Madhehebu ni nini na kwa nini watu hujiunga nayo?

x

Chanzo cha picha, EPA

Vifo vya waumini zaidi ya 80 wa dhehebu lenye utata nchini Kenya, ambao miili yao iligunduliwa katika makaburi ya pamoja baada ya kudaiwa kushawishiwa kujiua kwa njaa, vimedhihirisha hatari ambayo mashirika yaliyokithiri yanaweza kusababisha.

"Kuna dhehebu karibu kila mahali ulipo duniani," Dkt Alexandre Stein, mwanasaikolojia anayeishi Uingereza aliyebobea katika itikadi kali na mahusiano mengine hatari ya kijamii, aliambia BBC.

Vikundi kama vile Kanisa la Good News International, ambalo linaaminika kuwa ndilo lililosababisha mkasa huo nchini Kenya, hutenda kazi kote duniani na si mara zote hutegemea dini.

Kile wote walicho nacho ni uwezo wa kuvutia wafuasi - na hatimaye kufanya iwe vigumu sana kwa watu kujiondoka.

Dhehebu ni nini?

Jumuiya ya Kisaikolojia ya Marekani (APA) inafafanua dhehebu kama "kundi la kidini lenye sifa ya imani isiyo ya kawaida au ya kutatanisha, iliyotengwa na ulimwengu wa nje, na muundo wa kimabavu".

Ke

Chanzo cha picha, Getty Images

Ingawa ibada mara nyingi ni za kidini, zinaweza pia kujihusisha na masuala mengine, kama vile siasa.

"Ni imani potofu kuwa itikadi kali zipo tu katika dini na msimamo mikali" Richard Turner mshauri anayefanya kazi na washiriki wa sasa na wa zamani wa itikadi kali ameeleza.

"Sehemu yako ya kazi inaweza kuwa kama dhehebu kama una shurutishwa kufanya mambo kama vile kufanya kazi mara kwa mara kwa muda mrefu," aliongeza, pia akibainisha kuwa baadhi ya vikundi vya masoko vya ngazi mbalimbali vinaendekeza mbinu za kuajiri zinazofanana sana na madhehebu.

th

Ni nani anajiunga na dhehebu?

Dk Stein alisema watu hawastahili kuwahukumu watu ambao ni waathirika wa Madhehebu, hasa elimu yao na ujuzi wa kijamii.

"Watu wanawakemea wale wanaojiunga na madhehebu tata wakisema ni matokeo ya mtu kuwa mjinga na maskini, lakini utafiti wa madhehebu hayo unaonyesha vingine."

Viongozi wa madhehebu, aliongeza, wanataka kuajiri "watu wenye tija na wenye akili", kwa sababu wana uwezekano mkubwa wa kuleta rasilimali kwa ajili ya kikundi.

"Madhehebu hayataki watu ambao wangelazimika kuwatunza."

Dk Stein alionya kuwa moja ya hadithi zinazozunguka madhehebu ni kwamba watu wanajiunga nayo kwa kujua.

Richard Turner

Chanzo cha picha, Richard Turner

"Hawatangazi kabisa 'njoo ujiunge na dhehebu letu'. Mwitikio mwanzoni huwa mzuri ."

Hata hivyo, Dk Stein anasema kwamba misiba inayohusisha idadi kubwa ya vifo, kama tukio la hivi majuzi nchini Kenya, si ya kawaida katika mienendo ya madhehebu ya kidini.

"Siyo kwamba viongozi wa madhehebu walikuwa na nia ya kupatu watu hao wote ili kuuawa."

Dk Stein alisema hili halikuwa lengo la awali la Heaven's Gate, vuguvugu la kidini la Marekani ambalo liligonga vichwa vya habari vya kimataifa mwaka 1997 wakati wanachama 39 walipokufa katika mapatano ya kujitoa mhanga wakiamini kwamba wataokolewa na kufufuliwa na wageni.

"Marshall Applewhite, kiongozi wa madhehebu, aliamini kuwa ana saratani na alitaka watu hao wote kufa pamoja naye.

"Kujiua na mauaji yatatokea tu ikiwa ndivyo kiongozi anafikiria wakati huo."

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Unyonyaji na unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, ni hatari kubwa inayowakabili waathiriwa.

Kwa nini viongozi wa madhehebu wana ushawishi mkubwa?

Katika masomo yake ya tabia za kitamaduni, Dk Stein amegundua kwamba viongozi ni watu wenye mvuto ambao mara nyingi hutokana na uzoefu kama huo ambapo walijifunza jinsi ya kutumia mbinu za ushawishi kukusanya wafuasi.

"Wanajifunza hila na kuendelea wakati wanapofikiri wanaweza kufanya mambo peke yao," alisema.

"Viongozi wa madhehebu sio wajinga. Kwa kweli, wana akili nyingi na wenye nguvu, kwa sababu sio rahisi kuongoza dhehebu."

Viongozi wa madhehebu mengi ni wanaume, ingawa mtu mmoja mashuhuri alikuwa Valentina de Andrade, mwanasiasa wa Brazil ambaye aliongoza kikundi kiitwacho Superior Universal Lineage ambacho kilichunguzwa na kuachiliwa huru katika miaka ya 1990 kutokana na tukio lililohusisha mfululizo wa mauaji ya watoto.

Kwa nini watu wasiondoke?

Kulingana na Turner, ni "rahisi sana" kwa mtu kuvutiwa kwa sababu viongozi wa madhehebu wana uwezo mkubwa wa "kulipua-mabomu" - jaribio la kushawishi mtu kwa maonyesho ya umakini na mapenzi.

watu

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ni jambo ambalo amepitia moja kwa moja. Mnamo mwaka wa 2013, alivutiwa na kile anachokiita "dhehebu la Kikristo la hipster" wakati akitafuta kazi ya kuwahudumia waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu.

"Haijalishi mtu ni tajiri kiasi gani, amefanikiwa au ana akili kiasi gani, kila mtu huwa na hali ya kuyumba wakati fulani katika maisha yake, kama vile kupoteza kazi, kufiwa, au mabadiliko mengine ya kutatanisha," Turner alieleza.

"Kisha wanatumia hali uliyo nayo ya kutojielewa, kujenga mazingira yasiofaa na kukupa dawa ya kulevya. Dhehebu lenye imani potofu siku zote hujaribu kukutenga na marafiki na wapendwa wako ili iwe rahisi kukutumia vibaya."

Mshauri alikumbuka jinsi wakati fulani alipokuwa "kwenye dhehebu" lake alivyokuwa akitoa ujira wake moja kwa moja kwa shirika, hivyo ndivyo ushawishi wao ulivyokwa umeathiri maisha yake.

"Nilijiondoa kwa sababu nilikuwa na matatizo mkubwa, na madhehebu kawaida hupoteza hamu ya wafuasi wakati hili inatokea."

Nitajuaje kama shirika ni dhehebu?

Turner anaonya kwamba si rahisi kwa watu kutambua kwamba shirika ni ibada. Lakini upekuzi rahisi wa mtandao unaweza kutoa vidokezo.

“Angalia watu wanasemaje kuhusu kundi fulani mtandaoni likiwemo kundi lenyewe, nimejifunza kuwa mmoja wao akiandika jambo lolote likijadili ‘mbona wao si wadhehebu’ ni kawaida yao,” alisema.

"Pia, kuwa mwangalifu ikiwa kikundi ulichojiunga kitaanza kusema mambo mabaya kuhusu marafiki na jamaa zako na kujaribu kukufanya ujitolee zaidi na zaidi katika shughuli, pamoja na zile zinazodai malipo."

Hata hivyo, mshauri anaamini kwamba njia bora zaidi ni kuzingatia hisia yako.

"Amini hisia yako," anasema.

Wataalamu kama Dk Stein na Turner ni wepesi kusema kwamba kuzuia ni rahisi zaidi kuliko tiba wakati wa kushughulika na imani potofu. Wote wawili wanataka kazi iliyoratibiwa zaidi na serikali ili kudhibiti madhehebu yenye utata.

"Hatuchukui hatua [zinazohitajika] kuelimisha watu kuhusu makundi hatari," Dk Stein alisema.

"Serikali huwa zinahofia kuzidhibiti, hasa zile zinazojionyesha kama makanisa."

th