Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, watoto wanaotokana na DNA za watu watatu tofauti wanahaki ya kujua waliochangia kuzaliwa kwao?
Idadi ya watoto wanaozaliwa kwa msaada wa mbinu inayotajwa kitaalamu kama pioneering technique ambapo huzaliwa kutokana na maumbile kutoka kwa watu watatu inaongezeka. Lakini inafungua mjadala mpya juu ya haki gani wanapaswa kuwa nazo watoto hawa.
Utaratibu wa uzazi wa msingi unaotumia vinasaba (DNA) kutoka kwa watu watatu ili kuzuia magonjwa mbalimbali 'mitochondrial' yenye kuathiri watoto imesababisha kuzaliwa kwa watoto kadhaa wenye afya katika nchi nyingi duniani kote - ikiwa ni pamoja na, hivi karibuni, nchini Uingereza.
Mbinu hiyo mpya, inayoitwa tiba ya upandikizaji ya mitochondrial, inatoa matumaini kwa wanandoa ambao wamepoteza watoto kwa sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa adimu. Lakini pia imekabiliwa na upinzani, kwa sehemu kwa sababu ya wasiwasi mpana kuhusu michakato inayohusisha marekebisho ya kijeni kwa wanadamu.
Huku baadhi ya watoto wa kwanza kuzaliwa kwa kutumia mbinu hii ya 'mitochondrial' wakifikisha umri wa miaka saba mwaka huu, mbinu hiyo inazidi kusambaa duniani, wadhibiti na wazazi pia wanakabiliwa na maswali ya kimaadili kuhusiana na utambulisho na asili ya watoto wanaozaliwa.
Swali moja muhimu linaloulizwa ni kama watoto wanapaswa kuwa na haki ya kujua utambulisho watu waliohusika kuchangia vinasaba kwa mbinu ya mitochondrial vilivyowezeshwa wao kupatikana.
Wataalamu wanasema kwamba utafiti uliopo juu ya njia zilizothibitishwa zaidi za utungaji mimba unaosaidiwa na wafadhili au waliojitolea kuchangia, kama vile manii na uchangiaji wa yai unaweza kusaidia kujibu maswali hayo - na kutafuta njia bora ya kuhakikisha ustawi wa kihisia wa watoto wanaozaliwa kwa njia hiyo.
Mitochondria ni sehemu maalum ndani ya seli zetu ambazo hubadilisha nishati inayopatikana kutoka kwenye chakula kuifanya kuweza kutumika kuipa nguvu miili yetu. Lakini haiwezi kufanya hivyo ikiwa inavitu ambavyo vinasababisha magonjwa. Kawaida tunarithi mitochondria kutoka kwa mama zetu, kama mama amebeba mitochondria yenye hitilafu anaweza kuirithisha kwa watoto wake.
Tiba ya upandikizaji wa Mitochondrial ni aina ya IVF inayochanganya DNA kutoka kwa mama na baba ndani ya yai lililotolewa na mwanamke mwingine ambayo ina mitochondria yenye afya, ambayo haina shida wala hitilafu yoyote.
Mimba itakayopatikana itakuwa imebeba Vinasaba ama DNA kutoka kwa wazazi wawili, lakini pia hubeba kiasi kidogo cha vinasaba vya urithi kutoka kwa mtu wa watu aliyechangia yai - karibu 0.1%.
Wataalamu wanasisitiza kwamba mtoto atakayezaliwa haipaswi kuchukuliwa kama mtoto aliyetokana na "wazazi watatu", anapaswa kutambulika kama mtoto wa "watu watatu": Wana wazazi wawili, na mfadhili ama mchangiaji mmoja.
Ulimwenguni kote, sheria zinazozunguka utaratibu huo bado zinaendelea. Uingereza imeanzisha sheria na kanuni za kuruhusu mbinu za kubadilisha mitochondrial, na inasalia kuwa mojawapo ya nchi chache ambazo zimeihalalisha waziwazi mfumo huo wa uzazi. Australia pia ilihalalisha utaratibu huo mnamo 2022.
Nchini Marekani, utaratibu huo umepigwa marufuku kabisa: utafiti wa kimatibabu kwa kutumia mbinu za upandikiza wa mitochondrial kwa wanadamu hauwezi kuendelea kisheria baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa kuelezea wasiwasi wake wa usalama.
Nchini Canada, utaratibu huu pia umepigwa marufuku. Hata hivyo, watu wamepata njia za kukwepa vizuizi hivyo kwa kuhusisha nchi zilizo na sheria nyepesi au zisizo na sheria. Mnamo 2016 alizaliwa mtoto wa kiume wa wanandoa raia wa Jordani waishio MArekani kwa njia hii ya mitochondrial, ambayo sehemu ya mchakato wake ilifanyika Mexico.
Tofauti na DNA ya wazazi wawili, DNA ya mitochondrial ya wafadhili yenyewe hairithishi ama haileti athiri kwa vitu kama nywele au rangi ya macho, au utu. Tofauti hii, na ukweli kwamba ni sehemu ndogo tu ya nyenzo za kijeni kutoka kwa wafadhili wa mitochondrial, imekuwa na matokeo muhimu.
Nchini Uingereza, mwanamke ambaye hutoa mayai yake kwa ajili ya kupandikizwa kwa njia hii ya mitochondrial hachukuliwi kuwa mzazi wa kimaumbile wa mtoto atakayezaliwa, na mtoto huyu hawezi kuomba kumjua mwanamke aliyetoa ama changia yai lake. Kuanzia umri wa miaka 16, mtoto anaweza kufanya hivyo, kwa kufahamishwa tu taarifa chache ambazo hazitamtambulisha aliyechangia mitochondrial, atajua vichache tu kama vile maelezo kuhusu historia ya kimatibabu ya mtoa yai na historia ya kimatibaby ya familia ya mtoa yai.
Kichume chake uchangiaji wa manii na yai, sasa ni jambo lililo wazi kwa utambulisho nchini Uingereza pekee (mtoto anaweza kutuma maombi ya kujua utambulisho wa mchangiaji manii ama yai ama wote akiwa na umri wa miaka 18).
John Appleby, mhadhiri wa masuala ya tiba katika Chuo Kikuu cha Lancaster, nchini Uingereza, hakubaliani na uamuzi wa Uingereza kuzuia mchangiaji wa mitochondrial kutojulikana kisheria. Anasema kuwa watoto waliopatikana kwa kupitia mchango wa mitochondrial wanapaswa kuwa na haki ya kujua utambulisho wa mtu aliyechangia kuzaliwa kwao, kama wanavyofanya nchini Uingereza katika kwa upandikizaji wa manii na yai. Ni ruhusa kwa waliochangia manii na yai kutambulika lakini mtu wa tatu hairuhusiwi kutambulika.
“Ushahidi wa kisaikolojia hadi sasa unaonyesha kuwa baadhi ya watu walitunga mimba kwa kutumia mayai, mbegu za kiume au viinitete, wanaona ni muhimu kujua taarifa za kutambua wafadhili wao,” anasema. "Wana tabia ya kueleza sababu kadhaa kwa nini, kuanzia kutaka kumshukuru mfadhili 'mtu aliyemchangia, kutaka kutafuta ndugu wengine, au kwa sababu ni muhimu kujenga uhusiano na wafadhili wao na ikiwezekana kukutana nao."
Utafiti kuhusu familia zilizoundwa kwa usaidizi wa uchangiaji wa manii unatoa mwanga zaidi juu ya manufaa ya uwazi, na inaweza kusaidia inapokuja katika kufikiria jinsi mtoto wa watu watatu wa IVF aina ya mitochondrial anaweza kuhisi siku moja kuhusu mtu wa tatu aliyemchangia.
"Nadhani ni jambo kubwa kwamba wazazi ambao kwa kawaida wangepoteza mtoto kutokana na ugonjwa wa mitochondrial sasa wana fursa ya kuzaa mtoto mwenye afya," anasema Nanette Gartrell, daktari wa akili na mtafiti mkuu katika Utafiti wa Kitaifa wa Familia ya wapenzi wa jinsia moja (lesbian) nchini Marekani. Utafiti huo ulioanza katika miaka ya 1980, umefuata kundi la akina mama wawanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ambao walipata watoto kupitia uchangiaji wa mbegu za kiume, na pia kufuata ukuaji na ustawi wa watoto hadi utu uzima. Gartrell anasema matokeo ya utafiti yana mafunzo muhimu zaidi, kwa mfano linapokuja suala la uwazi kuhusu njia zlizotumika kupatikana kwa watoto.
"Watoto waliotungwa mimba na wazazi walio wachache kwa njia ya usaidizi wa teknolojia ya uzazi wanajua kuhusu mimba zao tangu utotoni," anasema Gartrell. Akina mama katika utafiti, kwa mfano, sikuzote walikuwa wazi na kuwaeleza watoto wao kuhusu asili yao. Wakiwa watu wazima, takribani nusu ya watoto waliotungwa mimba katika utafiti huo waliripoti uhusiano mzuri na wafadhili wao (watu waliochangia manii), huku 20% walitaka kuwa karibu zaidi.
Kwa sasa, mfumo huu mpya wa upandikizaji wa mitochondrial ni kama kujenga msingi mpya kabisa au kuleta kitu kipya kabisa - kuunda aina mpya kabisa ya mwanadamu. Lakini kama tafiti hizi za teknolojia zingine za uzazi zinavyopendekeza, watoto wenyewe wanaweza kutoshtushwa sana na asili yao kuliko umma.
Kwa muda gani umma utaikubali mbinu hii inayokua kwa kasi ya uzazi, hata hivyo, inaweza kuendelea kutofautiana kutoka nchi hadi nchi - kwa vile jamii bado zinaonyesha mitazamo tofauti kuhusu njia ambayo angalau yenye muda mrefu ya upandikizaji wa kawaida wa mbegu na manii peke kutoka kwa watu wawili (IVF) na si watatu.