Dalili za kwanza za ugonjwa wa kisukari na maswali mengine 4 yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu ugonjwa huu

f

Chanzo cha picha, PIXELSEFFECT

Maelezo ya picha, Sukari iliyochakachuliwa huongeza kiwango cha glucose katika damu yetu.

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa sugu ambao mtu yeyote anaweza kuugua.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 422 wanaishi na ugonjwa wa kisukari sasa duniani kote, ikiwa ni mara nne zaidi ya miaka 40 iliyopita, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Ugonjwa wa kisukari hutokea wakati mwili hauwezi kutumia sukari inayotengenezwa na mwili (glucose) yote katika damu.

Kwa kawaida glucose yenyewe si mbaya, kwani nimafuta ya seli zote katika mwili.

Kwa baadhi ya tishu, kutumia glucose hii, zinahitaji hatua ya insulini, ambazo ni homoni zinazozalishwa na kongosho ambayo inaruhusu sukari hii kupenya kwa urahisi zaidi ndani ya seli, na hivyo kubadilishwa kuwa nishati.

Matatizo ya kisukari yanaweza kusababisha mshtuko wa moyo, kiharusi, upofu, kushindwa kufanya kazi kwa figo na kukatwa kwa viungo vya mwili.

Licha ya hatari, watu wengi wenye ugonjwa wa kisukari hawajui kuwa wanao. Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kuzuia mtu kuugua kisukari.

BBC inaangalia maswali yanayoulizwa mara kwa mara ambayo watu wamekuwa wakiuliza katika mtandao wa Google kuhusu ugonjwa wa kisukari na tunayawasilisha kwa wataalamu watatu.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sukari iliyochakachuliwa huongeza kiwango cha glucose katika damu yetu.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Kwa kawaida, daktari hutoa tahadhari kwa mgonjwa mgonjwa kuwa mgonjwa ana aina ya kisukari cha aina ya 2 kulingana na matokeo ya vipimo vya maabara vya kupima sukari ya damu.

Wagonjwa wengi wenye aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari kwa kawaida huwa hawana dalili. Dalili ni za kawaida zaidi kwa wagonjwa wenye aina ya kisukari cha 1, wakati viwango vinapokuwa vya juu sana kwa muda mrefu.

"Mchoko wam wili, kiu, njaa, kukojoa kupita kiasi, maono ya ukungu na kupoteza uzito wa mwili kunaweza kuwa dalili," anasema Victor Montori, mtaalamu aliyebobea katika ugonjwa wa kisukari katika Kliniki ya Mayo nchini Marekani.

"Kwa watoto, mara nyingi huwa na ya 1 ya kisukari. Dalili kwa ujumla ni kali zaidi na hutokea ndani ya kipindi kifupi cha muda: kiu kali, kupoteza uzito, kukojoa mara kwa mara, uchovu, kusinzia." - José Agustín Mesa Pérez, rais wa Chama cha Kisukari cha Amerika ya Kusini.

"Katika miongo michache iliyopita, tumeona ongezeko la kutisha la visa vya aina ya 2 ya kisukari miongoni mwa watoto na vijana, linalohusishwa na tabia za maisha ya kukaa." - Dkt Fabiana Vazquez, Mwanachama wa Jumuiya ya Kisukari ya Argentina, anasema.

Insulin ni homoni inayozalishwa na kongosho inayoruhusu mwili wetu kunyonya glucose mwilini.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Insulin ni homoni inayozalishwa na kongosho inayoruhusu mwili wetu kunyonya glucose mwilini.

Ni wakati gani sukari ya damu ni hatari?

"Katika hali ya kufunga, kiwango cha kawaida cha sukari kwenye damu ni miligramu 70 hadi 110 kwa desilita (mg/dl). Baada ya chakula, kiwango hiki huongezeka, lakini insulini inahakikisha kuwa sukari inarudi kwenye kiwango cha kawaida haraka (kwa ujumla masaa 2 "Vipimo vya juu ya 180 mg / dl vinavyohifadhiwa kwa zaidi ya masaa 2 ni sumu kwa seli na, kiwango hiki kimejirudia mara kwa mara, inaweza kusababisha madhara ya kudumu hasa kwa figo, macho, moyo na mishipa ya miguu.

"Ikiwa kiwango cha sukari ni cha juu Kwa muda mrefu, mwili huathiriwa. Kwa hiyo, watu wenye ugonjwa wa kisukari wanapaswa kuwa na viwango vya sukari ya damu kati ya 70 na 180 mg / dl kwa siku." – anasema Dkt Fabiana Vazquez, mwanachama wa Jumuiya ya Kisukari ya Argentina.

"Mgonjwa wa kisukari aina ya 2 anaweza kuanza kupungukiwa na maji mwilini wakati kiwango cha sukari kinazidi 200 mg/dL, lakini watu wasio na matatizo mengine wanaweza kudumisha kiwango cha juu cha sukari bila hatari zaidi. Wakati kiwango ni cha juu sana, kwa mfano "juu ya 300 mg / dL. dL, hatari ni kubwa na inahitaji tahadhari maalum" - Victor Montori, mtaalam aliyebobea katika ugonjwa wa kisukari katika Kliniki ya Mayo nchini Marekani.

"Pia tunahitaji kuzungumzia kuhusu viwango vya chini. Watu wenye ugonjwa wa kisukari, hata wale walio na matatizo, wanapaswa kuepuka kuwa na kiasi cha sukari ya glucose chini ya 70 mg / dl, wakati wa kufunga na baada ya kula, "kwa mujibu wa José Agustín Mesa Pérez, rais wa Chama cha Kisukari cha Amerika ya Kusini.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuhisi uchovu sana, kiu ya mara kwa mara na kukojoa zaidi ya kawaida ni baadhi ya dalili za ugonjwa wa kisukari

Kuna tofauti gani kati ya aina ya kisukari cha 1 na aina ya kisukari cha 2?

"Katika uainishaji wa ugonjwa wa kisukari kuna aina 4, lakini kwa mazoezi inaelezwa kama aina ya 1 au 2. Aina ya 1 kawaida hutokea kwa vijana chini ya umri wa miaka 30, ambao hawana historia ya kurithi ya ugonjwa wa kisukari."

"Kwa kawaida hutokea kwa dalili kali. Aina ya kisukari cha 2 kawaida hutokea kwa watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 40, kuhusiana na uzito mkubwa na ukubwa wa tumbo uliopimwa sentimita 80 kwa wanawake na sentimita 90 kwa wanaume.

Sukari wakati mwingine huhusishwa na shinikizo la damu na ini lenye mafuta" kulingana na José Agustín Mesa Pérez, rais wa Chama cha Kisukari cha Amerika ya Kusini.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu milioni 422 wanaishi na ugonjwa wa kisukari duniani

Ugonjwa wa kisukari unaweza kutibiwa? Je, tunaweza kuepuka?

"Ugonjwa wa kisukari hauwezi kupona, lakini kama unadhibitiwa vizuri, mtu anaweza kuishi maisha ya kawaida. Hakuna njia ya kujua ni nani atapata aina ya kisukari cha 1, wala hakuna njia yoyote ya kukizuia

Kwa upande mwingine, kisukari cha aina ya 2 huwa na vichocheo wazi sana. "Kuwa na uzito wa kawaida, lishe bora na yenye uwiano. Shughuli za kawaida za mwili zinaweza kuzuia au kuchelewesha mwanzo wa ugonjwa wa kisukari kwa watu wenye maumbile makubwa," kulingana na Dk Fabiana Vazquez, mwanachama wa Jumuiya ya Kisukari ya Argentina.

"Upandikizaji wa kongosho ni njia mbadala ya haraka ambayo mara nyingi hutatua ukosefu wa insulini katika aina ya 1 ya kisukari" anaongeza Victor Montori, mtaalam aliyebobea katika ugonjwa wa kisukari katika Kliniki ya Mayo nchini Marekani.

"Hakuna tiba na lazima tuwe makini sana na wadanganyifu ambao wanaahidi. Lakini huu ni ugonjwa sugu ambao unaweza kudhibitiwa kabisa, na kazi kubwa zaidi inahitajika kupunguza sababu za hatari, ni rahisi kuudhibiti na kuepuka matatizo mengine, "anasema José Agustín Mesa Pérez, mtaalam na rais wa Chama cha Kisukari cha Amerika ya Kusini.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kutumia sukari ya matunda badala ya sukari ya viwandani na kula vyakula vya nafaka nzima ni njia moja ya kusaidia kudhibiti sukari kwenye damu

Ni vyakula gani vinavyosababisha ugonjwa wa kisukari?

" Hapana. Hakuna chakula ambacho kinaweza kusababisha kisukari peke yake. Mkanganyiko huo unatokana na ukweli kwamba mtu wa kale alihitaji kuweka akiba ya nishati ili kuweza kuishi na alifanikisha hili kupitia njia za kuokoa insulini." Lakini kwa sasa nishati hiyo hiyo haitumiki na badala yake inaleta athari za kiafya baada ya kulimbikizwa kwa kutotumiwa.

"Kula mboga za kijani kibichi na matunda ya rangi tofauti inaweza kusaidia kusawazisha lishe na kuongeza kinga ya mwili ya asili ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kisukari." "kiwango cha juu cha mafuta, hasa kama ya asili ya wanyama, pamoja na wanga rahisi na vyakula vya viwandani vinahusishwa na hatari kubwa ya kupata aina ya kisukari cha 2.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi