baadhi ya vifaa ambavyo tunahitaji ni kwamba havipo duniani kufikia leo," anaelezea Jim Dukhovny, mtendaji mkuu wa Aeronautics ya Alef.

"Kwa mfano, ili kuepusha dhiki tofauti tunahitaji mifumo maalum ya injini ya propela."

Ukubwa, uzito na bei vitaamua ni muda gani magari haya yatapatikana kwa umma, na kama yatakuwa salama kuyaendesha.

.

Chanzo cha picha, Alef

Maelezo ya picha, Gari linalopaa Modeli A la Alef bado halijatolewa kwenye maonyesho ya umma

Kampuni hiyo iliyoko California inatarajia kuanza utengenezaji mnamo 2025 au mapema 2026, ingawa magari hayo tayari yanapatikana kwa kuagizwa mapema (bei kwa sasa ni $300,000 (£246,000), lakini Alef anatarajia kuongeza gharama hadi $35,000 au £28,700 kila moja.)

Modeli A inachukuliwa kuwa yenye mwanga mwingi, "gari la mwendo kasi wa chini", uainishaji wa kisheria uliowekwa awali kwa kigari cha gofu na magari madogo ya umeme - inazingatia miongozo mikali kama ilivyowekwa na Utawala wa Kitaifa wa Usalama Barabarani.

"Ni la awali," anasema Dukhovny.

"Magari yalipoanza kuchukua nafasi ya farasi, maswali mengi kama hayo yaliibuka: kuhusu usalama, kile kitakachotokea kwa miji…wengi walitaka kurejea kwa farasi. Ikiwa itafanywa kwa njia sahihi, gari linalopaa linapaswa kuwa salama zaidi.

"Lakini Model A mwisho wa siku, inakusudiwa kuwa gari, na tena salama kwa anga – na kwa kweli kunaweza kumaanisha kuwa sio salama kwa barabara.

"Sehemu ngumu zaidi ni kwamba: hatujui nini kinatokea wakati gari linahamishwa kutoka ardhini hadi angani," anaelezea Dukhovny.

Ukweli ni kwamba, kungekuwa na uhamisho wa haraka wa mamlaka kutoka ardhini hadi kwenye anga, lakini vikwazo vya kisheria na usalama ni vigumu.

Shughuli za usafiri wa anga za mijini zitakuwa hasa na jukumu la mtoa huduma wa urambazaji wa anga nchini (ANSP), kama vile FAA nchini Marekani.

ANSP ina mamlaka kamili juu ya shughuli za anga ya taifa fulani, na ndiyo mamlaka inayoidhinisha aina mpya za ndege baada ya ukaguzi mkali wa usalama.

Jukumu la miji katika kuhakikisha usalama litakuwa ni kutekeleza kanuni zilizowekwa na watoa huduma hawa.

Kulingana na ripoti ya mwongozo iliyochapishwa na FAA, shughuli za magari yanayopaa kwanza zitatumia mfumo na sheria zilizopo za udhibiti (kama vile sheria za ndege za kuona, sheria za urukaji wa chombo) kama jukwaa la utendakazi bora wa ndege na viwango vya juu vya uhuru.

Ripoti hiyo inaibua wasiwasi fulani bila kuyashughulikia kikamilifu: masuala ya kelele, uchafuzi wa mazingira, usalama, uendelevu, gharama na kadhalika.

Pia kuna maswali kama vile, nani ataendesha haya magari ya kupaa?

Je, abiria watahitaji leseni?

"Viwanja vya ndege" na magari yanayopaa katika miinuko ya chini vitaathiri vipi maisha ya ujirani?

Ni eneo gani la mamlaka litawajibika kwa ajali katikati ya anga?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Magari yanayopaa hayatakuwa suluhisho ya moja kwa moja kukabiliana na msongamano wa magari katika miji kama vile Los Angeles

Kasi ambayo magari hayo yatakuwa yakisafiri inaweza kusababisha migongano, iwe kati ya magari au na majengo; njia sahihi, inayoongozwa kisayansi na upangaji wa njia ni muhimu.

FAA inalenga "teksi za kwenye anga" zinazofanya kazi ndani ya ushoroba mahususi kati ya viwanja vya ndege katikati mwa jiji.

Lakini hadi sasa, hakuna masharti kwa ajili ya njia ya gari linalopaa.

Na kisha kuna suala la kelele.

Kubuni magari ya kupaa ambayo yatakuwa hayatoi kelele kabisa ni vigumu, hasa wakati shughuli kubwa za kibiashara zinaweza kuwa na mamia ya safari na kutua kila saa.

Propela za umeme na vifaa vingine vya muundo wa mwendo wa gari la kupaa vinaweza kupunguza kelele, na wapangaji miji hakika wanapaswa kuzingatia kiwango cha desibeli cha sehemu za chini au mahali pa kutua, lakini kanuni kali za serikali zinaweza kuhitajika ili kudhibiti viwango vya kelele.

Miongozo ya miundombinu ya anga inaweza kuchukuliwa kutoka kwa kanuni zilizopo: vipimo vinavyotumika kwa ndege na helikopta za kitamaduni.

Nasa imeungana na FAA, watafiti wa vyuo vikuu na viongozi wengine wa tasnia ili kuunda zana za programu ambazo zinaonyesha mfano na kutabiri kelele, katika juhudi za kusaidia watengenezaji kuunda magari tulivu.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gari linalopaa litahitaji kusuluhisha masuala kadhaa - hasa kelele - ikiwa ni lianze kutumika

Arup, kampuni ya Uingereza inayotoa huduma za kubuni, uhandisi na uendelevu katika mazingira yote yaliyojengwa, hivi majuzi ilifanya mjadala wa pande zote ili kuchunguza uwezekano - na changamoto - za soko la usafiri wa anga.

"Ambapo miji ina nafasi zaidi ya kudai udhibiti kupitia leseni za biashara," anasema Byron Thurber, mkuu mshirika wa Arup huko San Francisco.

"Kama ilivyo kwa mashirika ya ndege na viwanja vya ndege, manispaa zina mamlaka ya kudhibiti utendakazi ulioidhinishwa wa huduma za usafiri wa anga za kibiashara; hii inaweza kujumuisha sheria kuhusu saa za marufuku ya kutotoka nje, msongamano wa juu wa vituo katika vitongoji na ada fulani."

Kwa maneno mengine, miji ina uwezo wa kuweka vituo vya ulinzi vinavyosaidia kujua ni lini na wapi huduma ya teksi ya anga inaweza kufanya kazi.

Labda haishangazi kwamba Los Angeles, pamoja na msongamano wake wa kawaida, ni jiji linalorejelewa sana kama mpokeaji wa mapema wa huduma hii. Lakini ni kiasi gani magari ya kupaa yanaweza kusaidia kufungua jiji lenye msongamano kama Los Angeles?

"Jambo moja la kukumbuka ni kwamba uhamaji hadi kwenye usafiri wa anga mijini hautasuluhisha msongamano wa magari," anasema Thurber.

"Ukweli ni kwamba, hatuna uwezekano wa kuona wingi wa magari kwenye anga kama ilivyo wingi wa magari ya ardhini - na ikiwa hilo litatokea, basi kungekuwa na msongamano kwenye anga."