Mamilioni ya punda huuawa kila mwaka kutengeneza dawa

g

Chanzo cha picha, THE DONKEY SANCTUARY

Maelezo ya picha, Punda anaweza kumaanisha tofauti kati ya maisha ya kawaida na ufukara kwa watu wengi katika jamii maskini, za vijijini

Na Victoria Gill na Kate Stephens

BBC, BBC News

Siku hiyo ilianza kama siku yoyote ya kawaida. Asubuhi, aliondoka nyumbani kwake viungani mwa jiji la Nairobi na kwenda shambani kuchukua mifugo yake.

"Sikuwaona," anakumbuka. "Nilitafuta siku nzima, usiku kucha na siku iliyofuata." Siku tatu baadaye alipigiwa simu na rafiki yake akimwambia amepata mifupa ya wanyama hao. "Waliuawa, kwa kuchinjwa, na ngozi yao haikuwepo."

Wizi wa punda kama huu umezidi kuenea katika sehemu nyingi za Afrika - na katika sehemu nyingine za dunia ambazo zina idadi kubwa ya wanyama hawa wanaofanya kazi. Kitendo alichofanyiwa Steve - na punda wake - ni shehemu ya uharifu ynaofanyika katika biashara yenye utata ya kimataifa ya ngozi ya punda.

f

Chanzo cha picha, THE DONKEY SANCTUAR

Maelezo ya picha, Uchinjaji na usafirishaji wa ngozi za punda unaweza kupigwa marufuku kote barani Afrika

Asili ya biashara ya wanyama hawa ni maelfu ya maili kutoka nchini Kenya. Nchini Uchina, dawa ya jadi ambayo imetengenezwa na protini na madini ya Amino Acid (gelatin) yanayopatikana kutoka kwenye ya punda inahitajika sana. Dawa hii inaitwa Ejiao.

Inaaminika kuwa inaimarisha afya na kuhifanya ujana. Ngozi za punda huchemshwa ili kutoa gelatin, ambayo hutengenezwa kuwa poda, vidonge au kimiminika au huongezwa kwenye chakula.

Wanaharakati dhidi ya biashara hiyo wanasema kwamba watu kama Steve - na punda wanaowategemea - ni waathiriwa wa mahitaji yasiyo endelevu ya kiungo cha jadi cha Ejiao.

Katika ripoti mpya ya Hifadhi ya Punda, ambayo imefanya kampeni dhidi ya biashara hiyo tangu 2017, inakadiria kuwa duniani kote angalau punda milioni 5.9 huchinjwa kila mwaka ili kuisambaza. Na shirika lmsaada linasema kuwa mahitaji yanaongezeka, ingawa BBC haikuweza kuthibitisha takwimu hizo kwavyanzo huru.

Ni vigumu sana kupata picha sahihi ya ni punda wangapi wanauawa ili kwa ajili ya kuuzwa kwa ajili ya dawa ya Ejiao.

w

Chanzo cha picha, THE DONKEY SANCTUAR

Maelezo ya picha, Ejiao ni dawa ya zamani ambayo hutumika kwa njia ya chakula, kimiminika au vidonge
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Barani Afrika, ambako karibu theluthi mbili ya punda milioni 53 duniani wanaishi, kuna sheria kadhaa. Usafirishaji wa ngozi za punda ni halali katika baadhi ya nchi na haramu katika nchi nyingine. Lakini mahitaji makubwa na bei ya juu ya ngozi huchochea wizi wa punda, na Hifadhi ya Punda inasema imegundua wanyama wakihamishwa kuvuka mipaka ya kimataifa ili kufikia maeneo ambayo biashara hiyo ni halali.

Hata hivyo, hivi karibuni kunaweza kuwa na mabadiliko kwani serikali ya kila taifa la Afrika, na serikali ya Brazil, ziko tayari kupiga marufuku uchinjaji na usafirishaji wa punda ili kukabiliana na kupungua kwa idadi ya punda.

Solomon Onyango, ambaye anafanya kazi katika Hifadhi ya Punda mjini Nairobi, anasema: "Kati ya 2016 na 2019, tunakadiria kuwa karibu nusu ya punda wa Kenya walichinjwa [ kwa ajili ya biashara ya ngozi]."

Hawa ni wanyama wale wale wanaobeba watu, bidhaa, maji na chakula - uti wa mgongo wa jamii maskini, za vijijini. Kwa hivyo ukubwa na ukuaji wa kasi wa biashara ya ngozi umewatia hofu wanaharakati na wataalam, na kuhamasisha watu wengi nchini Kenya kushiriki katika maandamano ya kupinga biashara ya ngozi.

Pendekezo la kupiga marufuku mauzo ya punda barani Afrika kwa muda usiojulikana liko kwenye ajenda katika Mkutano wa Wakuu wa Umoja wa Afrika, unaotarajiwa kuwajumuisha viongozi wote wa matiafa tarehe 17 na 18 Februari.

g

Chanzo cha picha, FAITH BURDEN

Maelezo ya picha, Wanawake na wasichana ndio hubeba mizigo wakati punda anapoibiwa

Akitafakari kuhusu uwezekano wa kupigwa marufuku barani Afrika, Steve anasema anatumai itasaidia kuwalinda wanyama hao, "l a sivyo kizazi kijacho hakitakuwa na punda".

Lakini je, marufuku kote barani Afrika na Brazili inaweza kubadilisha biashara mahali pengine?

Wazalishaji wa dawa ya Ejiao walikuwa wakitumia ngozi kutoka kwa punda waliotoka Uchina. Lakini, kulingana na Wizara ya Kilimo na Masuala ya Vijijini huko, idadi ya punda nchini ilishuka kutoka milioni 11 mwaka wa 1990 hadi chini ya milioni mbili mwaka wa 2021. Wakati huo huo, Ejiao ambayo ilikuwa kama kipodozi cha kawaida iligeuka na kuwa maarufu, maarufu kote.

Kampuni za Kichina zilitafuta bidhaa zao za ngozi nje ya nchi. Machinjio ya punda yalianzishwa katika sehemu za Afrika, Marekani Kusini na Asia.

Katika Afrika, hii ilisababisha vuta ni kuvute kuhusu biashara hiyo.

f

Chanzo cha picha, THE DONKEY SANCTUARY

Maelezo ya picha, Punda wanaofanya kazi ya kuvuta mkokoteni kwenye machimbo

Nchini Ethiopia, ambapo ulaji wa nyama ya punda ni mwiko, moja ya vichinjio viwili vya punda nchini humo vilifungwa mwaka 2017 kutokana na maandamano ya umma na vilio vya watu wenye mitandao ya kijamii.

Nchi zikiwemo Tanzania na Ivory Coast zilipiga marufuku uchinjaji na usafirishaji wa ngozi za punda mwaka 2022, lakini nchi jirani na Uchina Pakistan inaikubali biashara hiyo. Mwishoni mwa mwaka jana, ripoti za vyombo vya habari huko zilipigia debe taarifa kuhusu "zizi rasmi la punda" la kwanza nchini humo kukuza "baadhi ya mifugo bora".

Na ni biashara kubwa. Kulingana na msomi wa uhusiano kati ya China na Afrika Profesa Lauren Johnston, kutoka Chuo Kikuu cha Sydney, soko la Ejiao nchini China liliongezeka thamani kutoka takriban $3.2bn (£2.5bn) mwaka wa 2013 hadi takriban $7.8bn mwaka wa 2020.

Imekuwa wasiwasi kwa maafisa wa afya ya umma, wanaharakati wa ustawi wa wanyama na hata wachunguzi wa uhalifu wa kimataifa. Utafiti umebaini kuwa shehena za ngozi za punda hutumika kusafirisha bidhaa nyingine haramu za wanyamapori.

Kwa viongozi wa mataifa, kuna swali la msingi: Je, punda wana thamani zaidi kwa uchumi unaoendelea wakiwa wamekufa au wakiwa hai?

g

Chanzo cha picha, THE DONKEY SANCTUARY

Maelezo ya picha, Wanaharakati dhidi ya biashara ya ngozi wanasema ni ya kinyama na haiwezi kudumu

“Watu wengi katika jamii yangu ni wakulima wadogo na wanatumia punda hao kuuza bidhaa zao,” anasema Steve. Hupata pesa kwa kuuza maji ili kulipia karo za shule kusomea udaktari.

Faith Burden, ambaye ni daktari mkuu wa wanyama katika Hifadhi ya Punda, anasema kwamba wanyama hao "ni asili kabisa" kwa maisha ya mashambani katika sehemu nyingi za dunia. Hawa ni wanyama wenye nguvu, wanaoweza . "Punda ataweza kwenda labda kwa masaa 24 bila kunywa maji na anaweza kurejesha maji haraka sana bila shida yoyote."

Lakini kwa sifa zao zote, punda hawazaliani kwa urahisi au kwa haraka. Kwa hivyo wanaharakati wanahofia kwamba ikiwa biashara haitapunguzwa, idadi ya punda itaendelea kupungua, na kuwanyima watu maskini zaidi njia ya kujikimu kimaisha na kuwanusuru wake zao na kazi ngumu za kubeba mizigo.

Bw Onyango anaeleza: "Hatukuwahi kufuga punda wetu kwa ajili ya kuwachinja kwa wingi."

Profesa Johnston anasema kwamba punda "wamekuwa njia ya usafiri wa maskini" kwa milenia. "Wanabeba watoto, wanawake. Walimbeba Mariamu alipokuwa na mimba ya Yesu," anasema.

g

Chanzo cha picha, BROOKE

Maelezo ya picha, Wengine wana wasiwasi kwamba, ikiwa biashara haitazuiliwa, kizazi kijacho hakitapata punda

Wanawake na wasichana, anaongeza, hupata kubwa kwa kubeba mizigo mikubwa wakati mnyama huyo anapochukuliwa. "Punda akishaondoka, basi wanawake wanakuwa punda ," anaeleza. Na la kusikitisha kuhusu hilo ni kwamba Ejiao huuzwa hasa kwa wanawake matajiri wa Uchina.

Ni dawa ambayo imekuwa ikitumika kwa maelfu ya miaka, inaaminika kuwa na faida nyingi kuanzia kuimarisha damu hadi kusaidia usingizi na kuongeza uwezo wa uzazi. Lakini ilikuwa kipindi cha TV cha 2011 cha Kichina kiitwacho Empresses in the Palace - hadithi ya kubuni ya mahakama ya kifalme - ambacho kiliibua wasifu wa suluhisho la dawa hiyo

Prof Johnston anaeleza kuwa . "Wanawake katika tamthilia hiyo walitumia Ejiao kila siku ili kubaki warembo na wenye afya - kwa ajili ya ngozi zao na kuimarisha uwezo wao wa kuzaa. bidhaa hii ikawa ni bidhaa ya hali ya juu ya wanawake . Cha kushangaza, hilo sasa linaharibu maisha ya wanawake wengi wa Kiafrika."

f

Chanzo cha picha, ALAMY

Maelezo ya picha, Tamthilia ya Kichina ya 'Empresses in the Palace' iliangazia dawa ya ngozi ya punda Ejiao

Steve, mwenye umri wa miaka 24, ana wasiwasi kwamba, alipopoteza punda wake, alipoteza udhibiti wa maisha na riziki yake. "Nimekwama sasa," anasema.

Likifanyaka kazi na shirika la misaada la ustawi wa wanyama mjini Nairobi, shirika la hisani la Brooke linafanya kazi kutafuta punda kwa ajili ya vijana - kama Steve - ambao wanawahitaji kupata kazi na elimu.

Janneke Merkx, kutoka Hifadhi ya Punda, anasema kadiri nchi zinavyoweka sheria za kuwalinda punda wao, "ndivyo itakavyokuwa ngumu zaidi".

f

Chanzo cha picha, VICTORIA GILL/BBC

Maelezo ya picha, Janneke Merkx akiwa na mmoja wa punda kwenye zizi la Devon

"Tunachotaka kuona ni kwa kampuni za Ejiao kuacha kuagiza ngozi za punda na kuwekeza katika njia mbadala endelevu - kama vile ufugaji wa kuzalisha collagen katika maabara. Tayari kuna njia salama na nzuri za kufanya hivyo."

Faith Burden, naibu mtendaji mkuu wa Hifadhi ya Punda, anaiita biashara ya ngozi ya punda "isiyo endelevu na isiyo ya kibinadamu".

"Zinaibiwa, kuna uwezekano wa kutembea mamia ya maili, kushikiliwa kwenye zizi lililojaa watu na kisha kuchinjwa mbele ya macho ya punda wengine," anasema. "Tunahitaji kuzungumza dhidi ya hili."

f

Chanzo cha picha, BROOKE

Maelezo ya picha, Steve sasa ana punda mpya ambaye anasema atamsaidia kufikia ndoto zake

Brooke sasa amempa Steve punda mpya, jike ambaye amempa jina la Joy Lucky, kwa sababu anahisi kuwa mwenye bahati na furaha kuwa naye.

"Ninajua kuwa atanisaidia kufikia ndoto zangu," anasema. "Na nitahakikisha kwamba analindwa."

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi