Je ungekubali kupimwa uzani kabla ya kuingia katika ndege unayosafiria?

Chanzo cha picha, Finnar/Getty Images
Finnair imetangaza kuwa itawapima abiria kabla ya kupanda ndege zao.
Mapema wiki hii, kampuni hiyo ilitangaza kuwa itaanza kupima uzito wa abiria.
Katika taarifa, msemaji wa shirika la ndege Kaisa Tikkanen alisema: "hatua hiyo ilianza katika Uwanja wa Ndege wa Helsinki Jumatatu wiki hii."
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya kampuni hiyo ilisema: "Finnair itakusanya data za vipimo vya wateja na mizigo yao kabla ya kuingia katika ndege.
Salio ni la hiari na la siri, na data hiyo itatumika tu kuboresha hesabu ya mizani ya ndege ya Finnair".
"Hadi sasa, watumiaji 500 waliojitolea wameshiriki katika utafiti huo."
Kampuni hiyo ilisema kuwa kuchunguza uzani wa ndege hiyo, unaojumuisha "mizani ya mafuta, mifuko na mizigo, chakula, matangi ya maji, na bila shaka, wateja" ni sehemu ya kuifanya safari hiyo kuwa salama.
Abiria waliojitolea watapimwa pamoja na mizigo yao, na ni afisa wa huduma kwa wateja anayefanya kazi katika idara ya uzani ndiye atakayejua uzito wa mtu.

Chanzo cha picha, getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Data zitakazokusanywa hazitashirikishwa na data ya kibinafsi ya abiria kwa njia yoyote," kampuni hiyo ilisema.
Ingawa mashirika ya ndege yanafahamu uzito wa wahusika wengine wote, uzito wa abiria na mizigo yao huhesabiwa kwa kutumia wastani wa uzito uliotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (CAA).
Chaguo jingine ni kwa mashirika ya ndege kutumia vipimo vyao wenyewe au uzani wa kawaida uliofafanuliwa na Wakala wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Ulaya EASA.
Tangu 2018, Finnair imetumia uzani wa wastani unaoamuliwa na kiwango chake , lakini mamlaka inataka takwimu hizi kuimarishwa kila baada ya miaka mitano.
Ilisema ni wakati wa kukusanya data mpya ili kuboresha hesabu za mizani.
Suala hili limezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watu wakisema inaonekana ni suala la unene au ubaguzi dhidi ya watu wenye uzito mkubwa.
Jamii katika nchi za Ulaya na Magharibi kwa ujumla huona aibu ya kuwa mnene kupita kiasi na kuhusishwa na afya mbaya na ulaji kupita kiasi.
Kampuni hii sio ya kwanza kupendekeza mpango wa kupima abiria, Korean Air ilitangaza Agosti mwaka jana kuwa itawapima abiria kwenye ndege zake kabla ya kusafiri.

Chanzo cha picha, Getty images
Kama Finnair, kampuni ya Korea Air ilisema kwamba "abiria na mizigo yote itapimwa bila kujulikana, na data itashirikiwa na Wizara ya Ardhi, Miundombinu na Usafiri wa nchi".
Ikiwa abiria hawapendi data yao ya uzito ikusanywe, Korean Air inathibitisha kwamba wanaweza kujiondoa kwenye makubaliano hayo kwa kumjulisha mfanyakazi.
Ingawa wasafiri wengine wanaweza kushangazwa kuombwa kusimama kwenye mizani, uamuzi huu haufanywi na mashirika ya ndege - mara nyingi hufanywa na wadhibiti wa usafiri wa anga wa serikali.
Mapema mwaka wa 2023, kampuni ya ndege ya Air New Zealand ilitekeleza mpango sawa na huo kwa kupima baadhi ya wateja wanaosafiri kwa ndege kwenda nchi za kimataifa, kama vile safari za ndege za masafa marefu kati ya Auckland na New York.
"Tunajua kukaa kwenye mizani ni ngumu. Tunataka kuwahakikishia wateja wetu kwamba hakuna video inayoonekana popote. Hakuna anayeweza kuona kiwango chako, hata sisi," mwakilishi kutoka Air NZ, shirika la ndege la taifa alisema.
Baada ya data kukusanywa, husaidia mashirika ya ndege kufanya maamuzi kuhusu mahitaji ya mafuta na kusawazisha uzito wa ndege.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












