'Rais Erdogan anafuata nyayo za Saddam Hussein kwa kuitishia Israel'

Chanzo cha picha, Reuters
Kauli za Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumapili, ambapo alisema kuwa "Uturuki inaweza kuingia Israel, kama ilivyoingia Libya hapo awali na Karabakh," zilizua hisia kubwa nchini Israel, na kuzusha vita vya majibizano katika mtandao wa x zaani twitter kati ya maafisa wa nchi hizo mbili.
Baada ya rais wa Uturuki kutishia kuingia Israel - bila kutaja aina ya uingiliaji anaozungumzia - Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz alijibu kauli za Erdogan kupitia "X", ambapo alisema, "Erdogan anafuata nyayo za Saddam Hussein na kutishia kushambulia Israel
''Acha tu akumbuke kilichotokea huko na jinsi kiliisha," Katz aliongeza kwenye tweet yake.
Katz aliambatanisha picha iliyorekebishwa ya Erdogan na Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein kwenye tweet hiyo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Lazima alazimishwe kutoiunga mkono Hamas

Chanzo cha picha, EPA
Erdogan alitoa matamshi yake katika mkutano wa chama tawala cha Haki na Maendeleo katika mji aliozaliwa wa Rize ambapo alisema: "Lazima tuwe na nguvu nyingi ili Israel isiweze kufanya mambo haya ya kipuuzi kwa Palestina."
"Hakuna sababu kwa nini hatuwezi kufanya hivi. Lazima tuwe na nguvu ili kuweza kuchukua hatua hizi," Erdogan aliongeza katika hotuba yake kwa njia ya televisheni.
Majibu ya kauli hizo hayakuishia kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, kiongozi wa upinzani nchini Israel, Yair Lapid, alisema kwenye chapisho lake la "X", "Israel haitakubali vitisho kutoka kwa dikteta, na ulimwengu, hasa wanachama wa NATO, wanapaswa kulaani vikali vitisho vyake vya kuitishia Israel, na kumlazimisha kukomesha uungaji mkono kwa Hamas.

Chanzo cha picha, Reuters
Lapid aliongeza: "Rais Erdogan anapiga kelele na kufoka tena, ni hatari kwa Mashariki ya Kati."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
'Hatma ya Netanyahu haitakuwa tofauti na mwisho wa Hitler'
Majibu hayo ya Israel yalizua majibu mengine ya Uturuki, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ikitoa taarifa ikimlinganisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na "kiongozi wa Nazi Adolf Hitler."
Shirika la Anadolu la Uturuki lilinukuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ikisema: "Hata kama mwisho wa mauaji ya halaiki ya Hitler ungekuwaje, ndivyo mwisho wa mauaji ya Netanyahu utakavyokuwa," na kusisitiza kwamba "ubinadamu utasimama pamoja na Wapalestina."
"Hutaweza kuwaangamiza," Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki iliongeza, ikirejelea Wapalestina, ikieleza kwamba "kama vile Wanazi waliofanya uhalifu mkubwa walivyowajibishwa, ndivyo wale wanaotaka kuwaangamiza Wapalestina," kulingana na wizara

Chanzo cha picha, Reuters
Gazeti la Jerusalem Post lilisema kuwa "Vitisho vya Rais Erdogan wa Uturuki kuingia Israel" vinakuja huku kukiwa na ongezeko kubwa la vita vilivyodumu kwa miezi tisa kati ya jeshi la Israel na Hezbollah.
Mzozo huo umeenea zaidi ya Israel na Uturuki, huku Mbunge wa Uholanzi Geert Wilders - mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia anayejulikana kwa uadui wake kwa Waislamu na wahamiaji - akitaka Uturuki "ifurushwe" kutoka NATO kutokana na matamshi ya Erdogan.
Aliandika kwenye jukwaa la "X": "Erdogan fashisti wa Kiislamu anatishia kuivamia Israeli, mtu huyu ni kichaa kabisa, Uturuki inapaswa kufukuzwa kutoka NATO
Erdogan ni sauti ya dhamiri ya mwanadamu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amemtaja Rais Recep Tayyip Erdogan kuwa "sauti ya dhamiri ya binadamu" na kwamba duru za Israel na Wazayuni zimo katika hali ya hofu.
Fidan alisema kupitia jukwaa la "X": "Rais wetu (Erdogan) amekuwa sauti ya dhamiri ya mwanadamu, na wale wanaojaribu kunyamazisha sauti ya ukweli, inayoongozwa na duru za Kizayuni na Israeli, wanaishi katika hali ya kushangaza. wasiwasi."
Fidan alisema historia inaonyesha kuwa "matokeo yatakuwa sawa kwa wahusika na wafuasi wote wa mauaji ya kimbari.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Tofauti ya maono tangu mwanzo wa vita vya Gaza
Tangu nyakati za kwanza za shambulio la Oktoba 7, Uturuki ilimua kutumia sauti ya "kutopendelea upande wowote" na haijanyooshea kidole Israel au Hamas kuhusika na shambulio.
Katika siku za kwanza za vita, mazungumzo ya Uturuki yalikuwa na ukomo wa kulaani upotezaji wa maisha ya raia na kusisitiza mawasiliano ya pande zote zinazohusika kusaidia kumaliza mzozo.
Lakini sauti ya Uturuki ilionekana kuwa kali zaidi baada ya shambulio kwenye Hospitali ya Baptist katika Ukanda wa Gaza katikati ya Oktoba, ambapo karibu watu 500 waliuawa.
Rais wa Uturuki Erdogan alisema wakati huo kwamba "mashambulio ya bomu ya Israel ni jibu lisilo sawa na ni sawa na mauaji," na kuitaka Israeli kusitisha mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza, ambayo alielezea kama mauaji ya kimbari.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












