Vita vya Ukraine: Je, Ukraine itamudu bila msaada wa Marekani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani imekata msaada wa kijeshi na kifedha kwa Ukraine ili kuzima uvamizi wa Urusi mwaka huu. Jeshi la Ukraine linapoteza huku huko Kyiv na Magharibi wakizungumza juu ya tishio la ushindi wa Vladimir Putin katika vita ambavyo ameanzisha dhidi ya Ulaya.
Kwa nini wafuasi wa Donald Trump katika Congress wanakataa kutenga dola bilioni 60 zilizoahidiwa na Joe Biden, pesa hizi ni muhimu kwa maisha ya Ukraine na nini cha kutarajia katika siku za usoni?
Hivi ndivyo tunavyoweza kujibu leo maswali manne makuu kuhusu usaidizi wa Marekani kwa Ukraine.
1. Je, mchango wa Marekani kwa Ukraine ni muhimu kiasi gani?
Zaidi ya miaka miwili ya vita, nchi za Magharibi ziliiahidi Ukraine euro bilioni 250 na tayari zimetenga karibu robo tatu ya fedha hizi, kulingana na hesabu ya wataalamu kutoka kituo cha utafiti wa Taasisi ya Kiel.
Mfadhili mkuu wa Ukraine dhidi ya uchokozi wa Urusi ni Ulaya, baada ya Putin kuanzisha vita vikubwa zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Marekani ilichukua jukumu muhimu katika usambazaji wa silaha hadi mapema 2024, wakati mgao wa mwaka jana ulipokauka. Sasa Marekani na Ulaya wana karibu usawa katika usaidizi wa kijeshi, na Ulaya iko mbele sana katika usaidizi wa kifedha.
Hivi ndivyo inavyoonekana katika nambari.
"Ili kuchukua nafasi kabisa ya msaada wa kijeshi wa Marekani mwaka 2024, Ulaya italazimika kuongeza maradufu kiwango cha sasa na kasi ya usambazaji wa silaha," kwa mujibu wa wachambuzi katika Taasisi ya Kiel.
Hili haliwezekani, hasa ikiwa tunazingatia takwimu za makadirio badala ya takwimu kamili za misaada. Zinaonesha kuwa Ulaya ina hali ya wasiwasi zaidi kuliko Marekani, na kwa hiyo ina kiwango cha chini cha usalama.
Hivi ndivyo nchi zinazopakana na Urusi, ambazo zimekuwa za kwanza kuteseka katika tukio la uvamizi wa ardhi wa Urusi, zilijitolea kusaidia Ukraine:
• Estonia - zaidi ya asilimia 4 ya Pato la Taifa
• Lithuania – asilimia 2
• Norway na Latvia – asilimia 1.7 kila moja
Marekani na Uingereza waliahidi mara kumi zaidi.
Usaidizi wao haukuzidi 0.32% na 0.55% ya Pato lao la Taifa, mtawalia, kulingana na Taasisi ya Kiel. Na mamlaka za Anglo-Saxon zinazochukiwa na Kremlin zilituma pesa nyingi sio kwa Kyiv, lakini kwa akaunti za watengenezaji wa silaha zao wenyewe, na hivyo kusaidia uchumi wao wenyewe.
2. Kwa nini Congress inakataa kutenga pesa?
Kuidhinishwa kwa msaada kunahitaji idhini ya mabaraza yote mawili ya Congress.
Bunge la Seneti linadhibitiwa na wafuasi wa Rais wa Democratic Biden, na Warepublican wana wabunge wengi katika Baraza la Wawakilishi.
Seneti ya Democratic iliidhinisha kifurushi cha usaidizi mapema Februari, na pamoja na Wanademocratic, nusu ya wachache wa Republican walipiga kura ya kuunga mkono. Mswada huo una uwezekano mkubwa wa kupitisha bunge la Republican kwa urahisi, lakini Spika Mike Johnson anakataa kuuleta kwenye kura.
Sababu ni upinzani kutoka kwa wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Trump, mgombea wa Republican katika uchaguzi wa rais wa Novemba. Wanadai kwamba mgao wa pesa kwa Ukraine uhusishwe na uhamiaji wa kuvuka mpaka wa Mexico au kutoa leseni ya uuzaji nje wa gesi.

Chanzo cha picha, Reuters
Kwa maneno mengine, dola bilioni 60 zilizoahidiwa Ukraine ziligeuka kuwa mateka wa mapambano ya ndani ya kisiasa ya wafuasi wa Trump na Wademocrat walio madarakani na Warepublican wastani katika upinzani. Matokeo yake hayatakuwa wazi hadi uchaguzi wa rais wa Marekani mnamo Novemba 2024.
3. Je, Ukraine itaishi bila msaada wa Marekani?
Kama Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema mwishoni mwa wiki iliyopita, Ukraine haiwezi kushinda vita bila msaada wa Marekani. Na iwapo atashindwa, basi Putin atashambulia nchi nyingine na kuanzisha vita vya tatu vya dunia, Zelensky aliongeza.
Kwa kukosekana kwa usaidizi wa Marekani, Waukraine wanapaswa kuokoa risasi, na hii ina manufaa makubwa kwa Putin, jenerali mkuu wa Marekani barani Ulaya alimuunga mkono Zelensky Jumatano.
"Ikiwa wengine watapiga risasi na wengine hawatapiga, basi yule ambaye hana cha kurudisha atapoteza," Christopher Cavoli, kamanda wa vikosi vya pamoja vya NATO huko Ulaya, alielezea hesabu ya mstari wa mbele wa vita kwa wabunge.
"Waukraine hawatashinda bila msaada wetu," Jenerali Cavoli alisema.
Jambo hilo sio tu kwa msaada wa kijeshi. Ukraine inahitaji si tu makombora, mizinga na ndege.

Chanzo cha picha, Reuters
Karibu kila kitu ambacho Ukraine inapata sasa huenda kwenye matumizi ya ulinzi.
Lakini hii ni nusu tu ya matumizi yote ya hazina. Vitu vyote vya amani, mishahara, pensheni, na kadhalika hufadhiliwa na wafadhili na wadai wa Magharibi.
Gazeti la biashara la FT liliandika mapema Machi kwamba matumizi ya jumla ya bajeti ya Ukraine kwa mwaka huu yamepangwa kwa dola bilioni 87, wakati mapato yanakadiriwa kuwa dola bilioni 46 tu.
Ikiwa nchi za Magharibi hazitafunga nakisi, italazimika kuchukua hatua chungu kama vile kubana matumizi ya kijamii, kuongeza ushuru, kujaribu kubinafsisha mali ya serikali na kuchapisha pesa.
Hata kama Wamarekani watafungua kimiujiza mfuko wa sasa wa msaada, mazungumzo juu ya ufadhili wa 2025 yataanza Oktoba hii - mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani. Hayaahidi chochote kizuri.
4. Ni lini kila kitu kitatatuliwa?
Msaada unazuiwa na wafuasi wa Trump katika Bunge la Wawakilishi.
Lengo lao ni kulemaza utawala wa Biden kabla ya uchaguzi wa Novemba, ili kumuonesha kama rais dhaifu na kuboresha nafasi ya Trump kushinda.

Chanzo cha picha, EPA
Wafuasi wa Trump wanamzuia Spika Johnson kuleta muswada huo kupigiwa kura.
Wa mwisho kujaribu kuwashawishi Wamarekani ni washirika wao wakuu, Waingereza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron alisafiri kwenda Washington wiki hii na ujumbe kuhusu umuhimu wa kuisaidia Ukraine.
Spika Johnson alikataa kukutana naye, akitaja ratiba yake kuwa yenye shughuli nyingi.
Cameron alimtembelea Trump kwanza, hata kabla ya kuelekea Ikulu. Lakini haiba yake haikutosha kubadili msimamo wa wafuasi wa Trump kuhusu suala la usaidizi kwa Ukraine, ambayo ilielezwa na Marjorie Taylor Greene, ambaye anawakilisha Georgia katika bunge la Congress, hata kabla ya ziara ya waziri mkuu mstaafu wa Uingereza.












