Bagaragaza, kijana anayewapatia mbwa 'mazishi ya kipekee'

G
Maelezo ya picha, Bagaragaza (mbele) akiwa na baadhi ya mbwa anaowafunza

Mkufunzi wa mbwa Daniel Bagaragaza anaonyesha furaha yake kwa kuwa karibu nao, kuwatunza, kushughulikia matibabu yao,huku yeye akijiita 'mbwa mkubwa'. Isitoshe, alinunua shamba na kulifanya kuwa kaburi la kuzika mbwa hao kwa heshima aliyosema wanastahili.

 Kutoa mafunzo kwa mbwa na kuwatunza ndiyo taaluma yake jijini Kigali ambapo watu wenye mbwa wanawaleta kwake na yeye anawafundisha kutii na kuishi vizuri na watu. Anawaita 'wanafunzi' wake, na anasema anawafundisha adabu-ikiwa kuna mbwa anayekufa Bagaragaza anahakikisha kwamba anazikwa ipasavyo ishara ya kuonyesha kwamba aliishi vizuri na mbwa huyo.

Katika miji, kama vile Kigali, watu ambao mbwa wao wanakufa bila kuwa na ardhi yao wenyewe huwa na wakati mgumu kupata mahali pa kuwazika.

Getty
Maelezo ya picha, Bagaragaza (mbele) na wakufunzi wa mbwa wasaidizi wake

Akizungumza ni kwa nini anapenda mbwa sana, alisema : "Nilipata kwamba mbwa ni mnyama wakuishi naye ambaye ni Rafiki mwaminifu’’

"Ninahisi kama nikiwa na mbwa 500 na kukaa katikati mwao -anayetaka maji au chakula nilkampa ... ni jambo kubwa sana kwangu ninapokuwa katikati ya mbwa, naweza kusema kwamba mimi ndiye mbwa mkuu."

 Ijapokuwa mbwa wana manufaa sana majumbani, Bagaragaza anasema kuwa anasikitishwa na wale wasiowathamini, kuwatesa kwa kuwanyima chakula ,kutowatibu wanapogonjwa na kuwazika vibaya wanapokufa.

Hii ndiyo sababu alichukua uamuzi usio wa kawaida kununua ardhi kwa kitita cha franga milioni 17 takriban elfu 17 kwa ajili ya kaburi la mbwa peke yake.

 Anasema baada ya kujiunga na taaluma ya kufunza mbwa huko Kigali, alianza kushtushwa na kitendo cha jinsi wanavyotupwa ovyo mitaani au vichakani wanapofariki.

g
Maelezo ya picha, Bagaragaza na wanaume wengine wakienda kumzika mbwa aliyekufa katika makaburi yao huko Birembo mjini Kigali

Inanitia wasiwasi wakati mwanafunzi [mbwa] niliyemfundisha wakati maisha yake duniani yanapofikia mwisho...[kufa] wanamchukua kwenye mfuko na kwenda kumtupa taka,

Alisema: "Hapo ndipo nilipofikiria juu ya jambo hili [makaburi ya mbwa], na pia nitoe mchango wangu wa kulinda mazingira’’

Kumuaga Rafiki kwa heshima

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sheria ya makaburi nchini Rwanda,inaamua tu jinsi ya kuzika watu,haina kipengele hata kimoja kinachohusu Wanyama wanaoishi na watu kama mbwa.Pia ni wakati ambapo idadi halisi ya mbwa wanaoishi majumbani haijulikani.

Katika hafla ndogo ya mazishi ya mbwa aitwaye Maxi ambaye alikuwa na umri wa miaka 8, Bagaragaza alisindikizwa na watu wengine.

Gratien Munyentwari, kijana aliyefuatana na Bagaragaza, alikuwa amebeba msalaba, je mbwa huyu alikuwa Mkristo?

"[Msalaba] Ni ishara ya kukumbuka tulipoacha mbwa wetu." Hivyo ndivyo Munyentwari, ambaye pia anapenda mbwa, alivyoeleza.

Alisema, "mimi pia nilihuzunika sana ndipo nikasema 'nisipobeba msalaba ili niweze kutofautisha mbwa huyu na wengine nitakuwa nimefanya jambo baya'." Mara tu nilipoweka msalaba kwenye kaburi lake nilijihisi napumzika moyoni.”

Mwanamume mwenye umri wa miaka 70 ambaye alikuwa karibu na makaburi akiwatazama wakimzika mbwa, aliambia BBC kuwa hilo ni jambo zuri.

Akasema Mbwa walikufa wakawaweka kwenye mfereji huku na kule, mvua inaponyesha mizoga ya mbwa hutiririka hadi mtoni ambapo watu huchota maji ya kunywa lakini tukio hili sasa lilitufurahisha kupata makaburi ya mbwa.

G
Maelezo ya picha, Mmoja wa waliokuja kumzika mbwa huyu alibeba msalaba kukumbuka mahali walipomzika

Rwanda kama sehemu nyingi duniani , mbwa ni mnyama anayeishi na watu tangu historia yao ianze kuandikwa, kulingana na wanahistoria.

Katika maeneo mengi Rwanda mbwa huingia katika Maisha ya watu ambapo anajulikana kama 'rafiki mwaminifu'. Kuna wale tu ambao hawathamini uhusiano huo, kulingana na Bagaragaza.

Anataka mambo kubadilika kwamba kubadilika, uaminifu wa mbwa ukazawadiwa kwa kutunzwa vizuri, matibabu, huduma na mazishi mazuri wakati wa kifo.

Ingawa hakuna makaburi mengine ya mbwa yanayojulikana nchini Rwanda, sasa kuna kliniki tatu za mbwa nchini humo.