Jinsi Putin anavyoiweka Afrika Kusini kwenye njia panda ya kidiplomasia

Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Imekuwa miezi michache ya msukosuko wa kidiplomasia kwa Afrika Kusini.

Nchi ambayo ingependa kuonekana kama balozi mwenye busara na katika mazungumzo ya amani ya Ukraine, na mpatanishi asiyeegemea upande wowote imenaswa katika msururu wa mizozo ya hadhara ya kimataifa ambayo iliiacha serikali yake ikionekana kuchanganyikiwa na kutokuwa na maamuzi, na sarafu yake kudorora kwa hali mpya.

Suala linaloleta kizungumkuti ni uhusiano wakaribu wa Afrika Kusini na Urusi - na mtazamo unaokua wa Magharibi kwamba nchi hiyo imeamua kuunga mkono Moscow katika vita vyake dhidi ya Ukraine, na pengine hata kuipelekea silaha.

Lakini je, mtazamo huo ni wa haki? Na yote yanaweza kumaanisha nini kwa sifa ya Afrika Kusini na uchumi wake unaozidi kudorora?

"Ni ndoto mbaya," alikiri afisa mmoja mkuu wa Afrika Kusini. Walikuwa wakizungumza faraghani mjini Cape Town wiki hii, pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la Brics, linalojumuisha Urusi, China, Brazil, India na Afrika Kusini.

Wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wameelezea faraghani jinsi walivyokwazwa na msimamo wa Afrika Kusini dhidi ya Urusi na jaribio lake la "kutopendelea" upande wowote iliyojitangazia yenyewe kuhusiana na uvamizi wa Kremlin nchini Ukraine.

"Moyo wa serikali uko kwa Warusi. Hakuna shaka juu ya hili. Wanaamini kwamba ulimwengu unatoka mikononi mwa nchi za Magharibi - kwamba Warusi wana nguvu zaidi na watashinda, na kwamba wanawekeza katika mustakabali wa kimkakati, mpangilio mpya wa ulimwengu. ," alisema Irina Filatova, msomi wa Kirusi anayeishi Cape Town.

Rais wa Afrika Kusini (kulia) amekataa kulaani uvamizi wa kiongozi wa Urusi nchini Ukraine

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais wa Afrika Kusini (kulia) amekataa kulaani uvamizi wa kiongozi wa Urusi nchini Ukraine

Lakini wengine hapa wanasema kuwa nchi za Magharibi zimekosea na zinaielewa vibaya Afrika Kusini na kuhangaika juu ya kile ambacho ni sawa na dhoruba katika kikombe cha chai cha kidiplomasia.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Hakuna mtu makini ndani ya serikali [ya Afrika Kusini] anayetaka kuachana Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulya (EU). Kila mtu anajua kuwa hawa ni washirika muhimu sana wa kibiashara. Ni mkanganyiko tu katika suala la muda na mtazamo, si katika suala la msingi," alihoji mchambuzi wa masuala ya kisiasa Philani Mthembu.

Kwa hiyo mambo yaliharibikia wapi?

Jibu la awali la Afrika Kusini kwa uvamizi wa Urusi lilikuwa kuitaka Moscow iondoe majeshi yake "mara moja".

Muda mfupi baadaye ilibadilika, kukataa kulaani Kremlin katika Umoja wa Mataifa, na kupitisha sera ya kutoegemea upande wowote katika mzozo huo.

Lakini msimamo huo wa kutoegemea upande wowote tangu wakati huo umehujumiwa na msururu wa vitendo na matamshi ambayo yamewakashifu washirika wa Ukraine.

Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa jeshi la wanamaji la Urusi kwa mazoezi katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa uvamizi huo.

Ilikaribisha kwa uchangamfu msururu wa maafisa wakuu wa Kremlin, na baadaye ikatuma mkuu wake wa jeshi kwenda Moscow kwenye ziara iliyoashiria "utayari wa kupigana".

Na maafisa waandamizi hapa wamerudia mara kwa mara hoja za Kremlin zinazoangazia jinsi Marekani inavyoendesha vita vya visvyo vya "moja kwa moja" na jinsi Ukraine iliyo na silaha za Magharibi inavyotishia Urusi.

Uchunguzi unaendelea kuhusu mazingira iliyopelekea kutia nanga kwa meli ya Urusi The Lady R nchini Afrika Kusini Desemba mwaka jana
Maelezo ya picha, Uchunguzi unaendelea kuhusu mazingira iliyopelekea kutia nanga kwa meli ya Urusi The Lady R nchini Afrika Kusini Desemba mwaka jana

Mkanganyiko wa kidiplomasia wa nchi za Magharibi hatimaye ulizuka hadharani katika mkutano wa hivi majuzi na balozi wa Marekani Reuben Brigety.

Aliishutumu Afrika Kusini kwa "kuipa Urusi silaha" kwa kusafirisha "silaha na risasi" kwenye meli ya Urusi ambayo ilitia nanga katika bandari yenye ulinzi mkali karibu na Cape Town Desemba mwaka jana.

"Tuna uhakika kwamba silaha zilipakiwa kwenye chombo hicho. Naweza kuapa kwa maisha yangu juu ya madai hayo," alisema Balozi Brigety, ambaye aliendelea kuongeza uwezekano kwamba Marekani inaweza kujibu hatua hiyo kwa vikwazo vya biashara.

Matamshi ya balozi huyo yalichochea hasira kutoka kila upande nchini Afrika Kusini, huku baadhi ya watu wakitafsiri msimamo wa kikoloni katika matamshi hayo.

"Alikuwa nje ya utaratibu kabisa. Je, tunapaswa kuzingatia chochote Wamarekani wanachosema? Kwa kweli sikubaliani na hilo. Huu ni uhuni wa kisiasa," alisema Mavuso Msimang, mkongwe maarufu wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Waafrika Kusini wengi wanakumbuka uungwaji mkono wa Moscow kwenye vuguvugu la ukombozi katika bara zima, na kupendelea harakati - zinazoendeshwa na kundi la Brics.

Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini Thandi Modise alielezea jinsi serikali ilivyofadhaishwa na kauli hiyo. Aliongea neno moja la lugha ya kiafrika Kusini, ambalo kwa upole linamaanisha "hakuna chochote", kuelezea ni silaha ngapi ambazo Afrika Kusini ilikuwa imesafirisha kwenda Urusi.

Pendekezo la amani la Afrika

Kumekuwa na minong'ono ya hapanapale kwamba balozi wa Marekani huenda alivuka mpaka, na baadaye alitaka "kufafanua kauli yake", lakini alishindwa kuomba msamaha au kufuta madai hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini (kulia) alimkaribisha mwenzake wa Urusi (R) kwa mkutano wa Brics wiki hii

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini (kulia) alimkaribisha mwenzake wa Urusi (R) kwa mkutano wa Brics wiki hii

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa - ambaye amezongwa migogoro ya ndani - amepuuza madai hayo kwa kutoa wito wa uchunguzi huru kuhusu kile kilichokuwa, au kisichokuwa, kilichosafirishwa, au kutosafirishwa, kupitia kambi ya jeshi la wanamaji la Afrika Kusini huko Simon's Town.

Tangu wakati huo, katika hatua ambayo inaweza kusaidia kurekebisha hali ya kutoegemea upande wowote kwa serikali yake, ametangaza mipango ya wajumbe sita wa amani wa Kiafrika wanaohudumu mjini Moscow na Kyiv.

"Hii haitakuwa jambo rahisi ... lakini lazima ifanyike," Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor aliambia kituo cha redio cha ndani.