Kisukari: Unahitaji kujua nini kuhusu ugonjwa wa kisukari?

A girl

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aina ya 1 ya kisukari hugundulika mapema wakati wa utoto au ujana. Inaweza kuhusishwa na maumbile au kusababishwa na maambukizi ya virusi

Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanaua watu zaidi ya milioni moja kila mwaka - na mtu yeyote anaweza kuupata.

Husababishwa wakati mwili hauwezi kuchakata sukari (glucose) yote katika mfumo wa damu; matatizo yake yanaweza kusababisha mshtuko wa moyo, kiharusi, upofu, figo kushindwa kufanya kazi na kukatwa kiungo cha chini.

Ni tatizo linaloongezeka kila uchwao- wastani wa watu milioni 422 wanaishi na kisukari duniani - mara nne zaidi ya miaka 40 iliyopita, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Licha ya hatari ya ugonjwa huu, nusu ya watu walio na ugonjwa wa kisukari hawajui. Lakini mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kuzuia kupatwa ugonjwa huu.

Nini kinachosababisha ugonjwa wa kisukari hasa?

Tunapokula, mwili wetu hugawanya wanga ndani ya sukari (glucose). Homoni iitwayo insulini, inayozalishwa kwenye kongosho, kisha huelekeza seli za mwili wetu kunyonya sukari hizo kwa ajili ya nishati.

Kisukari kinatokea wakati kongosho haizalishwi au haifanyi kazi ipasavyo, hivyo kusababisha sukari kujilimbikiza katika damu.

Sugar cubes and a spoonful of sugar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matumizi makubwa ya sukari huongeza kiwango cha sukari kwenye damu

Je, kuna aina gani za kisukari?

Kuna aina kadhaa za ugonjwa wa kisukari.

Aina ya ya 1 ya kisukari, kawaida kongosho huacha kuzalisha insulini, hivyo sukari hujilimbikiza kwenye damu.

Wanasayansi hawajui hasa kwa nini hii hutokea lakini wanaamini kuwa inaweza kuchochewa na jeni au kutokana na maambukizi ya virusi ambayo huharibu seli zinazozalisha insulini kwenye kongosho. Takriban asilimia 10 ya watu walio na ugonjwa wa kisukari wana aina hii ya 1.

Kisukari aina ya 2 , kawaida kongosho inakuwa haitoi insulini ya kutosha au homoni haifanyi kazi vizuri.

Medical illustration of the pancreas

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Insulini ni homoni inayozalishwa kwenye kongosho ambayo huwezesha mwili wetu kunyonya sukari

Hii kwa kawaida hutokea kwa watu wenye umri mkubwa, wa makamo na wazee, lakini pia vijana ambao ni wazito na wanao kaa tu bila kuushughulisha mwili, na watu kutoka makabila fulani, hasa Asia Kusini.

Baadhi ya wanawake wajawazito wanaweza kugunduliwa kuwa na kisukari wakati miili yao haiwezi kutoa insulini ya kutosha kwa ajili yao na mtoto.

Tafiti mbalimbali zinazotumia vigezo tofauti zinakadiria kuwa kati ya asilimia 6 hadi 16 ya wajawazito watapata kisukari wakati wa ujauzito. Wanahitaji kudhibiti viwango vyao vya sukari kupitia lishe, mazoezi ya mwili na/au matumizi ya insulini ili kuizuia isiendelee kuwa aina ya 2.

Watu wanaweza pia kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa kisukari - kwa kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu na kusababisha ugonjwa wa sukari.

Nini dalili za ugonjwa wa kisukari?

A tired doctor sleeps in a hospital armchair

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuhisi uchovu mwingi, kiu ya mara kwa mara na kukojoa kuliko kawaida ni miongoni mwa dalili za kisukari

Dalili za kawaida ni pamoja na:

  • Kuhisi kiu sana
  • Kukojoa zaidi ya kawaida, hasa usiku
  • Kujisikia kuchoka sana
  • Kupunguza uzito bila kujaribu
  • Thrush ambayo inaendelea kurudi
  • Uoni hafifu
  • Vidonda ambavyo havitibiki

Kwa mujibu wa Mamlaka ya huduma za kitaifa za Afya ya Uingereza, dalili za ugonjwa wa kisukari cha aina ya 1 huonekana mapema wakati wa utoto au ujana na kuwa mbaya zaidi.

Watu walio katika hatari zaidi ya aina ya 2 ni zaidi ya umri wa miaka 40 (au 25 kwa watu wa kusini mwa Asia); wenye mzazi au ndugu mwenye kisukari; wenye uzito mkubwa; na wana asili ya Asia Kusini, Wachina, Caribbean au Wenye asili ya Afrika.

Naweza kuzuia kupata Kisukari?

Ugonjwa wa kisukari hutegemea maumbile na mazingira lakini unaweza kusaidia kuweka viwango vya sukari kwenye damu yako kwa lishe bora na mtindo wa mzuri wa maisha.

Fruits, wholemeal grains and healthy oils

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uchaguzi wa vyakula ni muhimu katika kudhibiti uhonjwa wa kisukari

Muhimu kuepuka vyakula na vinywaji vya sukari vilivyochakatwa, na kuachana na vyakula kama mkate mweupe.

Sukari iliyosafishwa na nafaka zilizosafishwa zinakuwa na virutubishi vichache kwa sababu sehemu zenye nyuzi, zenye vitamini nyingi zinakuwa zimeondolewa. Mifano ni pamoja na unga mweupe, mkate mweupe, wali mweupe, tambi nyeupe, maandazi, vinywaji vya sukari/sukari, peremende, na vitafunwa kama maandazi, chapati nk, zilizoongezwa sukari.

Lishe nzuri yenye afya ni pamoja na mboga mboga, matunda, maharage na nafaka nzima. Pia inajumuisha mafuta yenye afya, karanga na samaki wenye mafuta mengi ya omega-3. Ni muhimu kula mara kwa mara na kuacha kula wakati umeshiba.

Mazoezi ya mwili pia yanaweza kusaidia kupunguza viwango vyako vya sukari kwenye damu. Mfumo wa Kitaifa wa Afya wa Uingereza (NHS) unapendekeza angalau saa 2.5 za mazoezi ya aerobic kwa wiki, ambayo yanaweza kujumuisha kutembea haraka na kupanda ngazi.

Shot

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni muhimu kufanya mazoezi angalau kwa masaa 2 na nusu kila wiki

Uzito wenye afya utarahisisha mwili wako kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu. Ikiwa unahitaji kupunguza uzito, jaribu kufanya hivyo polepole, upunguze kati ya kilo 0.5 na kilo 1 kwa wiki.

Ni muhimu pia kutovuta sigara na kutazama viwango vyako vya cholesterol ili kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Je, matatizo ya kisukari ni yapi?

Kiwango cha juu cha sukari katika damu kinaweza kuharibu mishipa ya damu.

Ikiwa damu haiwezi kutiririka vizuri katika mwili wako, haiwezi kufikia sehemu za mwili zinazohitaji damu, kunapoteza hisia na maumivu), kupoteza kuona na maambukizi ya miguu.

Shirika la afya duniani (WHO) inasema ugonjwa wa kisukari ndio chanzo kikuu cha upofu, figo kushindwa kufanya kazi, mshtuko wa moyo, kiharusi na kukatwa viungo vya chini vya miguu.

An actor simulating a heart attack

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ugonjwa wa kisukari ndio chanzo kikuu cha upofu, kushindwa kwa figo, mshtuko wa moyo, kiharusi na kukatwa viungo vya chini vya miguu, kwa mujibu wa UN.

Mwaka 2016, inakadiriwa kulikuwa na vifo milioni 1.6 vilivyosababishwa moja kwa moja na ugonjwa wa kisukari.

Je! ni watu wangapi wana kisukari duniani?

Kwa mujibu wa WHO, idadi ya watu wenye ugonjwa wa kisukari imeongezeka kutoka milioni 108 mwaka 1980 hadi milioni 422 mwaka 2014.

Mwaka 1980, asilimia chini ya 5% ya watu wazima wenye umri wa miaka 18 na kuendelea walikuwa na ugonjwa wa kisukari ulimwenguni - wakati 2014, kiwango kiliongezeka na kuwa 8.5%.

Shirikisho la Kimataifa la Kisukari linakadiria kuwa karibu 80% ya watu wazima wanaoishi na hali hiyo wako katika nchi za kipato cha kati na cha chini, ambapo tabia ya ulaji imekuwa ikibadilika kwa kasi.

Katika nchi zilizoendelea, inahusishwa na umaskini na matumizi ya vyakula vya bei nafuu, vilivyotengenezwa.