Hifadhi ya maji yagunduliwa katika miamba ya sayari ya Mars

Mchoro unaoashiria chombo cha Nasa kikiwa kazini

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Ugunduzi huo unatokana na uchanganuzi wa data kutoka kwa chombo cha Nasa, ambacho kilichukua kipima tetemeko hadi Mars.
    • Author, Victoria Gill
    • Nafasi, Mwandishi wa habari za Sayansi, BBC News
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Wanasayansi wamegundua hifadhi ya maji kwenye sayari ya Mars - ndani ya miamba wa sayari hiyo.

Ugunduzi huo unatokana na uchambuzi mpya wa data kutoka kwa chombo cha Nasa kilichochunguza matukio ya katika sayari hiyo mnamo 2018.

Chombo hicho kilitumia kipima mtetemo, ambacho kilirekodi mitetemoko ya miaka minne - mitetemeko ya Mars - kutoka ndani kabisa ya Sayari Nyekundu.

Kuchambua matetemeko hayo - na jinsi sayari inavyosonga - kulibaini "ishara za uwepo" wa maji.


Picha ya mchanganyiko inayoonyesha ukubwa unaolingana wa sayari za Dunia na Mars

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Ujumbe wa Insight uliazimia kuchunguza mabadiliko ya sayari zenye miamba, ikiwa ni pamoja na Dunia na Mars

Ingawa kuna maji yaliyoganda kwenye nguzo za Mars na ushahidi wa mvuke katika angahewa, hii ni mara ya kwanza maji kupatikana kwenye sayari hiyo.

Matokeo ya uchunguzi yanachapishwa katika jarida la Majadiliano ya Chuo cha Kitaifa cha Sayansi .

Ujumbe wa kisayansi wa Insight uliisha mnamo Desemba 2022, baada ya chombo chao kukaa kimya akisikiliza "mapigo ya Mars" kwa miaka minne.

Wakati huo, uchunguzi huo ulirekodi zaidi ya matetemeko 1,319.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa kupima kasi ya mawimbi ya tetemeko la ardhi, wanasayansi wamegundua ni nyenzo gani wana uwezekano mkubwa wa kupita.

"Hizi ni mbinu zilezile tunazotumia kutafuta maji duniani, au kutafuta mafuta na gesi," alisema Prof Michael Manga, kutoka Chuo Kikuu cha California, Berkeley, ambaye alihusika katika utafiti huo.

Uchanganuzi huo ulifichua hifadhi za maji kwenye kina cha maili sita hadi 12 (km 10 hadi 20) kwenye sakafu ya sayari ya Mars.

"Kuelewa mzunguko wa maji ya Mars ni muhimu kwa kuelewa mabadiliko ya hali ya hewa, uso na mambo ya ndani," alisema mtafiti mkuu Dk Vashan Wright, kutoka Taasisi ya Scripps ya UC San Diego ya elimu ya mambo ya Bahari.

Prof Manga aliongeza kuwa maji ndiyo "molekuli muhimu zaidi katika kuchagiza mageuzi ya sayari". Ugunduzi huu, alisema, unajibu swali kuu la "maji yote ya Mars yalipotelea wapi?".

Uchunguzi wa uso wa Mars - pamoja na njia zake na mawimbi - unaonyesha kwamba, katika nyakati za kale, kulikuwa na mito na maziwa kwenye sayari.

Lakini kwa miaka bilioni tatu, imekuwa jangwa.

Baadhi ya maji hayo yalipotelea angani wakati Mars ilipopoteza angahewa yake. Lakini, Prof Manga alisema, hapa Duniani, "mengi ya maji yetu yako chini ya ardhi na hakuna sababu ya kwanini isiwe hivyo pia kwenye Mars".

Soma pia:
Picha ya karibu ya mto wa kale kwenye syari ya Mars

Chanzo cha picha, Nasa

Maelezo ya picha, Sayari ya Mars ina ushahidi wa mito ya kale na maziwa

Uchunguzi wa Insight ulifanikiwa tu kurekodi matukio ya moja kwa moja ya miamba iliyokuwa chini ya miguu yake, lakini watafiti wanatarajia kuwa kutakuwa na hifadhi sawa katika sayari. Ikiwa hilo litafanyika, wanakadiria kuwa kuna maji ya kutosha kwenye sayari ya Mars ambayo ukubwa wake unaweza kuwa zaidi ya nusu maili.

Lakini, wanaonyesha, eneo la maji haya ya chini ya ardhi ya Mars sio habari njema kwa mabilionea walio na mipango ya Mars kwani kuna viumbe wangine wanaweza kuyavamia.

"Yametengwa umbali wa kilomita 10-20 ndani ya miamba," aalisema Prof Manga.

"Kuchimba shimo lenye kina cha kilomita 10 kwenye Mars - hata kwa [Elon] Musk - itakuwa vigumu," aliiambia BBC News.

Ugunduzi huo unaweza pia kuashiria lengo lingine la utaftaji unaoendelea wa ushahidi wa viumbe hai kwenye sayari ya Mars.

"Bila maji, huna uhai," Prof Manga alisema. "Kwa hivyo ikiwa kuna mazingira ya kuishi kwenye Mars, basi yanaweza kuwa chini ya ardhi."

Maelezo zaidi:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi