Fahamu jinsi uokoaji wa ajabu kutoka sakafu ya bahari ulivyofanyika miaka 10 iliyopita

Chanzo cha picha, PA Media
Miaka 50 iliyopita mabaharia wawili wa Uingereza walizama kwa nyambizi karibu futi 1,600, maili 150 karibu na Ireland, kwenye kina kirefu cha maji.
BBC ilichapisha makala ifuatayo mwaka wa 2013. Utafutaji wa nyambizi ya umeamsha hamu.
Wakiwa wamenaswa kwenye mpira wa chuma wenye kipenyo cha futi 6 kwa siku tatu, wanaume hao walikuwa wamesalia na dakika 12 tu za oksijeni walipookolewa.
Awali BBC ilichapisha makala ifuatayo mwaka wa 2013.
Utafutaji wa nyambizi ya Titan umesababisha gumzo duniani kwa mara nyingine tena.
Fuatilia simulizi ya nyambizi Pisces III, ambayo iligonga vichwa vya habari wakati huo.
Lakini siku ya Jumatano tarehe 29 Agosti 1973 aliyekuwa mpiga mbizi wa zamani ya Jeshi la Wanamaji Roger Chapman, wakati huo akiwa na umri wa miaka 28, na mhandisi Roger Mallinson, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35, walizama chini kabisa ya bahari ya Atlantiki katika ajali nyambizi, na kusababisha operesheni ya uokoaji ya kimataifa ya saa 76.
01:15 – Uokoaji wa waliozama kwa nyambizi ukaanza
Nahodha Roger Chapman na nahodha mkuu Roger Mallinson walianza kupiga mbizi kama kawaida kwa nyambizi Pisces III.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Chombo cha chini cha maji cha Canada - kilikuwa kikiweka kebo ya simu inayovuka Atlantiki kwenye bahari ya maili 150 kusini magharibi mwa Cork.
"Ilichukua kama dakika 40 kuzama, si mbali sana hadi futi 1,600 (m 500) na kwa haraka zaidi kuanza tena kupanda juu," anasema Chapman. "Tungefanya zamu za saa nane, tukienda kwenye sakafu ya bahari kwa nusu maili kwa saa, tukiweka kebo na pampu ambazo ziliyeyusha matope na kuhakikisha kuwa zote zimefunikwa. Ilikuwa polepole sana, kazi iliyofanyika kwa giza."
Mallinson anasema kutoonekana vizuri kulifanya kazi hiyo kuwa ya kuchosha.
"Ilikuwa kama kuendesha barabara kwenye ukungu mzito na kujaribu kufuata mstari mweupe - ilibidi uzingatie zaidi imani. Upande mmoja nahodha angekuwa na udhibiti wa nyambizi ndogo kwa mkono wake na manipulator yaani mkono kwenye nyambizi ambao ungeinua, kupinda, kupanua na kusonga upande upande - kisha tungebadilishana," anasema.
"Pia haikuwa kazi rahisi. Ilitubidi tupige magoti."
Kwa Mallinson, zamu hiyo ilifuatia muda wa saa 26 bila kulala. "Upigaji mbizi uliopita ulikuwa umeharibu manipulator, hivyo nilifanya kazi siku nzima nikiitengeneza. Nilijua nyambizi Pisces III ndani nje kwa sababu nilikuwa nimeijenga upya ilipotoka Canada kama mabaki," anasema.
Kwa bahati nzuri, mhandisi pia aliamua kubadilisha tanki ya oksijeni. "Ilikuwa ya kutosha sana kuendesha nyambizi lakini kwa sababu fulani niliamua kuibadilisha kuwa kamili, ambayo haikuwa kazi ya kimwili kwa kuwa ilikuwa nzito sana. Ningeweza kupata shida kwa kubadili nusu ya chupa iliyotumika, lakini kama ilivyotokea, iwapo nisingelifanya hivyo, tungekuwa tumefariki."
Pamoja na kuwekewa kebo, manahodha walilazimika kuvaa vifaa vinavyosaidia kuokoa maisha majini. Kila baada ya dakika 40 waliwasha feni ya lithiamu hidroksidi ili kunyonya kaboni dioksidi waliyokuwa wakipumua na kisha kutumia kiasi kidogo cha oksijeni.
Pia walirekodi maoni yao kwenye video kila walipopiga mbizi ili kuweka rekodi.
09:18 – Ajali
Pisces III ilikuwa kwenye sakafu ya bahari wakati inavutwa.
"Tulikuwa tukingoja kamba ya kuning'inia iunganishwe ndio ituinue na kuturudisha kwenye nyambizi kubwa. Kulikuwa na kamba nyingi zilizojifunga - kama kawaida wakati wa awamu ya mwisho ya operesheni - ghafla tulijeruhiwa nyuma na kuzama kwa kasi. Tulikuwa tukining'inia juu chini, kisha tukainuliwa," anasema Chapman.
Mallinson anasema nyambizi ilikuwa ikitetemeka, na kila kitu kikivunjika huku wakiwa wanazama. "Ilikuwa inatisha sana - injini zinapiga kelele na vipimo vya shinikizo zinazunguka."
09:45 - Mawasiliano
Nyambizi Pisces III ilifanya mawasiliano ya simu, na kutuma ujumbe kwamba wote walikuwa sawa, ari ilikuwa nzuri na walikuwa wanajipanga.
Dalili za mapema zilionyesha kwamba usambazaji wa oksijeni ungeendelea hadi Jumamosi asubuhi.
Nyambizi ndogo ilibeba oksijeni kwa saa 72 endapo ajali itatokea, lakini tayari walikuwa wametumia saa nane kupiga mbizi. Walikuwa wamesalia na saa 66.
10:00-16:30 – Nyambizi inazunguka
Nahodha walitumia saa chache za kwanza "kujipanga, kulingana na Chapman. "Nyambizi ilikuwa karibu juu chini, ilibidi tuipange upya, kurekebisha vifaa na kuhakikisha kuwa hakuna kinachovuja," anasema.
Waliamua ikiwa oksijeni ingedumu, walihitaji kufanya shughuli kidogo sana. "Ukizima, unatumia robo moja ya oksijeni. Hakuna kuzungumza wala kusogea," anasema.
Wanaume hao wawili walilala sehemu ya juu kwenye nyambizi ndogo huku hewa nzito ikiwa chini, kulingana na Mallinson. Kipenyo cha ndani cha nyanja ya wafanyakazi kilikuwa futi 6 tu kwa hivyo wanaume walikuwa na nafasi ndogo sana.
"Hatukuwa na uwezo wa kuongea, tulishikana tu mkono wa kila mmoja wetu na kuuminya ili kuonyesha tuko sawa. Kulikuwa na baridi sana - tulikuwa tumelowa kila sehemu. Sikuwa katika hali nzuri zaidi kwa vile nilikuwa nimepata matatizo ya tumbo kwa siku tatu au nne. Lakini kazi yetu ilikuwa kuendelea kuwa hai," anasema.
Kwenye uso wa bahari juhudi za uokoaji zilikuwa zikiendelea.
Meli ya usaidizi ya Vickers Venturer, ambayo wakati huo ilikuwa katika Bahari ya Kaskazini, ilipata mawasiliano baada ya saa 10:30 na kuamriwa kurudisha nyambizi ndogo Pisces II kwenye bandari iliyo karibu zaidi.
Jeshi la Wanamaji la Kifalme lilitumwa kwenye eneo la tukio na kamba maalum saa 12:09 na ndege ya RAF Nimrod ilipaa juu.
Nyambizi ya chini ya maji ya Marekani, CURV III - iliyoundwa kuchukua mabomu kutoka baharini - ilitumwa kutoka California na meli ya Walinzi wa Pwani ya Canada John Cabot ikaondoka kutoka Swansea.

Chanzo cha picha, OTHER
Alhamisi, Agosti 30
Meli ya kubwa Vickers Voyager ilifika Cork saa 08:00 ili kupakia nyambizi Pisces II na Pisces V, ambazo ziliwasili usiku kucha kwa ndege. Meli ilisafiri kutoka Cork saa 10:30.
Wakati huo huo, Chapman na Mallinson walitazama vitu walivyokuwa navyo vikianza kupungua.
Wawili hao walikuwa na sandwichi moja ya jibini na chutney na kopo moja la limau, lakini hawakutaka kula au kunywa, kulingana na Chapman.
"Tuliruhusu CO2 kujitengeneza tena kidogo ili kuhifadhi oksijeni - tulikuwa na vipima muda vya kufuatilia kila baada ya dakika 40, lakini tungesubiri kwa muda mrefu zaidi. Hii ilitufanya kuwa walegevu na kuhisi kisunzi.
"Pia tulianza kufikiria kuhusu familia zetu. Nilikuwa tu ndio nimeoa kwa hivyo nikaanza kumfikiria mke wangu Jane. Lakini Roger Mallinson alikuwa na watoto wanne na mke, na alianza kuwa na huzuni kidogo kuhusu jinsi walivyokuwa," anasema.
Hata hivyo Mallinson anasema meli moja iliwaachia manahodha ujumbe ambao uliwafanya "kuhisi vizuri sana".
"Tulipata ujumbe kutoka kwa Malkia Elizabeth, ambaye alitutumia salamu za heri kwa ajili ya kuokolewa haraka – ambao ulitupa moyo sana. Inashangaza jinsi unavyoweza kuhisi baridi kali, na kisha kitu kinatokea ambacho kinakufanya uanze kupata joto."
Ijumaa, Agosti 31
"Ijumaa ilikuwa janga kwa mtazamo wa juu juu," anasema Chapman.
Saa 02:00, nyambizi Pisces II iliinuliwa - na kamba maalum ya polipropeni iliyounganishwa na kufungwafungwa – na kamba ya kuinua ikakatika kutoka kwa manipulator kwa sababu ya ueleaji wake, hivyo ilibidi irudishwe kwenye meli kubwa kwa matengenezo.
Kisha nyambizi Pisces V - ilizamishwa tena kwa kamba ya polipropeni iliyoambatanishwa na kuanza tena safari - iliweza kufika chini ya bahari lakini haikuweza kupata nyambizi Pisces III kabla ya kuishiwa na umeme. Ilirudi kwenye uso wa bahari na baadaye ikajaribu tena.
"Ilikuwa karibu saa saba mchana kabla ya nyambizi Pisces V kutupata. Ilitia moyo sana kujua mtu fulani alijua tulipo. Lakini nyambizi Pisces V ilipojaribu kujiunganisha na nyambizi ndogo iliyozama jaribio lilishindikana kwa sababu ya kuelea kwa kamba," anasema Chapman.
Nyambizi Pisces V iliamriwa kukaa na Pisces III, licha ya ukweli kwamba haikuweza kuinua. Pisces II ilishuka tena chini ya bahari, lakini ilibidi kuibuka tena baada ya kupata maji katika nyanja yake.
Kisha CURV III - ambayo ilikuwa imewasili na John Cabot karibu 17:30 - ilikuwa na hitilafu ya umeme hivyo haikuweza kuingia chini ya bahari.
"Kufikia usiku wa manane siku ya Ijumaa tulikuwa na nyambizi Pisces V ikiwa inaishiwa karibu na kila kitu, na nyambizi mbili zilizoharibika," Chapman anasema.
"Kisha Pisces V iliagizwa kurejea kwenye uso wa bahari baada ya usiku wa manane, ambayo ilikuwa pigo kidogo.
Ilikuwa ni kama tumerudi kwenye sifuri. Saa zetu 72 za oksijeni zilikuwa zimeisha, tulikuwa tukiishiwa na lithiamu, hidroksidi ili kupambana na CO2, ilikuwa tukio la kuchanganyisha akili sana na baridi na tulikaribia kukata tamaa tukijua hakuna kinachowezekana tena kutuokoa."
Mallinson anakubali kwamba matumaini yalikuwa yanafifia.
Jumamosi 1 Septemba 04:02 – Kuingizwa kamba
Pisces II iliinuliwa tena na kigeuzi kilichoundwa mahususi na kamba nyingine ya polipropeni.
"Baada ya saa kumi na moja asubuhi ilikuwa na kamba, kwenye nyanja ya aft - walijua tulikuwa bado hai," anasema Chapman.
"Kisha saa 0940 CURV III ikashuka na kuweka kamba nyingine, huku kigeuzi kikiingizwa kwenye ufunguzi wa nyanja ya aft. Tulikuwa tunashangaa ni nini kilikuwa kikiendelea, kwa nini hatukuwa tukiinuliwa."
Chapman anasema ilikuwa wakati huu - wakati manahodha walijua kuwa kuna kamba ilikuwa imeunganishwa – wakiwa wamebaki na mkebe wa limau na sandwich.
Lakini Mallinson anasema hakuwa na uhakika kwamba shughuli ya kuwainua kutoka kwenye sakafu ya bahari ingefanikiwa.
10:50 – Kuinuliwa kwa Pisces III kulianza
"Mara tu tulipoanza kuinuliwa kutoka kwenye sakafu ya bahari hali ilikuwa mbaya sana," anasema Chapman. Kuinuliwa kulisimamishwa mara mbili wakati wa kupanda.
Mara moja kwa futi 350, ili CURV itenganishwe, na mara ya pili kwa futi 100, ili wapiga mbizi waweze kuambatanisha kamba nzito zaidi za kuinua.
13:17 – Kusafisha maji
Pisces III aliburutwa kutoka chini ya maji.
"Inaonekana walidhani tumekufa walipotutazama, ilikuwa vurugu sana," anasema Chapman.
"Walipofungua milango na hewa safi na mwanga wa jua ukaingia ndani tulipata maumivu ya kichwa, lakini tulipata ufumbuzi wa kilichokuwa kinatusumbua, tulikuwa na furaha.
Lakini pia tulikuwa wanyonge kidogo. Ilikuwa vigumu kutoka nje ya nyambizi ndogo, tulikuwa tumeishiwa nguvu sana, hatungeweza hata kusonga."
Ukweli ni kwamba Mallinson anasema ilichukua dakika 30 kufungua mlango.
"Ulikuwa umejifunga na haikufunguka juu chini. Ulipofunguka, ilipasuka na kutoa mlio kama bunduki, tulisikia tu harufu ya hewa ya bahari yenye chumvi," anasema.
Manahodha hao walikuwa wamekaa katika nyambizi Pisces III kwa saa 84 na dakika 30 wakati hatimaye waliokolewa.
"Tulikuwa na masaa 72 ya maisha tulipoanza kupiga mbizi kwa hivyo tulifanikiwa kuchukua masaa 12.5 zaidi. Tulipotazama kwenye silinda, tulikuwa na dakika 12 za oksijeni," anasema Chapman.
Baada ya tukio

Chanzo cha picha, PA Media
Majaribio ya uokoaji yaliteka hisia za vyombo vya habari na umma.
Muda mfupi baada ya uokoaji, Roger Chapman aliondoka Vickers na kuunda kampuni ya Rumic, ikitoa huduma na shughuli za baharini kwa tasnia ya pwani na ulinzi.
Alikua mamlaka inayoongoza juu ya uokoaji chini ya maji, na kujumuishwa kwa timu ya kuzama majini kwa niaba ya Jeshi la Wanamaji la Kifalme mnamo mwaka 2000, na kuchukua jukumu kuu katika kuwaokoa wafanyakazi saba wa manowari ya Urusi AS-28 Priz mnamo 2005.
Wakati huo huo Mallinson, ambaye anaishi katika Wilaya ya Ziwa, aliendelea kufanya kazi kwa kampuni hiyo hiyo upande wa kuzama majini hadi 1978.
Alijihusisha sana katika kurejesha injini za stima, akipokea tuzo ya Lifetime Achievement kutoka kwa Prince Michael wa Kent kwa kujihusisha na The Shamrock Trust, huko Windermere, mwaka wa 2013.
Wanaume hao wawili waliendelea kuwasiliana, wakikutana kila mwaka.
Chapman alifariki dunia kutokana na saratani mnamo mwaka 2020, akiwa na umri wa miaka 74.














