Zifahamu njia nane za kupunguza matumizi ya sukari mwilini

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Tunafahamu kwamba matumizi ya sukari kwa kiasi kikubwa sio nzuri kwa afya yako. Utafiti umeonyesha kuwa utumiaji wa sukari nyingi huchangia magonjwa kama vile kunenepa kupita kiasi, ugonjwa wa moyo, kisukari cha aina ya 2, na kuoza kwa meno.

Sukari asilia hupatikana katika matunda na mboga, lakini zinachukuliwa kuwa zenye afya kwa sababu zina wingi wa vitamini, madini, na virutubishi vingine, hii inamaana kuwa mara nyingi huwa na athari kidogo kwenye viwango vya sukari ya damu.

Tatizo halisi ni sukari iliyoongezwa, kama zile zinazopatikana katika vyakula vilivyochakatwa sana kama sukari nyeupe na sharubati ya mahindi.

Sukari hizi mara nyingi huletwa kwenye vyakula vilivyosafishwa ili kuboresha ladha na zinaweza kujilimbikiza haraka ikiwa hazijadhibitiwa.

Ikiwa unatafuta mbadala wa sukari, miongozo ya kuoka keki na mikate bila sukari au unataka tu kujua kiasi kinachopendekezwa kutumika kwa siku, huu hapa ndio mfumo unaopendekezwa.

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Njia 8 za Kupunguza Ulaji wa Sukari

Kwa kufanya mabadiliko machache kwenye lishe yako, unaweza kupunguza ulaji wako wa sukari isiyo ya lazima:

1. Punguza kiasi cha sukari unachoongeza kwenye vinywaji vya moto

Endelea hatua kwa hatua ili kutoa ladha yako wakati wa kurekebisha. Jaribu kuongeza mdalasini kwenye mchanganyiko wa chokoleti moto. Mdalasini una faida kadhaa za kiafya na huongeza ladha bila kuongezwa utamu.

2. Epuka vyakula vinavyosemekana kuwa ''vina mafuta kidogo''

Aina ya vyakula hivi mara nyingi huwa na sukari nyingi. Ni bora kula chakula tu cha kawaida ila kwa kiasi kidogo.

w

Chanzo cha picha, Getty Images

3. jua aina ya vyakula ambavyo havina sukari".

Mara nyingi aina ya vyakula vyenye mafuta huwa na utamu wa kuongezwa kama vile sucralose, saccharin, na aspartame. Ingawa vina ladha tamu, utafiti unapendekeza kwamba hazisaidii kuzuia kuongeza sukari mwilini,, kutuma ujumbe wa kutatanisha kwa ubongo ambao unaweza kusababisha kula kupita kiasi.

4. Sawazisha ulaji wako wa wanga na protini

Jumuisha vyakula kama vile samaki, kuku, bata mzinga na tofu katika mlo. Protini hupunguza na husaidia kwenye kuondoa kitambi., lakini pia ulaji wa vyakula vyenye protini husaidia kwa asilimia kubwa kudhibiti hamu ya kula ovyo ovyo. Jaribu pia ulaji wa mchanganyiko wa matunda kama parachichi na maharagwe meupe.

w

Chanzo cha picha, Getty Images

5. Badilisha ulaji wa vyakula vilivyookwa.

Badilisha mkate mweupe, wali na tambi na matoleo kamili kama vile shayiri, mkate na mkate wa unga, wali wa kahawia na tambi. Badala yake kula mkate uliotengenezwa kutokana na unga mchanganyiko wa.

6. Tumia viungo

Punguza kiasi cha sukari katika mapishi yako badala yake tumia sana viungo ili kuongeza ladha. Lakini pia unaweza kujaribu kula mkate wenye mchanganyiko na unga wa tufaa ( apple).

7. Punguza sukari ya kioevu

Pata glasi moja ya juisi ya matunda badala ya pombe kwa wikendi. Kunywa chai iliyopikwa kwa viungo vya mitishamba au maji na vipande vya machungwa.

8. Kuinua afya

Chukua tunda zima na kiganja cha karanga au sufuria ndogo ya mtindi wa kawaida. Vyote viwili vina protini zinazosaidia kusawazisha viwango vya sukari ya damu na nishati. Jaribu ulaji wa korosho wa mdalasini iliyoenezwa na vipande vya tufaha au mtindi.

Maudhui yote ya afya kwenye BBC yametolewa kwa maelezo ya jumla pekee, na hayapaswi kuchukuliwa kama mbadala wa ushauri wa matibabu wa daktari wako au mtaalamu mwingine yeyote wa afya. Ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu afya yako kwa ujumla, unapaswa kuwasiliana na mtoa huduma wa afya wa eneo lako.