Panya, mifupa, tope na vyakula vingine ambavyo watu wanakula kutokana na baa la njaa

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika Siku ya Chakula Duniani, tuliongea na watu ambao wamekata tamaa na kuwauliza jinsi walivyonusurika kufa njaa.
Njaa, umaskini, vita, magonjwa: Sababu nyingi zinaweza kubadili kabisa mlo wetu.
Katika hali isiyo ya kawaida, watu waliokata tamaa wanaweza kushawishika katika kula tope, tunda, maua, panya, mifupa iliyoachwa, au ngozi za wanyama, ndizo wanazokula ndio wawe hai.
Njaa na utapiamlo mkali ni changamoto ya kila siku katika sehemu nyingi za dunia, na kiwango chao ni cha ajabu: Programu ya Umoja wa Mataifa ya Chakula Duniani inadai kuwa "watu milioni 828 huenda kitandani kila usiku wakiwa na hawajakula kitu" na kwamba "watu milioni 345 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula".
"Panya walikuwa chakula tulichohitaji vibaya sana"
Katika Siku ya Chakula Duniani, iliyoadhimishwa Oktoba 16, BBC ilizungumza na watu wanne kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambao wamekabiliwa na njaa, na kuuliza jinsi walivyonusurika. "Nimekula nyama ya panya tangu nilipokuwa mtoto na sijawahi kupata matatizo yoyote ya kiafya.

Chanzo cha picha, RANI
Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 49 anaishi karibu na Chennai na ni mmoja wa jamii zinazotengwa sana nchini humo: Aliacha shule baada ya mwaka wa tano.
Katika muundo wa kijamii wenye makao yake makuu nchini India, kabila lake lilikumbwa na ubaguzi wa miaka mingi. Rani anafanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali linalosaidia watu wa jamii yake, Irula, ambalo linalazimishwa kufanya kazi kwa bidii.
"Tumekuwa tukiishi nje ya miji na vijiji. Wazazi wetu na babu zetu walituambia kwamba wakati mwingine hawakuwa na kitu cha kula, hata chakula kama mihogo hawakupata. Katika nyakati hizi ngumu, panya wakawa chakula ambacho tulihitaji sana. Nilijifunza kuwanasa tangu nikiwa na umri mdogo ", Rani aliiambia BBC.
Ujuzi wa kuishi Rani alijifunza kama mtoto sasa unasaidia familia yake mwenyewe kula kwa kupika panya takriban mara mbili kwa wiki.
Irula hula aina ya panya wanaopatikana kwenye vitaluni vya mpunga, si wale wanaopatikana majumbani.

Chanzo cha picha, RANI
"Tunawanyofoa panya ngozi na kuchoma nyama juu ya moto na kuila. Wakati mwingine sisi hukata kata vipande vidogo na kupika kama mchuzi wa dengu", Rani anaelezea.
Nafaka zilizofichwa na panya katika mashimo yao pia huchukuliwa na Irula na kuliwa.
"Naweza tu kumudu kula kuku au samaki mara moja kwa mwezi. Panya wanapatikana kwa wingi, na wao ni bure. Nilikunywa maji yenye tope na kuona watu wakila nyama ya mizoga ", anaongeza.
Umoja wa Mataifa unasema Somalia inakabiliwa na njaa na ukame mbaya katika kipindi cha miaka arubaini na tayari watu zaidi ya milioni 1 wamehama makazi yao.

Chanzo cha picha, ABDULKADIR MOHAMED/NRC
Sharifo Hassan Ali, 40, mama wa watoto saba, ni miongoni mwa wale waliohama makazi yao.
Ilibidi aondoke kijiji chake na kusafiri zaidi ya kilometa 200 - kwa miguu - kutoka mkoa wa Loaker Shabell hadi kambi iliyo nje ya mji wa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. Ilimchukua siku tano.
"Wakati wa safari, tulikula mara moja tu kwa siku. Wakati hapakuwa na chakula kingi, tuliwalisha watoto tu ", anasema.
Akiwa njiani kuelekea mji mkuu, alishuhudia matukio ya kushangaza.
"Niliona mamia ya wanyama waliokufa wakielekea Mogadishu. Watu wanakula mizoga na ngozi za wanyama ", anasema.
Hassan Ali alikuwa na ng 'ombe 25 na mbuzi 25. Wote waliangamia katika ukame. "Hakuna mvua na hakuna kitu kinachokua kwenye shamba langu", anasema.

Chanzo cha picha, ABDULKADIR MOHAMED/NRC
Sasa anapata chini ya dola mbili kwa siku akifua nguo za watu wengine, ambazo hazitoshi kununua chakula. "Ni vigumu kununua kilo ya mchele na mboga za majani, na kamwe haitoshi kwa kila mtu. Ukame huu umekuwa mgumu kwetu ".
Hassan Ali anasaidiwa na mashirika ya kutoa misaada, lakini anasema haitoshi.
"Hatuna kitu. Familia yangu inategemea ngozi iliyokatwakatwa na mifupa kutoka kwa wanyama", anasema. Kwa miaka miwili iliyopita, Lindinalva Maria da Silva Nascimento, mwenye umri wa miaka 63 aliyestaafu kutoka Sao Paulo, amekuwa akila mifupa na ngozi iliyokatwakatwa na wachinja nyama.

Chanzo cha picha, FELIX LIMA/ BBC NEWS BRAZIL
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mtu anayestaafu ana bajeti ya kila siku ya dola nne tu kwa ajili yake mwenyewe, mume wake, mtoto wa kiume na wajukuu wawili. Hawezi kumudu kula nyama, hivyo huenda kwa wachinjaji nyama tofauti na kununua mizoga ya kuku na ngozi kwa dola 0.70 kilo.
"Ninapika mifupa yenye nyama nyama zilizobaki kwenye ngozi. Naongeza maharage ili iwe na ladha. Ngozi ya kuku, anasema hukaangwa kwenye sufuria isiyo na mafuta na mafuta yanayolimbikizana hukusanywa na kuhifadhiwa ". Lindinalva Maria da Silva Nascimento anaihifadhi kwenye mitungi mitupu ya mayonnaise na jibini vyakula vingine vilivyokauka ndani yake baadaye.
"Hata sifikirii kununua matunda, mboga au vyakula vitamu. Hapo kabla, nilikuwa na friza iliyojaa nyama na mboga mboga na jokofu alikuwa na kabeji, nyanya, vitunguu, yaani vilikuwa vingi tu", anakumbuka. "Leo ni tupu na kitu pekee nilicho nacho ni vitunguu kwenye bakuli la tunda".
Lindinalva Maria da Silva Nascimento alipoteza kazi yake wakati wa janga hilo na mwanawe pia hana kazi.
"Nategemea michango ya chakula kutoka kwa watu ninaowajua na pia baadhi ya misaada kutoka kwa kanisa Katoliki nchini. Hivyo ndivyo ninavyoendelea kuishi ", anasema.

Kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Mtandao wa Brazil wa Hifadhi ya Chakula, zaidi ya watu milioni 33 nchini Brazil wanaishi kwa njaa. Kwa mujibu wa utafiti huu mpya uliochapishwa mwezi Juni, zaidi ya nusu ya idadi ya watu wanaathirika na ukosefu wa chakula.
"Mara nyingi wanaochinja nyama wanasema hawana mifupa", Lindinalva analalamika, akisema anahitaji kula kidogo tu ili kuhifadhi baadhi ya chakula.
"Mimi pia huishi kwa imani tu, nikijiambia kwamba mambo yatakuwa sawa wakati fulani. Mimi na watoto wangu tumenusurika kutokana na matunda ya mekundu ya dungusi".
"Hakuna mvua na hakuna mavuno. Hatuna cha kuuza. Hatuna pesa. Siwezi kumudu kula wali ", alisema.
Fefiniaina ni mama wa miaka 25 kutoka Madagascar.
Miaka miwili ya mvua za vuli ziliharibu mazao na kupungua kwa mifugo.
Hii inafanya zaidi ya watu milioni 1 kuwa na njaa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Chanzo cha picha, UNICEF/RAKOTO/2022
Maisha ya Fefiniaina katika mji wa Amboasary, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame.
Yeye na mumewe wanapata riziki kwa kuuza maji. "Wakati mimi napata fedha, mimi hununua mchele au muhogo.
Wakati sina chochote, ninapaswa kula tunda la jekundu la dungusi au kwenda kulala bila kula kitu ", aliambia BBC kupitia kwa mfasiri wa Unicef.
"Watu wengi hapa wanakula tunda la dungusi. Lina ladha kidogo kama ukwaju. Tumekuwa tukila kwa muda wa miezi minne iliyopita na sasa watoto wangu wawili wanaugua ugonjwa wa kuhara,” alisema.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa mwaka jana liliripoti kwamba katika nchi ya Madagascar ya kusini, "watu walikula udongo mweupe na juisi ya ukwaju, majani ya dungusi, chakula mwitu, ili kukidhi njaa yao".
Tunda hili linaweza kusaidia kuifanya familia ya Fefiniaina kuwa hai, lakini halitoi vitamini na madini anayoyahitaji - mtoto wake wa miaka minne ni mmoja wa watoto wengi wanaopata matibabu ya utapiamlo.

Chanzo cha picha, UNICEF/RAKOTO/2022
"Kwa kuwa tuna mvua kidogo, tunaweza kupata mazao. Tunaweza kula viazi vitamu, mihogo na matunda. Na hatutahitaji kula matunda mwitu ya dungusi", anasema Fefiniaina. Mpango wa Chakula Duniani unasema dunia ni ya njaa kuliko wakati mwingine wowote ule.
Anasimulia "janga hili la njaa" kwa kuzingatia sababu nne: Mgogoro, mabadiliko ya hali ya hewa, athari za kiuchumi ya janga la Covid-19 na kupanda kwa gharama ya maisha.
"Gharama za uendeshaji wa mpango wa chakula duniani kwa mwezi ni Dola za Marekani milioni 73.6 (sawa na asilimia 49.6 za faranga za CFA) zaidi ya wastani wao wa mwaka 2019, na ongezeko la asilimia 44 la mwaka huu", ripoti hiyo ilisema.
"Ongezeko la gharama za uendeshaji kwa leo hapo awali zingewalisha watu milioni nne kwa mwezi", nyaraka hiyo inaongeza.
Lakini shirika hilo limedai kuwa halitoshi kuwa na fedha za kuzuia mgogoro huo: Isipokuwa kama kutakuwa na utashi wa kisiasa wa kumaliza migogoro hiyo na kujitolea kukabiliana na ongezeko la joto duniani, la sivyo, hali hii itaendelea," ripoti hiyo inahitimisha. Felipe Souza alichangia ripoti hii.















