Aubameyang, Ayew, Lukaku... wafahamu wachezaji wa soka Ulaya ambao baba zao walikuwa wachezaji nyota Afrika

.

Chanzo cha picha, instagram

Maelezo ya picha, Aubameyang, Andrew Ayew and Jordan Ayew and Romelu Lukaku

Kandanda ndio mchezo unaopendwa zaidi barani Afrika kwa sababu ya jinsi watu wanavyoupenda.

Ukanda wa Afrika umeipa dunia watu wengi maarufu katika mchezo huo na ndio maana jina la Afrika linapotajwa , majina mengi maarufu yatakuwa kwenye mioyo ya watu.

Kadiri miaka inavyosonga mbele, mafunzo ya soka yamekuwa yakitoka kwa wazazi waliocheza soka zamani na kurithiwa na Watoto wao.

Haya hapa ni baadhi ya majina ya Kiafrika ambayo ni maarufu kwa sasa kama vile majina yao ya ukoo yalivyokuwa nyakati za kale:

Andre na Jordan Ayew

.
Maelezo ya picha, Andrew Ayew na Jordan Ayew wakiwa pamoja na baba yao Abedi Pele

Andre Ayew na kaka yake Jordan Ayew ni wachezaji nyota ambao baba yao Abedi Pele aliwahi kuwa mchezaji tajika barani Afrika.

Abedi anachukuliwa kuwa mchezaji bora wa kandanda barani Afrika kwa sababu ya jinsi aliyocheza wakati akiiwakilisha nchi yake ya Ghana kutoka 1982 hadi 1998.

Alikuwa sehemu ya timu ya Ghana ilioshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 1982, lakini hakucheza Kombe lolote la Dunia kabla ya kustaafu.

Wanawe watatu, Andre, Jordan na Rahim wote ni wanasoka, lakini ni Andre na Jordan ambao majina yao yanasikika zaidi.

Mnamo Desemba 2011, Andre Ayew alishinda tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka; babake Abedi pia aliwahi kushinda tuzo hii mnamo 1991.

Kwa sasa, Andre anachezea klabu ya soka ya Al Sadd nchini Qatar huku Jordan akiichezea klabu ya soka ya Crystal Palace ya nchini England.

Pierre-Emerick Aubameyang

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Chelsea Pierre Emerick Aubameyang na babake Aubameyang kuliaPierre-François Aubameyang

Aubameyang amechezea timu nyingi za soka maarufu barani Ulaya zikiwemo: AC Milan, Borussia Dortmund, Arsenal, Barcelona, na Chelsea anakocheza kwa sasa.

Nyota huyo pia ameichezea nchi yake Gabon mechi 72 na kufunga mabao 30 kabla ya kustaafu kuichezea nchi yake Mei 2022.

Baba yake Pierre-François Aubameyang pia aliichezea Gabon kutoka 1985 hadi 1998.

Aliichezea Gabon katika Kombe la Mataifa ya Afrika 1994 (kama nahodha) na 1996, lakini hakushinda taji lolote kabla ya kustaafu.

Mzee Aubameyang pia aliwahi kuzichezea Stade Lavallois na Le Havre za Ufaransa.

Roger Lukaku, babake Romelu Lukaku

.

Chanzo cha picha, African football twitter

Maelezo ya picha, Romelu Lukaku na babake Roger Lukaku

Romelu Lukaku ni jina maarufu katika soka barani Ulaya kutokana na uwezo wa nyota huyu, lakini wengi hawajui kuwa baba yake Roger Lukaku pia aliwahi kuichezea Kongo ilipokuwa Zaire, kuanzia miaka ya 1993 hadi 1996.

Roger Lukaku alichezea KV Oostende, KV Mechelen na Germinal Ekeren za Ubelgiji kabla ya kustaafu mwaka 1999.

Romelu Lukaku kwa sasa anachezea Ubelgiji na ndiye mfungaji bora wa timu ya taifa ya soka, kwani amefunga mabao 68.

Kaka yake, Jordan Lukaku, pia anachezea SD Ponferradina ya Uhispania.

Timothy Tarpeh Weah

.

Chanzo cha picha, George Weah Instagram

Maelezo ya picha, Rais wa Liberia George Weah na mwanwe Timothy Weah wakati wa kombe la dunia la 2022

Tangu kuanza kwa soka, ni Mwafrika mmoja tu aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia; mtu huyo ni nyota wa Liberia anayeitwa George Weah, ambaye sasa ni rais wa nchi ya Liberia.

Lakini jambo moja ambalo George Weah hajalifurahia ni kushiriki katika Kombe la Dunia.

Mnamo 2022, mwanawe Timothy Weah alifanya kile ambacho baba yake alishindwa kufanya aliposafiri na USA kwenye Kombe la Dunia huko Qatar.

Kabla ya kujiunga na timu ya soka ya Marekani, Timothy Weah alipata fursa ya kucheza soka katika nchi nne: Marekani - alikozaliwa, Liberia - nchi ya baba yake, Jamaica - nchi ya mama yake, na Ufaransa ambako amekuwa tangu akiwa na umri wa miaka 14. .

Nchini Qatar 2022, Timothy alifunga bao dhidi ya USA na Wales, bao lake la kwanza la Kombe la Dunia.

Wachezaji wengine...

.

Chanzo cha picha, Screen Grab

Maelezo ya picha, Mchezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na mwanawe Isaac Drogba

Isaac Drogba, mtoto wa Dider Drogba, tayari anacheza soka, lakini timu ya taifa ya kandanda ya Cote D'Ivoire haijamwalika kujiunga nao. Isaac alichezea klabu ya mazoezi ya Chelsea, lakini kwa sasa yuko Italia ambako anachezea Falgore Caratese.

Etienne Eto'o, mtoto wa Samuel Eto'o Fils wa Cameroon, alianza kucheza soka katika klabu ya Real Mallorca ya Uhispania. Baba yake Samuel Eto'o ndiye mwanasoka aliyetuzwa na kuheshimiwa zaidi barani Afrika. Kwa sasa, Samuel Eto'o ndiye mkuu wa shirikisho la soka nchini Cameroon. Mwanawe Etienne pia ameichezea Cameroon katika timu za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21.

Sean Nwankwo, mtoto wa Kanu Nwankwo wa Nigeria anachezea timu ya soka ya Watford nchini Uingereza, akiwa na umri wa miaka 16. Kanu Nwankwo mwenyewe ni mmoja wa wanasoka maarufu wa Nigeria.

Kevin Martins, mtoto wa Obafemi Martins wa Nigeria, kwa sasa anachezea timu ya Italia yenye wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16.